Tume ya Uchaguzi imetangaza nafasi 104 ya wabunge wa viti maalumu kwa mgawanyo wake wa kuweza kuingazia uwiano wa wingi wa kura za ubunge. Hivyo baada ya kukokotoa uwiano wa viti hivyo CCM imejizolea viti 65, CHADEMA kimepata viti 23 na CUF kimepewa viti 10.

Katika bunge lililopita kulikuwa na Viti maalumu 75 ambapo CCM ilikuwa ina viti 58, CUF viti 11 na CHADEMA viti 6. Viti vingine 6 vimeachwa wazi vikisubiri matokeo ya majimbo 7 ambayo uchaguzi wake haukufanyika.

Yafuatayo ni majina ya wanaopewa nafasi kutajwa kuwa wabunge wateule kutoka CCM na CHADEMA. Chama Cha Wananchi CUF bado hakijapeleka orodha ya majina waliyopendekeza kuchukua nafasi zao 10.

MAJINA YA WABUNGE WATEULE
WA VITI MAALUMU WA CCM NI:

Wabunge 65 wateule wa Viti Maalumu toka CCM waliotajwa ni Sophia Simba, Gaudentia Kabaka, Ummi Mwalimu, Agness Hokororo, Martha Umbulla, Lucy Mayenga, Faida Mohamed Bakari, Felista Bura, Kidawa Hamid Saleh na Stella Manyanya.
Wengine ni Lediana Mng’ong’o, Sarah Msafiri Ally, Catherine Magige, Tauhida Galos Cassian, Asha Mohamed Omari, Rita Mlaki, Anna Abdallah, Fenella Mukangara, Terezya Huvisa na Al-Shaymaa Kwegir.

Wengine ni Maria Hewa, Hilda Ngoye, Josephine Genzabuke, Esther Midimu, Maida Hamad Abdalla, Asha Mshimba Jecha, Zarina Madabida, Namalok Sokoine, Munde Abdallah na Benardetha Mushashu.
Pia wamo Margreth Mkanga, Angellah Kairuki, Zainab Kawawa, Mwanakhamis Said, Riziki Lulida, Devotha Likokola, Christina Ishengoma, Mariam Mfaki, Margreth Sitta na Subira Mgalu.

Wengine ni Vicky Kamata, Pindi Chana, Fatuma Mikidadi, Getrude Rwakatare, Betty Machangu, Diana Chilolo, Fakharia Shomari Khamis, Zaynabu Vulu, Abia Nyabakari na Pudenciana Kikwembe.

Wengine ni Rita Kabati, Martha Mlata, Dk Maua Daftari, Elizabeth Batenga, Azza Hamad, Mary Mwanjelwa, Josephine Chengula, Bahati Abeid, Kiumbwa Mbaraka na Roweete Kasikila, Anastazia Wambura, Mary Chatanda, Rosemary Kirigini, Mariam Kisangi na Kemilembe Lwota
-------------------------------

MAJINA YA WABUNGE WATEULE 23
WA VITI MAALUMU WA CHADEMA NI:

Lucy Owenya, Ester Matiko, Mhonga Ruhwanya, Anna Mallac, Paulina Gekuli na Conchesta Rwamlaza, Suzan Kiwanga, Suzan Lyimo, Grace Kiwelu, Regia Mtema, Christowaja Mkinda, Anna Komu, Mwanamrisho Abama, Joyce Mukya, Leticia Nyerere na Chiku Abwao.

Wengine ni Naomi Kaihula, Grace Kiwelu, Rose Kamili, Christina Lissu Mughiwa, Raya Ibrahim, Philipa Mturano, Miriam Msabaha na Rachel Mashishanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. Msaada tutani: Wadau Rose Kamili namsikia sana, ni nani? naomba data zake. Mangelepaa.

    ReplyDelete
  2. Mbona wabunge kumi (30%)wa chadema wametoka mkoa mmoja tu? Mhhh.....

    ReplyDelete
  3. Chadema mnatutisha.wabunge 90percent dini moja.

