Habari wakubwa,

Natumai wote ni wazima na mnaendelea vyema katika ujenzi wa taifa, wakubwa nina issue naomba muitoe katika blog zenu ambayo inagusa kila mtanzania, bila uwoga wakubwa naomba muiweke maana blog zenu zimegeuka sauti ya wanyonge na wanyonge wanawategemea katika kuwatetea namna moja au nyingine, ujumbe ni kama ifuatavyo:

-------------------------

Hoja ya msingi:

Kutokana na kutokuwa na ufumbuzi mkubwa wa nishati ya kudumu ya Umeme nchini Tanzania na kushindwa kwa uendeshaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), ningeomba Serikali kuliangalia swala zima la nishati ya umeme kwa undani zaidi, kwanini nasema hivi, ni miaka 49 tangu Tanzania tupate uhuru lakini mpaka sasa leo hii Tanzania bado inakuwa na migawo ya umeme ya mara kwa mara miaka nenda rudi na sehemu nyingine kutokuwa na umeme kabisa na kubakia kwenye giza!!

Ni aibu kubwa kwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Serikali ya Tanzania, Viongozi wote wa Serikali pamoja na Taifa zima, Hauwezi kusema unataka uwe na Taifa lenye nguvu kiuchumi na kimaendeleo kama nchi haina nishati ya uhakika, utawezaje kushawishi wawekezaji waje nchini kuwekeza katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na maendeleo kama kuna giza!!

Hii inaonesha ni jinsi gani wahusika ktk ili jambo kutokuwa makini na kutojua kazi zao, miaka yote 49 wameshindwa kuweka mikakati thabiti ya muda mfupi na mrefu kuwezesha kulitokomeza tatizo ili??!!

Hivyo basi ningeliomba Serikali na Tanesco kuangalia yafuatayo:

Suluhisho:

A: Tungeomba Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) liweze kugawanywa eidha mara 2 au 3 ili kuzidisha ushindani pamoja na ufanisi wa Shirika kwenda kwa wateja wao ambao ni raia wa Tanzania na wengineo wasio watanzania.

Mfano, Miaka ya 1990’s Uingereza iliweza kufanya reform katika Nyanja mbali mbali ikiwemo usafiri ambapo British Rail baada ya kushindwa kufanya kazi vizuri iligawanywa ambapo matokeo yake yaliweza kuongeza ufanisi mkubwa ndani ya hiyo sekta, hivyo basi nasi tunaweza kufanya hivyo hivyo cha msingi ni kuwa waangalifu na mafisadi.

B: Serikali kuweka mtazamo na mikakati thabiti ya kuwezesha wizara ya nishati na Madini inatokomeza ili tatizo la umeme, mikakati hii iwe ya kudumu na ifanyiwe kazi kwa maana sioni sababu ya waziri wa nishati na Madini na wafanyakazi wote wa wizara ya nishati na Madini kulipwa mishahara mikubwa ambayo inatokana na kodi inayolipwa na Mtanzania na wakati huo huo kushindwa kutekeleza wajibu wa kazi zao na kushindwa kutokomeza tatizo la umeme nchini Tanzania!!

C: Serikali inatakiwa kuzidisha nguvu zake za kutafuta wawekezaji walio serious, wenye experience na wenye financial capabilities kuweza kuwekeza ktk sekta hii ya nishati na kuleta ushindani mkubwa katika hii industry ambapo itawezesha kudumisha huduma zinazotolewa na kuwezesha kutokomeza tatizo la umeme nchini Tanzania ambapo hizi kampuni za nje zitakuja na mitazamo tofauti mbali mbali ya kuweza kupambana na ili tatizo tulilo nalo.

D: Inasemakana kwamba Tanzania tuna vyanzo vingi vya Umeme vikiwemo mito, maziwa, upepo mwingi, makaa ya mawe, Gas, pamoja na Uranium, sasa sioni ni kwanini nchi kama Tanzania kushindwa ku-utilise hizi resources tulizo nazo ili kuwezesha Tanzania na Watanzania kupata ufumbuzi wa Umeme wa kudumu na kuzidisha chachu ya maendeleo nchini Tanzania!?

Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) mnafanya kazi gani na kushindwa kuwekeza millions of money ktk hizi Nyanja na kupata ufumbuzi wa tatizo la umeme Tanzania?? Mnashindwa ata kwenda kukopa nje au kushirikiana ku-invest pamoja na makampuni mengine ktk hizo nyanja??

Serikali mpo wapi mnashindwa kwenda kukopa nje ya nchi ili kuondoa tatizo la umeme Tanzania?? Tusidanganyane kwamba mnataka maendeleo nchini Tanzania kama mnashindwa ku-sort out ili tatizo la umeme once and for all!!??

