Spika anayemaliza mda wake Mhe. Samuel Sitta akiwasili katika ofisi ndogo za CCm Lumumba, Dar es Salaam kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake hiyo nakupokelewa na baadhi ya wananchama wa CCM
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM Ndg. Mattison Chiza akimkabidhi fomu Mh. Sitta ya kuwania UspikaSpika anayemaliza mda wake Mhe. Samuel Sitta akisani kitabu cha watu waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika kwenye Ofisi za CCM Lumumba Mh. Sitta akirejesha fomu zake baada ya kuzijaza Spika Sitta akiongea na waandishi wa habari katika Ukumbi wa CCM Lumumba jijini Dar es salaam mara baada ya kurudisha Fomu ya kutetea kiti chake cha Uspika Kupitia CCM, ambapo uchaguzi wa Spika unatarajiwa kufanyika wiki ijayo Dodoma. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge
SAMWEL SITTA NA WENGINE KADHAA WACHUKUA FOMU

Spika anayemaliza mda wake Mhe. Samuel Sitta leo amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge katika Bunge la Kumi kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mjini Dodoma.

Spika Sitta amechukua fomu hiyo kupitia chama chake cha CCM katika ofisi ndogo za CCm Lumumba, Dar es Salaam na kuijaza kisha kuirudisha leo hii baada ya kukamilisha mahitaji yote ikiwa ni pamoja na kugharamia fomu hiyo kwa kiasi cha Tsh 500,000/= kwa mujibu wa taratibu wa chama hicho.

kwa Mujibu wa ibara ya 84 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, chama chochote cha siasa kilichosajiliwa kina haki ya kushiriki katika Uchaguzi wa Spika kwa kumpendekeza mwananchama wake mmoja ambaye ni Mbunge au asiye Mbunge mwenye sifa za kuwa Mbunge kuwa Mgombea wa nafasi hiyo.
Wagombea wengine waliojitokeza kugombea kiti hicho ni pamoja na Mbunge metule wa Same Mashariki, Anne Kilango-Malecela, Mbunge Mteule wa Njombe Kusini, Anna Makinda na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tambaza, Bw. Salim Kungulilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Best of luck mr Six, kwa Bunge hili jipya sioni mtu mwengine yeyote CCM anaefaa.

    ReplyDelete
  2. mtani wa wakwere woteNovember 04, 2010

    Hatimae chuma cha pua kinarudi tena mjengoni,safi safi tunakutakia kila la kheri baba SAM SITTA bunge lijalo uliendeshe vizuri kwa hekima na busara kubwa bila kusahau ile mizaha yako ya hapa na pale inayolichangamsha bunge wabunge na cc wafuatiliaje wa bunge live,huwa unatufurahisha sana ikikikalia kiti.

    Tuko pamoja,wapiga nawaambia hivi MZIGO MZITO SIKU ZOTE MPE MNYAMWEZI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...