    ReplyDelete
  4. Mmmmhhh jamani hawa CCM wanatupeleka wapi? Mbona hawa wakongwe wameshatuchosha bado wanawarudisha tena? Inakuwaje mbunge kakataliwa na wananchi kwa kuwa aliprove failure then anarudishwa bungeni? Mmmh hayaaaa yetu macho ingawa tumeshakata tamaa na hayo maisha bora maana kumbe wanayatafuta hao viongozi wetu kwa ajili yao na familia zao na si maskini walio wengi

    ReplyDelete
  5. MHhhhhhhhhhhhhhhhhh je ni majina ya ukoo yanafanaa au ndio kupeana? Maanake kama si wake ni watoto wa kike wa viongozi, kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  6. Njia wanazotumia NEC kugawa hizi kitu si za uhakika, uhuru na uwazi. Mwaka huu tofauti na mwaka 2005 CCM imepata idadi pungufu ya wabunge wa kuchaguliwa na kura za urais. Kwanini sasa wao wapate 63% ya viti maalum!? Bila tume huru, kila uchaguzi nchi hii litakuwa kama bomu linalosubiri kulipuka.

    ReplyDelete
  7. CADEMA iko kichaga zaidi....Rose Kamili ni mke wa Dr. Slaa mtalikiwa.

    ReplyDelete
  8. Asilimia 91% wabunge viti maalum chadema ni WAKRISTO???? CHADEMA acheni udini ndio maana mnang'ang'ania MBOWE awe kiongozi wa upinzani bungeni badala ya ZITO kwakua ZITO muislam

    ReplyDelete
  9. Wewe anony (30%) acha maneno nyie mikoa mingine si mmeona vyama vya upinzani ni vita? si ndvyo mnavyowaambia wananchi wenu? SAS KAMA HAKUNA MWANACHAMA WA CHADEMA MTAPEWAJE VITI MAALUM?

    ReplyDelete
  10. WE ANO. WA 2, KWANI HUJUI KUWA CHADEMA INA HARUFU YA UKABILA??......

    ReplyDelete
  11. mtaongea mengi kwani hapo wameandikwa wametoka mkoa gani, oh mara Rose Kamili ni nani ooh mara 30% wametoka mkoa mmoja tu, umejuaje wametoka mkoa fulani wakati hawajaonyeshwa mkoa walikotoka acheni kuchonga fanyeni mambo yenye maendeleo. Hata kama watakuwa wametokea kagera au kigoma wote sisi tunamaind maendeleo thats all.

    ReplyDelete
  12. Chadema kwa kweli kina harufu mbaya.....mimi mwenyewe Mkristo na pia natokea kaskazini. Chama kinatakiwa kiwakilishe jamii sasa hii Chadema hayo majina kweli yanaonyesha uwakikilishi wa jamii ya Watanzania??!! Hawa jamaa wasije wakawa wanataka kuturidisha nyuma.
    Kila jema
    Mzawa

    ReplyDelete
  13. Watu jamani mmendekeza ukabila na udini, mbona hamsemi CCM ni watoto na wake za vigogo. Pili mikoa mingine haitaki upinzani kwa hiyo unataka walazimishe majina kuingia upinzani, tatu hiyo percentage ya udini umeitoa wapi mbona husemi percentage ya CCM wakristo ni wangapi nawatoto wa vigogo wangapi. Halafu nakuomba uangalie mikoa wabunge wanakotoka, kuna siyo majina> Mlianza Chadema ni Wakristo bila kujua viongozi ni dini zote na makabila yote. Kuwa mchunguzi siyo kudandia

    ReplyDelete
  14. '''Mbona wabunge kumi (30%)wa chadema wametoka mkoa mmoja tu? Mhhh.....;;;

    Jibu, Ndo mkoa wenye wasomi zaidi!


    ''Chadema mnatutisha.wabunge 90percent dini moja.''

    Ndo wasomi jamani, mbona hamtaki kukubali??''