Nendeni kakopeni katika institutions mbalimbali duniani na wapeni tenders watu walio serious watupatia solutions, mbona tunashindwa na nchi mbalimbali za Africa ambazo hazina matatizo kama sisi?? Kwanini Tanzania!!!!

Naipenda nchi yangu sana, napenda maendeleo ya nchi yangu sana lakini mwenendo tulio nao unanisikitisha sana tena sana, vijana wengi hawana kazi, vijana wengi hawana pesa, wananchi wengi hawana elimu, nchi haina maendeleo, na umeme pia mnawakatia hawa hawa wananchi na kushindwa kuwapa ufumbuzi wa kudumu, je mnaipeleka nchi hii kwenda wapi???

Hakuna uzalishaji bila umeme, hakuna maendeleo bila ya uzalishaji, hivyo kwa yoyote anayehusika katika ngazi za juu usomapo ujumbe huu ningeomba mtafute ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme nchini Tanzania ili kuzidisha maendeleo, uzalishaji, ukuaji wa uchumi, idadi ya wawekezaji kuongezeka na pia kuleta mwanga ndani ya watanzania waliokosa kila kitu.

Pia wewe mtanzania, ningeomba uweze kuongea na mwakilisha wako wa sehemu unayokaa haswa haswa wabunge wenu ili waweze kuwapigania na kuwatetea haki zenu ndani ya bunge na kuwezesha kupata ufumbuzi wa shida hii kubwa iliyokaa miaka 49!! Na kama ikiwezekana wahusika wawajibishwe maana sijawahi kuona Tanzania wahusika wanawajibishwa! Na kama wewe ni mbunge basi peleka hoja hii bungeni ili badala ya serikali kununua majenereta, watafute serious long term solutions!

Nawaomba mtoe comment zenu nyingi sana kwa uhuru maana nina uhakika wahusika wengi watasoma hii post ili nao wasikie kilio chenu.

Naomba niishie hapa maana nina uchungu mwingi kwa uzembe wa watu wachache wanao fanya raia zaidi ya Milioni 40 kuteseka kwa ili tatizo la umeme. Nilitaka kusahau, Sinza hatuna umeme wa kudumu zaidi ya wiki nzima!! Tanesco wanakata umeme kila dakika na kurudisha kila dakika watakavyo bila ya kujali kuungua kwa mamilioni ya gharama za vitu ambavyo wateja wao wanavyo.

Nashukuru.

Mtanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Kama Tanzania tunaweza kukubali kuwa na makampuni mengi ya simu, tumeshindwa nini kuleta hata kampuni lingine la Umeme, Train na Airline?! Viongozi wanatuambia vitu vingi wanavyotaka kufanya, lakini wakirudi kwenye uongozi hakuna wanachofanya bali kula hela ya nchi.

    ReplyDelete
  2. Tatizo kubwa la viongozi wetu wa Tanzania hakuna kitu wanachochukuliaga serious hata siku moja kila siku ni ahadi na uzembe tu hata mtu akifa wanaona sawa tu hakuna shida.Na jingine ndugu mtoa mada tanzania kuna wataalamu wengi na naamini uwa wanatoa ushauri wao laknini tatizo ikionekana Taifa likakomboka na kuzuia miradi mingine ya wa wakubwa kamwe huo ushauri hauwezi chukuliwa kama endelevu.Wamekuwa watu wakutupa hadithi sana kuna kipindi umeme ulikosekana wakasema maji yamepungua,baadae maji yakajaa wakasema yamekuwa mengi wanataka kufungulia yapungue yaondoke,hii nchi yangu lakini mambo yanavyoenda inakera sana tena sana.Sijuiwanahiskuwa kiongozi ni kuvaa suti na kwenda kuweka mawe ya msingi tu bila kuwa na mtazamo wa kuona mbali?Jamani hii Tanzani ni ya kwetu wote sio nyinyi mawaziri na wabunge tu naomba muelewe hilo.Tuna vyanzo vingi sana vya umeme lakini viongozi hawataki kutumia lakini naamini tatizo sio pesa ni ubinafsi.Ni hayo tu kwa leo

    ReplyDelete
  3. mkuu ulichozungumza hapa mimi binafsi nimekikubali. ni aibu sana. na sio kama tuanasema aibu kwakuwa kumekuwa na udanganyifu na usanii sana kwenye nyanja za nishati na madini.. na naamini yote unayoyasema sio kama viongozi wetu hawayajui ila kama unavojuwa akili haipo kwenye kazi. akili siku zote zinahamia kwenye tumbo.hawajui kama technology inakuwa kwa kasi. umeme wa solar unaingia kwa kasi sana mpaka watu wakishapata sulhisho hilo ndio watatia akilini.

