Kwa mujibu wa katiba ya ATSA kifungu cha 5 .4(c) ”kila mwanachama ana haki ya kugombea au Kupiga kura ili kumchagua mgombea ampendaye katika nafasi yoyote ya uchaguzi kwa kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi” kwa maana hiyo wizara ya katiba na sheria iliunda tume ya uchaguzi kusimamia shughuli zote za uchaguzi za mwaka huu kama ilivyo ada.

Tume inawataarifu wanachama kuwa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zitaanza kutolewa rasmi tarehe 10/11/2010 siku ya JUMATANO na siku ya mwisho ya kurudisha(deadline) ni tarehe 10/12/2010,baada ya hapo kikao cha tume kitafanyika ili kupitisha na kutangaza majina ya wagombea na tarehe rasmi ya uchaguzi.

Uchaguzi utafanyika kati ya tarehe 24 na 28 mwezi ujao kwani kutokana na ratiba za vyuo mbalimbali nchini muda huo vyuo vitakuwa vimefungwa.Tunaomba mwenye maoni kuhusu tarehe rasmi ya uchaguzi awasiliane na tume ya uchaguzi au wizara ya katiba na sheria.
Fomu za uchaguzi zinapatikana kwa viongozi na wajumbe wa Tume kama walivyoorodheshwa hapo chini:

Raymond Mauki-KATIBU WA TUME –ALGIERS
Issah Maluka-MWENYEKITI WA TUME-BEJAIA
Tedyina Simba-MJUMBE -
Ally Musa-MJUMBE –Tizi Ouzou
Hamadi Hamis-MJUMBE -Burmedes
Sarah Swai-MJUMBE –ALGIERS
Nafasi za uongozi ni kama ifuatavyo kama inavyosema katiba ya ATSA;
MWENYEKITI
MAKAMU MWENYEKITI
WAZIRI MKUU
MWEKAHAZINA

Tume inawahamasisha wanafunzi wote waTanzania waliopo Algeria kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa jumuiya yetu hii.Maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe hivyo tuungane kwa moyo mmoja kulisukuma jahazi hili.
Mwisho tume inawatakia masomo mema na maandalizi mema ya mitihani itakayofanyika mwezi ujao.

Imetolewa na RAYMOND MAUKI
KATIBU –Tume ya Uchaguzi
ATSA-Association of Tanzanian Students in Algeria

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...