    ReplyDelete
  15. Kwa wale wanaosema ni mkoa mmoja angalia mgawanyo acha vijicho vya usuda bure
    Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao majina yao yamepitishwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Lucy Owenya (Kilimanjaro), Esther Matiko (Mara) Mhonga Luhanywa (Kigoma), Anna Mallac (Katavi), Paulina Gekul (Manyara), Conchesta Rwalumulaza (Kagera), Suzan Kiwanga (Morogoro), Grace Kiwelu (Kilimanjaro), Suzan Lyimo (Kilimanjaro), Regia Mtema (Morogoro), Christowaja Mtinda (Singida), Anna Komu (Dar es Salaam), Mwanamrisho Abama (Zanzibar), Joyce Mukya (Arusha), Leticia Mageni Nyerere (Mwanza) na Naomi Kaihula (Dar es Salaam), Chiku Abwao (Iringa), Rose Kamili (Manyara), Christina Lissu (Singida), Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano (Dar es Salaam), Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga (Dar es Salaam).

    ReplyDelete
  16. Mtu anakuwa mdini yeye kama katika kila kitu amangalia based on dini na kabila,kwanii usiangalie performance?tukianza hivyo nchi hii itawaka moto maana CCM raisi muislam plus makamu Zanzibar Raisi muislam plu all makamu acha ujinga angalia vigezo not dini or kabila

    ReplyDelete
  17. Relationship:Rose Kamili(Dr. Slaa), Lucy Kiwelu Owenya, Grace Sindato Kiwelu(Ndesamburo),na Lissu.Dini:90% ni wakristo(its crucial but not important),Kabila na mkoa: 85% Kanda ya Kaskazini. wadau nawasilisha...

    ReplyDelete
  18. Kuna watu wanachekesha hawajui jinsi walivyowachagua hivyo viti maalum waulizeni NEC watawambia wametumia mfumo gani sasa wengine wanongea ovyo kwanza uliza utapewa majibu ya kina sio kulopoka

    ReplyDelete
  19. Grace Kiwelu imeandikwa mara mbili!

    ReplyDelete
  20. Nyie mnaodai ukabila na udini Chadema mmeshiriki vipi ndani ya chama hicho na mkatupwa nje kisha mnatuletea malalamiko sisi? Isije ikawa ni wale msioshiriki lakini ni walalamikaji wakubwa. Wewe Mangelepaa unayetaka data za Rose Kamili mbona wewe haujatupa data za mkeo? tupe nasi tutakupa.

    ReplyDelete
  21. walalahoi wa tanzania watabaki hivyooooooo tu. Naomba kuuliza wabunge maalum kazi yao nini hasa bungeni? Je wanatakia wawe na sifa zipi? Je wanalipwa sawa na wabunge tulowachagua? why wasichaguliwe na wananchi wenyewe. Mbona wengi mno jamani? why wasichukue kwa kila mkoa mwanamke mmoja?

    Kumbe serikali ina hela jamani tusidanganyike sie maskini wabunge 104 wengi mno ukizingatia mishahara yao mikubwa.

    Hebu angalieni hili waanguna. Imeniuma sana mie nikiumwa naenda hospitali naambiwa dawa zimeisha nikanunue hali hela zinatupwa kwa watu waso kuwa na msaada kwa jamii ila kwa familia zao.

    Je bunge litakuwa na wabunge wangapi piga mahesabu mara posho, mara semina zisizoisha, mishsahara juu, wabunge maalumu imeniuma sana wengi mno jamani KIKWETE angaalie upya usiwafurahishe tumekuchagua sisi sio hao.

    WENGI WENGI WENGI WENGI MNO MNO MNO MNO

    HERI KAMA SERIKALI INA FEDHA BASI IFUNGUE KIWANDA HATA KIMOJA IAJIRI VIJANA WA KITANZANIA UWIIIIIIIIIIIII NAKUFA NA PRESHA MANA HATA SIE WAFANYA BIASHARA WADOGO TUNATOZWA FEDHA ZA USHURU WANALIPWA WABUNGE MAALUM.