    ReplyDelete
  4. Dah! niko na nyie kwa asilimia zote,ukweli ni aibu kubwa kwa nchi kama tanzania kuwa na tatizo hili sugu la umeme kwa miaka mingi, viongozi mko wapi, mnafanya nini, mnafaida gani, si afadhali mfe tu tuchague wengine wenye mapenzi na nchi yao pamoja na raia wake???!!! au kwasababu nyie kwenu mgao haupiti? ama kweli kitanda usicho kilalia uwezi kujua kunguni wake!! tunahasila, uzalendo utatushinda halafu iwe taabu, ooohooo!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Mdau nakuunga mkono kwa ujumbe wako mzito,ila sikubaliani na wewe kuwa tatizo ni la viongozi,Tatizo lipo kwetu wenyewe,watanzania sisi ni wazembe,tunakubali kudanganywa na kupelekwa pelekwa kiraisi,sio umeme tu public service zote zimeoza,sasa kama serikali kwa miaka 49 imeshindwa kuboresha hali zenu,kwa nini bado tunang'ang'ania kuwarudisha uongozini,ni lini sisi tutaamka na kusema hatutaki upumbavu wa ahadi hewa.
    Tanzania amkeni,sisi ndio tutakaoinua nchi yetu na sio viongozi
    mdau istanbul

    ReplyDelete
  6. HIYO NCHI YENU IMEKWEISHA. MIE NA WANANGU HATURUDI KAMWE
    mie juzi nimesoma yalioandikwa na john mashaka kuhusu mafuta ya petroli kuchanganywa na mafuta ya taaa, nikaishiwa hamu.
    HIYO NCHI SIRUDI HATA KWA DAWA, NITAKAA NA KUFA ULAYA NGGOJA NILE SOCIAL WELFARE CHECKS LAKINI nisirudi tanzania. malkia ananipenda sana kwa nini nirudi kujiumiza na ujinga na upuuzi wa kikwete na kundi lake la wezi. mimi nakufa na kuzikwa hapa hapa UK

    ReplyDelete
  7. Ahsante mdau kwa kuleta such topic.. Tanzania inasikitisha, maendeleo hayaji kama sector muhimu kama hii ya umeme ipo ipo tu.. Ukataji wa umeme, unaongeza wezi na majambazi, watoto kushindwa kusoma, mbu kuongezeka n.k mwishoni mnasema idadi ya wanafunzi walio-pass mitihani inapungua hamjui kuwa umeme ni chanzo kimoja wapo. Nipo nchi ya watu hapa na nipo miaka na miaka sijasikia hata siku moja umeme ukikatika..y tz? wakati tuna kila sababu ya kupata umeme..tumejaliwa na all those resources..Anyways, nadhani solution nyingi zimeishia semwa na mdau aliyetoa hii habari..inasikitisha tz!!
    Mdau,
    USA

    ReplyDelete
  8. Tuna matatizo mawili mkubwa hapo kwetu.moja vichwa vya viongozi wetu vikishasikia kuna swala la kubadilisha mfumo wa utendaji au kuweka mwekezaji vinatanguliza kuangalia vitafaidikaje binafsi na hatimae mikataba inayofuka moshi kama bomu.

    pili maamumuzi mengi yanafanyika mezani hatuna research za kuleta maendeleo research ni kitu muhimusana ila mfanya research wa tanzania ni bora akagombee ubunge kwani ndiko kuna ulaji.bila kufufua sehemu hii ambayo ni chachu kwa maendeleo tusau kabisa sisi isue ya maendeleo.

    ReplyDelete
  9. Asante mdau ,Tanesco hata ikigawanywa mabadiliko hayatakuwa makubwa , WAJE WAWEKEZANI . KAMA ILIVYO KWENYA SIMU.

    ReplyDelete
  10. Na huyu sijui Ngeleja amerudishwa tena. Sioni anachokifanya. Tatizo la nishati Tanzania litaisha pale kutakapokuwa na political will kwa hao wahusika. Hata hivyo sisi kama wananchi tujitahidi ku-push hili jambo kwa kuweza sauti zetu zisikike.

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli Tanesco mnachosha hii tabia ya kukata umeme usiku kucha ni mbaya sana. Kwani usiku huwa kuna mambo mengi sana kwa kweli.

    ReplyDelete
  12. Asante sana mtoa mada, kwa kweli tunatia aibu. Umeme tuliambiwa itakuwa ni historia, ujinga mtupu. Serikali hii ya ccm iruhusu mashirika ya kushindana na huyu kikongwe TANESCO. Inatia hasira sana. Sinza kwa kweli tumechoka, umeme unawaka na kukatika bila mpango wowote. Hiki ni kipindi kipya tunataka kuona mabadiliko. Ingawaje wine ni ile ile kwenye chupa mpya.