    HERI NISINGEZALIWA TANZANIA JAMANI MIE NCHI NZURIIIIIIIIIIIIIIII, MALI ASILI NYINGIIIIIIIIIIII, MADINI KIBAOOOOOOOOOOOOO, MBUGA ZENYE SIFA NZURIIIIIIIIIIII,

    WANANCHI WAKE HOIIIIIIIIIIIIIIIIIII


    WANANUFAIKA WACHEEEEEEEEEEEEEEEEE

    SINA LA ZIADA DUKUDUKU LANGU HILO WENGI SANA HAO

    ReplyDelete
  22. Wewe anony wa 11.21, usilete udini hapa, kama hawo waislam hawajajitokeza CHADEMA, mbona rais na makamu wake ni waislam lakini watu hawasemi? mbaguzi wa dini wewe.

    ReplyDelete
  23. Afadhali CHADEMA 90% ya wabunge ni dini moja CUF je??????

    ReplyDelete
  24. MNAOSEMA CHADEMA NI CHAMA CHA UKABILA NA UDINI NA UMAENEO SIO WANAFUNZI WA MWALIMU NYERERE NA SIO WAZALENDO SAFI. KWANINI MSIISEME CCM AMBAYO RAIS NA MAKAMU NI WAISLAMU? UWT UONGOZI WOTE WA JUU NI WAISLAM, JE MTU MWENYE SIFA ASICHAGULIWE KWA SABABU YA DINI YAKE? MBONA ASILIMIA 90 YA WAWAKILISHI ZANZIBAR NA WABUNGE WA CUF NI WAPEMBA HAMJAWASEMA, MBONA ASILIMIA 100 YA WAWAKILISHI ZANZIBAR NA WABUNGE WA CCM KUTOKA ZENJI NI WA-UNGUJA! MBONA HAMJASIKIKA MKIITUHUMU CCM NA UMAENEO! NARUDIA, MTU MWENYE SIFA ASICHAGULIWE KWA CHADEMA KWA SABABU NI MCHAGA!? ACHENI HIZO!! NANI ASIYEJUA KWAMBA NGOME KUU YA CHADEMA NI KILIMANJARO KAMA ILIVYO DODOMA NGOME KUU YA CCM NA PEMBA KWA CUF? ACHENI HIZOO!!!

    ReplyDelete
  25. acheni akili zenu finyu nyie,chama mnakiita cha kikristo miaka nenda rudi na kukikimbia alafu leo mnalalamika mbona 93% ya waliochaguliwa ni wakristo.


    waislamu wanakikimbia kw akusema ni chama cha kikristo wameenda ccm na cuf sasa leo mnataga chadema wapite miskitini kuwatafuta wabunge maalum wakuwakilisha?

    ReplyDelete
  26. Swali langu ni hili Hivi wabunge wa kuteuliwa(viti maalum) wanamwakilisha nani mjengoni? Utamwekaje mbunge anayewakilisha "walemavu" wakati yeye si mlemavu,au mbunge anayewakilisha maskini wakati hajui adha ya kushinda siku nzima kwa uji na maandazi 2?Ipo kazi.Sababu hakuna kundi maalum katika jamii ya tanzania lakini tuna wabunge maalum.Katiba inabidi ibadilishwe kidogo.Mtu unakataliwa na wananchi(kama mdau mmoja alivyosema awali) halafu unarudishwa mjengoni.Ubabaishaji hautakwisha nyumbani.

    ReplyDelete
  27. wote mliochangia hapo juu naona comments zenu zimejaa chuki, ubinafsi na husuda. tukianza kuangalia watu kwa dini zao au wanatoka wapi sidhani kama tutafika popote. tutaanza kujiuliza mbona uongozi wa serikali wote ni Waislamu, na mbona zitaendelea. wanaochaguliwa katika uongozi hawachaguliwi kwa misingi ya kabila udini au wanatoka wapi. nadhani haya masuala ya kuwabagua watu yanatakiwa kukemewa vinginevyo hatutafika popote. nilidhani sasa tunapaswa kuangalia kuwa bunge la sasa linashiriki vipi kuleta maendeleo ambayo yamekuwa yakinadiwa na wagombea na si kurudi nyuma na kuanza kuangalia huyu ni nani na yukoje.