    ReplyDelete
  13. P. Mkiwa (Indondesia)November 26, 2010

    hi, dr shayo na john mashaka mambo yenu yanaanza kuonekana kuleta mtizamo mpya wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayolikumba tanzania. Ni kweli kuwa kuna haja ya watanzania kutoa mawazo yao ili wamzaidie Rais Jakaya kikwete kuwabana mawaziri aliyowateua. Kuna haja pia ya kuwawekea malengo mawaziri wote ambayo watatakiwa kusign mkataba wa kuyatekeleza na endapo basi wakishindwa wawape nafasi wale wanaoweza kufanya mambo yaende kwa manufaa ya watanzania.

    Ningefurahi sana rais akafikiria kuanza kuweka vijana damu changa katika hizi tume anaounda za kushughulikia matatizo mbalimbali. Kwa mfano issue ya mikopo ya wanafunzi ambayo ameahidi kuliundia tume, wekeni vijana ambao watapewa task na siyo wazee wale wale wa miaka nenda rudi kisa wanauzoefu. Mheshimiwa rais, try these young men and women, use your machinery to spot them and give them hizo task. They will not let you down.

    ReplyDelete
  14. sisi kama watanzania lazima tujue kwamba Tanzania itaendelezwa na sisi wenyewe sio wawekezaji au wageni!Hakuna mwekezaji ambaye atakuja kuktuletea umeme! Ni uzembe na umpumbavu wetu sisi kuwarudisha madarakani watu ambao wameshindwa kutuondolea Kero ya maji na umeme kwa zaidi ya miaka49.Wakulaumiwa ni sisi na viongozi ambao tumewachagua ambao hawajui nini Priority kwa Watanzania watu wasojui ili Mtanzania aendelee inatakiwa nini kifanyike kwanza!Mimi hata mkisema kuna wataalam hao mnawaita wataalaam walishatufanyia nini au nsi sifa tu za mitaani kwamba kamaliza shule na kafaulu lakini hakuna lolote walofanya hao wataalaam zaidi ya kukariri masomo na kujibu Mitihani??hawana lolote nikimaanisha kwamba maarifa hakuna!!Miradi ya umeme wa uhakika ilifanyiwa upembuzi yakinifu toka enzi za Nyerere na Makabrasha yapo wizara ya Nishati.sasa jiulize toka mwaka1980 kwanini haijatekelezwa???Kama ni ujenzi wa mabwawa ya umeme inamaana hao wasomi wetu wameshindwa hata kuiga hayo yalojengwa na wakoloni???kwani kama ni Mitambo inanunulika Korea au china!kweli teknologia inabadilika lakini hata hiyo ya zamani nayo inasumbua???Hao wataalam wengi wako wapi??Na huu uongozi wa CCM ndio kikwazo cha maendeleo Tanzania kama hujagundua maana wao hata tatizo la foleni nalo watatafuta mwekezaji,yani ni Wapumbavu watupu na kama mtawang'ang'ania mjue hakuna jipya kwani upumbavu hauna dawa, Mpumbavu ni mpumbavu mpaka anakufa.unaweza ukawa umesoma lakini bado pumbavu kwakua huna maarifa,unashindwa kuitumia elimu yako kuondoa matatizo yako kazi kwelikweli!!

    ReplyDelete
  15. Tatizo kubwa la nchi hii inaangalia sana Siasa badala ya uchumi. Wanaotuwakilisha mjengoni wanazungumzia zaidi masuala ya kisiasa badala ya uchumi ambao ndio muhimu. Yote haya sababu ya maslahi yao binafsi na sio kwa manufaa ya nchi kwa ujumla.

    Naomba mnielimishe, hivi hawa wabunge wa viti maalum hua kazi zao ni zipi?, na hivi juzijuzi nimeona rais wa Zanzibar ameteua mawaziri kadhaa wasiokua na wizara maalum nini maana yake au kazi zao zipi???

    ReplyDelete
  16. Yule Boss aliyefanya ubabe kwa mafundi matokeo yake tumeingia gizani ameshaachishwa kazi?. Kama bado wafanye haraka liwe fundisho.

    ReplyDelete
  17. Kitu cha kwanza ambacho naona ni muhimu sana kukifanya na kinafanyika bila tatizo lolote kama tutataka na kutekeleza uamuzi ni kutenganisha uzalishaji na ugavi wa umeme. Hao hao TANESCO wahangaike na maji kujaa au kutokujaa Mtera haohao wahangaike kuja nyumbani kwangu kuchungulia kama umeme wangu unapitia kwenye mashine ya luku ama nimeshachakachua umeme wangu.

    ReplyDelete
  18. Big up Michuzi kwa kupost mada za maana kama hizi. Kwa bahati mbaya sana viongozi wetu waliowengi hawapitii maoni yanayotolewa kwenye mitandao kama hii, na hata wakipitia sidhani kama wana uchungu wa kutosha na nchi yao.
    Maendeleo tunayoimba kila siku kamwe hayatatokea endapo swala la miundo mbinu, haswa la umeme, litakuwa limetafutiwa ufumbuzi. Viongozi wetu wanatembelea nchi nyingi duniani, sijui wanajifunza nini katika matembezi yao. Nimekaa South Africa miezi sita sasa sijawahi kuona umeme umekatika hata siku moja, na hata wakipanga matengenezo maaluum wananchi hutangaziwa angalau wiki moja kabla ya kukata, na matengenezo hufanywa usiku. Ndiyo maana mambo yao yanaenda. Huo ni mfano tu. Nadhani umefika wakati watanzania tuanze kudai mambo ya nsingi kama hili.

    ReplyDelete
  19. mwaka huu wa mgawo nitaendelea kuuza majenereta. teh! teh! samahani wadau.
    karibuni.
    au mwataka kutuharibia wengine biashara?

    ReplyDelete
  20. TATIZO NI WIZARA.IMEOZA KABISA.
    HAKUNA INFORMATION ZA MAANA KWENYE WEBSITE YAO KWA AJILI YA WAWEKEZAJI.WEBSITE IMEJAA BANNERS ZA WAHESHIMIWA TU,MARA KAIBUKA NA SUTI NYEUSI,NYEKUNDU,NJANO.WALA CONTACTS ZAO HAZIPO.
    WEKENI INFORMATION ZA KUELEWEKA KWA AJILI YA WAWEKEZAJI.

    ReplyDelete
  21. Kweli hakuna kama Tanzania!!!!Tuna vyanzo karibu vyote vya umeme...maji ,gesi ,Uranium etc to name a few..lakini hatuna umeme wa kueleweka..halafu mtu unajiita waziri sijui mkurugenzi etc ndani ya ofisi kubwa gari la mamilioni...bize for nothing....nafikir ishu kubwa ni ubinafsi....hata ningekuwa mimi....

    ReplyDelete
  22. ikulu umeme ungekuwa unakatika JK angeenda kwa bill gate kuomba msaada. lakini haukatiki shida iko wapi. wengine mtajiju. lumi wa mazense

    ReplyDelete
  23. Mdau! nakushukuru kwa kupost kilio chako/chetu ili tuweze kuchangia. Umeandika vizuri lakini naomba nikukumbushe ulichosahau.
    Nataka nikuhakikishie,ulichoshauri, Tanesco kwa maana ya wafanyakazi na Management pamoja na serikali kwa maana ya wizara ya nishati na madini na serikali kwa ujumla wake, wanatambua ushauri wako hata pengine zaidi ya wewe ulivyoshauri.
    Tatizo ni nini? Wananchi kwao sio priority, kama ambavyo wewe unafikiri (na,hili naongelea serikali wala sio Tanesco), wana vipaombele vyao wao kama serikali ya CCM. Watayahubiri haya majukwaani wakitaka kitu/kura kwenu lakini mioyoni kwao hawamaanishi hivyo kabisa. Ndio maana nchi iko hapa ilipo baada ya miaka 49 ya uhuru. Wewe umeongelea Umeme of which ni one aspect tu ndio maana nataka uitazame kwa upana ujue sio Tanesco yenye tatizo. Kama serikali ingekuwa hairidhiki na utendaji wa management ya Tanesco wala isingekuwa swala la kuisumbua kichwa. Juzi ulisikia Ngeleja akisema kwamba "anataka swala la tatizo la umeme liwe historia kwa watanzania" lakini amekuwepo kwenye baraza la mawaziri lililopita kwa wizara hiyo hiyo akiwa kama waziri, amefanya nini so far?
    Hitimisho, ulisema vizuri kuhusu kugawanya Tanesco na kuleta wawekezaji ili kuongeza ushindani, likiwezekana hilo ni vizuri. Lakini, mimi nataka kushauri kwamba, tuongeze ushindani kwenye serikali kwa maana ya chama kinachotuongoza ambacho kimetuongoza kwa miaka hiyo 49 na kutufikisha hapa tulipo. Ushindani huo tunauongezaje? kwa kubadilisha katiba ya nchi yetu inayoipa jeuri serikali ya CCM kwamba either itumikie au isitumikie wananchi itaendelea kuwepo tu madarakani. Bila kufanya hili wakajua kwamba wasipo-deliver wanaondoka tutaishia kupiga kelele, leo Tanesco kesho maji, kesho kutwa afya e.t.c

    ReplyDelete
  24. wengine tuko kibiashara kama umeme hakuna twauza solar nq generator kwa wingi ati.

    ReplyDelete
  25. Tanzani baada ya miaka 49 ya uhuru inazidi kuelekea kubaya.wakati wa mwalimu kulikuwa na barabara za lami hata kwenye baadhi ya mitaa ya Dar es Salaam mfano magomeni,kinondoni.Lakini hadi leo hii hakuna huduma hata moja unaweza sema inapatikana kwa uhakika maji hayapatikani,umeme ndo hivyo,barabara nazo uzushi tu hapo wanapokuita posta katikat ya mji kuna mashimo yanafukuliwa yanakaa hata mwezi hayafukiwi wanaziba na matawi ya miti.Hivi TANESCO kwa ubora gani waliokuwa nao hata leo hii serikali inkataa watu wengine wa kuwekeza kwenye umeme?ni ujinga kuendelea na mambo yasikuwa na faida,mimi siwaelewi viongozi wa Tanzania kama kiongozi anaweza akasimama mbele ya wananchi akasema foleni za barabarani ni dalili kwamba watu wameendelea nadhani tuna tatizo kubwa sana la viongozi na kitu kinachoitwa maendeleo tunaweza tukawa tunasikia tu hadi mwisho wa dunia.Uingereza hapa magari ni mengi kuliko ya Tanzania lakini hakuna foleni kwa maaana hiyo Tanzania imeendelea kuliko Uingereza??Halafu kibaya zaidi viongozi hao hawaoni kama kukosekana kwa umeme ni tatizo,wanaona ni maisha ya kawaida tu kwa vile wao haiwagusi hata kidogo.Na kila siku viongozi hao wanasafiri kwenye nchi nyingine na wanaona mambo yanavyoenda lakini wao kama wamefungwamacho na masikio.Kwa kweli inachosha na kusikitisha ukiona maisha yanayoendelea kwa Tanzania yetu.Kiwango cha umasikini kinaongezeka gap ya aliekua nacho na asiye kuwa nacho limekuwa kubwa sana na linazidi kuongeza,itafika hatua hata zile kuta wanazojinzungushia majumbani kwao itabidi waziongeze urefu ziwe kama za jela kwasababu tabaka la chini halitavumilia kuona anashinda hata kula mlo mmoja halafu mwingine kapark VX 4 uwani huko.Sasa ikifika hatua ya masikini kuchoka na kuona heri afe kuliko kuendelea kuona mali za nci yake wanfaidi wachache Tanzania haitakalika tena.
    Mdau,

    ReplyDelete
  26. he he heeee, miaka 50 ya uhuru chagua ccm yajenga nchi ...!!!!

    ReplyDelete
  27. HALAFU TUKISEMA HATURUDI BONGO, MNAANZA MKATAA KWAO NI MTUMWA, SASA HAPA NANI MTUMWA?? WAKATI VIBOSILE WANAFAIDI KIPUPWE NYIE MNALIA NA JOTO KAZI HAZIFANYIKI MNALALAMIKA WEEE HAMNA UWEZO WA KUWAELEZA LAIVU MNAOGOPA, HUO NDO TUNAITA UTUMWA MAMBO LEO NA BADO!!! MAJUU RAHAAA, SASA HIVI NI WINTER NA MIBARAFU YA HATARI LAKINI UKIINGIA IN THE HOUSE SHWARIIII JOTO LA KUTOSHA SABABU KUNA HEATER JE MAJUU NDO INGEKUWA BONGO? SI WATU WANGEGANDA NDANI YA NYUMBA ZAO???? HUKO HATURUDI NG'OOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!

    ReplyDelete
  28. HUKO HATURUDI KAMWE, NA HATA YESU AKIRUDI MARA YA PILI ATUNYAKULIA HUKUHUKU MAJUU!!

    ReplyDelete
  29. Huku Morogoro mgao wa umeme umeanza kiaina!

    ReplyDelete
  30. Kabla ya netgroup solusheni kulikuwa na Pendekezo la kuigawa TANESCO katika sehemu tatu za 1.Uzalishaji 2.Usambazaji na 3.Ukusanyaji wa mapato lilitolewa na waliotaka kuwekeza lkn halikukubaliwa na wenye maamuzi.

    Mapendekezo yaliitaka serikali kubeba jukumu la kuzalisha umeme kitengo ambacho kina madeni ya muda mrefu na yenye riba ndefu.Madeni yote yawe mzigo wa serikali na wasambazaji na wakusanya mapato wasihusike na madeni ya nyuma.Baada ya kukusanya mapato yatagawanywa kwa mujibu wa mkataba kwa mzalishaji, msambazaji na mkusanyaji.wapo waliokuwa tayari kwa kazi hiyo.Maamuzi yalitoka kwamba atakae amua kuwekeza abebe na mzigo woote wa madeni toka shirika lilipoanzishwa.Kilichobaki mambo yamebaki kama yalivyo na mikataba kwa manufaa ya wachache huku wengi tukilipa gharama hizo na kuambulia maumivu.

    MUUNDO HUU UTATUFAA ZAIDI IKIWA NI PAMOJA NA KURUHUSU WAWEKEZAJI WENGINE ILI KUTOA USHINDANI.

    ReplyDelete
  31. Ndugu yangu uliye toa hiyo maada nafikiri una haki na unastahili kupewa big up!

    Mimi mwenyewe nilifanya kazi TANESCO kama mechanical technician kwa miaka ya nyuma kidogo. Kwa maana hiyo ninaifahamu Tanesco vizuri. Kuna matatizo ya aina kama tatu:
    1. Huduma mbovu kwa umeme uliopo. Hili tatizo ni la Tanesco wala si seriakali.
    Jawabu lake: Ni kama ulivyo sema hapa inatakiwa ushindani wa kutoa huduma- Kwa mfanyakazi yeyote anayejua kuwa mshahara wake utapatikana kama mteja atalipia umeme nafikiri haatakuwa mzembe.
    2. Mipango mibovu ya serikali ambayo inapangwa kwa kufikiria kwanza 5-10% ya watu binafsi.
    Jawabu lake: Linapatikana kutoka kwa wanannchi wenyewe. Lugha ambayo ni rahisi serikali kuisikia na kuinyenyekea ni kuwakataa kwa kupiga kura. Na kuhakikisha kura yako haipotei na italindwa hata kama kupoteza maisha yako. Kwa maana hiyo ni kuwambia malengo yenu hayakukamilika hivyo tupisheni.
    3. Hapa nitaomba wasomi mnisamehe kwa kuwagusa. Mimi ninaelewa kuwa na Degree ya udaktari siyo sababu ya kuafanya kazi ikaonekana. Hapa naona watanzania wengi tunatanguliza degree/Phds ili iwe justification ya mtu fulani kufanya kazi vizuri. Siyo ukweli hata kidogo! Tunataka mtu ambaye atafanya kazi na kudeliver! Sasa jamani nieleze nyie phds holders utapangaje project kubwa kwa nchi kama yetu bila hata kuwa na pilot project? Nieleze utawezaje kuokoa hayo mabilioni ya fedha endapo hayo maproject makubwa yasipofanikiwa? Mfano ni project ya mvua ya mheshimiwa Luwasa. Hakukuwa na kitu kama pilot project wakati hao wanaomzunguka ndio hao phds holders! Basi tujirekebishe kwani kazi ya ushauri hata mtendaji mzuri mwenye degree moja anaweza kufanya maaajabu.

    Ahasanteni sana

    ReplyDelete
  32. Si uliona wale watuhumiwa wanapigiwa kampeini za ubunge au umesahau. Wewe upati umeme, lakini mafisadi wana umeme 24hrs/7Day a wiki. Maendeleo katika nchi yenu Tanzania mnatwangia maji kwenye kinu.

    Koo zenu zitakauka bure, lakini maendeleo ni kwa mafisadi. Wapo huku Marekani wanatumia hela ya serikali kuja kununua nyumba Marekani kwa cash. Ngoja nikae huku USA nibebe wazee na mikono iendelee kuota vigimbi.

    Nabeba wazee USA sijawahi kukosa umeme hata second moja. Na hela ninayoipata kuosha BM ni haki yangu sio ya udanganyifu. MMMMMMMMMMMMMM yangu macho kwa Watanzania.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  33. Pamoja na hayo mapendekezo, njia nyingine ni kuligawa shirika hilo ki-kimkanda:

    Kasikazini Mashariki (Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga); Mashariki (Dar, Moro, Pwani); Kati (Singida na Dodoma); Kusini (Lindi, Mtwara na Ruvuma); Nyanda za Juu Kusini (Iringa na Mbeya); Ziwa (Mara, Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Kagera); Magharibi (Rukwa, Tabora na Kigoma).

    Hii itasaidia endapo sehemu fulani takosa umeme, sio Tanzania nzima kuathirika.
    ---------------------------

    Na wewe uliyetamka, "Si uliona wale watuhumiwa wanapigiwa kampeini za ubunge au umesahau," nimekusikia.

    Lakini usisahau:

    Chadema imekuwa mstari wa mbele wa kupinga udisadi nchini. Sawa!

    Na huyo mkereketwa mkuu wa Chadema Mabere Marando amekuwa kimbelembele akimsakama Rais Kikwete kwa kulinda mafisadi, ikiwa ni pamoja na kumnadi aliyekuwa mgombea ubunge wa Rombo Basil Mramba, akidai kuwa JK alikuwa akimsafishia Mramba kesi inayomkabili.

    Lakini mbona huyu Mabere Marando ndiye mtetezi wa kesi ya ufisadi inayowakabili akina Basil Mramba, Daniel Yona na Grey Mgonja?

    ReplyDelete
  34. Nafikiri siku Mhe Rais atakapoiweka Tanesco chini ya JKT mambo yatakuwa mazuri,lazma Tanesco iongozwe na wanajeshi.

    ZAUNUNU.

    ReplyDelete
  35. Wewe uliyejibu comment yangu kuhusu Mabere Marando kutetea Mafisadi. Kumbuka kuwa Mabere Marando ni Mwanasheria anatafuta ulaji. Mwanashereia hata kama anajua kuwa mtu anakosa na kuna ushahidi wa kutosha bado mwanasheria ataendelea kumtetea, lakini akijua kuwa siku moja huyu mteja wake atafungwa ama atanyongwa. Hii nafikiri hata wewe mwenyewe unajua kabisa. Sasa Marando kwa JK naye anatafuta jinsi ya kuingia Ikulu. Ama kama hujawahi kuona wanasheria wanatetea kesi za mauji na zenye evidence za kutosha uwe unaangalia TV na unasoma magazeti mbali mbali utapata jibu. Kwa hiyo Mabere Marando sio kuwa anatetea Mafisadi hii ni kazi yake. Kama wamemnyima hii nafasi eti kwa sababu alikuwa anawatetea akina Mramba ni kosa. Field yake ni kutetea watu hata kama yeye anajua unakosa atakwambia twenda kujaribu ndo mshahara wake.

    Lakini viongozi wabovu mnawachagua wenyewe baadae mnaanza kulalamika.
    Ni Watanzania wachache ambao wamejaribu kukumbuka shuka kumekucha.

    Wacha niendelee kuwasafisha wazee mavi na mkojo ili mradi napata ile ambayo ni haki yangu. Hao vijana mnao watetea ndo wamepigia kura mafisadi kuliko wazee. Juzi wanaandamana eti kwa nini CHADEMA walitoka nje ya Bunge!!

    Watanzania mmelala sana na ndo maana nchi imeliwa kila kona hakuna upenyo.

    Kipindi cha uchaguzi nimeona vijana wengi wakipeperusha vitambaa vya kijani.

    Kazi kwenu.

    ReplyDelete
  36. A politician thinks of the next election. A statesman, of the next generation.

    ndio maana unakuta kuna makundi kwenye vyama na ubinafsi,chuki,majungu na kila jambo la kurudisha nyuma maendeleo,leo hii nyerere angekuwa hai hawa wahuni wanao tuongoza sijui wapi wangesimama na mambo haya,ujumbe wa juu tukitafakari tazama china,idonesia,india wapi leo wako sisi miaka 50 inakwenda bado tuna katiba ya 1961 na mashirika mabovu kama tanesco,watanzania tunatakiwa kudai haki zetu

    ReplyDelete
  37. CCM hoyeeeee. Watanzania wakaitikiahoyeeeeeeeee. Waliitikia hivyo kwa kuchanganywa na pamba za ccm, ti-shirt na caps.

    CHADEMA juuuuuu,juuuuuuuuuuuu. Wabongo waliona kuwa chadema italeta maendeleo na mabadiliko. Ahadi ziliwachanganya na kweli zilikuwa nzuri na wakafurahia sana kuona chama cha ukombozi.

    Kidumu chama cha mapinduzi.. Kidumuuuuuu. Watanzania hao hao wakaitikia tena na kumruudisha alieshashindwa kuwahudumia miaka mitano ilopita madarakani.

    Ukipenda boga penda na ua lake. Watanzania wanajua kabisa ubaya wa serikalli ilorudi madarakani ila sababu ya u-coward wameipa tena nafasi.

    Uozo kama tanesco, afya, elimu etc uliozeshwa na hao mliwapa tena nchi.

    Mwenye uwezo wa kukimbiia nchi na akimbie. Ni bora ingeuzwa kila mtu apewe chake akaangalie ustaarabu mbele.

    Nishachoka kutoa mawazo ya maana hakuna mtu anasoma bora kusafisha kinywa tu. Hapa nilipo umeme hamna natumia simu yangu kutuma hii comment.

    Mabadiliko yataletwa na kudhubutu peke yake. CCM ikiendelea kudumu sahauni maendeleo.

    Wengine tumerudi na masters zetu toka nje ya hii nchi. Tuna mawazo mapya lakono hatupewi ajira.. 2umeishia kuwaandikia desertaion wanaofanya masters hapa kwa ujira walau tuendelee kusurvive..

    CCM oyeee.
    Mdau anaesubiri mabadiliko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...