    ReplyDelete
  28. wote mliochangia hapo juu naona comments zenu zimejaa chuki, ubinafsi na husuda. tukianza kuangalia watu kwa dini zao au wanatoka wapi sidhani kama tutafika popote. tutaanza kujiuliza mbona uongozi wa serikali wote ni Waislamu, na mbona zitaendelea. wanaochaguliwa katika uongozi hawachaguliwi kwa misingi ya kabila udini au wanatoka wapi. nadhani haya masuala ya kuwabagua watu yanatakiwa kukemewa vinginevyo hatutafika popote. nilidhani sasa tunapaswa kuangalia kuwa bunge la sasa linashiriki vipi kuleta maendeleo ambayo yamekuwa yakinadiwa na wagombea na si kurudi nyuma na kuanza kuangalia huyu ni nani na yukoje.

    ReplyDelete
  29. Michuzi hakiki list ya wabunge wa chadema. Kwenye list umeweka majina 24, wakati kwenye heading chadema itakuwa na wabunge 23. Naona utakuwa umedesa kwa mwananchi b'se ndio walioadkika hivyo.

    ReplyDelete
  30. chadema oyeeeeeee tunatisha

    ReplyDelete
  31. HONGERA MWALIMU WANGU WA CBE, MAMA NAOMI KAHIULA(MAMA WA GWAMAKA KAHIULA (G.K) NAKUAMINI UTAPELEKA CHANGAMOTO BUNGENI KWANI ILALA HAWAKUJUA UMUHIMU WAKO,KARIBU SANA MJENGONI....

    ReplyDelete
  32. mie kuna kitu ambacho hivi kama mnaanzisha chama siunatafuta watu wakaribu yako na pia ikumbukwe muanzilishi wake ni Mtei sasa wa nyumbani kwake wengi ni wachaga hilo nafikiri halina ubishi sasa na pia ukiangalia walioelimika zaidi sana ni wachaga kubali au kataa upo hapo anoy namba 30% upo sasa ukija ccm ndio udini usiseme asilimia kubwa ni waisilamu na je najiuliza iweje familia ya kikwete ndio ilikuwa front line watu wengine walikuwa wapi au ndio mnataka kusema ccm ni ya familia ya kikwete !!

    ReplyDelete
  33. aaaahhhhh niliposoma koments nyingi hapo juu sijwaeza kuamini hadi sasa hivi kua tanzania bado kuna udini na ukabila kiasi hiki....chuki sana pia.

    nyie anonis wote mnaozungumza kuhusu chadema 90% wakristo, je tukiangalia CUF???

    je mbona hujatupa idadi ya wakristo na waislam ndani ya ccm??

    je mbona hujatupa idadi ya wapemba na waunguja bungeni??

    mbona hujatupa mikoa yenye idadi kubwa ya wapinzani??

    je mbona hujasema rais wa jamhuri, makamu, nk ni waislam sio wakristo??

    je mbona hujasema serikali ya z'bar top wote ni waislam sio wakristo??? nk

    kwa staili hii nimeamini kua yaliyo moyoni mwa watanzania sio maendeleo bali mamjungu njaa fitina, chuki, lawama , umasikini, tabu,shida,ubinafsi, nk nk nk

    ninawashauri hebu tusahau udini, ukabila nk then tuangalie nani mwenye sifa husika tumpe nafasi akishindwa pia kuna uhuru wa kubadilisha na kumpa mwingine kwa kufuata taratibu husika kama vile kupiga kura japo ni jambo la kushangaza hamtokei kupiga kura mnabaki kupika majungu.

    pia tuwe wchapa kazi sio kukalia majungu sio mtaji hata kidogo

    kwa hali hii ni bora watumwa ulaya kuliko walio huru Tanzania.

    mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  34. wakristo wana elimu baba, waislamu elimu ndogo!

    ReplyDelete
  35. Cuf ni chama cha zanzibar na wale msiojua zanzibar ni asilimia 90 waislam hivyo wanasiasa wake wote watakua waislam. Tanzania bara ni 50-50 ndio maana watu wana uliza Chadema ni wakristo pekee?

    Kisheria Tanzania makamu wa rais lazima atoke bara hivyo atakua muislam na rais wa tanzania ni ki awamu miaka 10 mwinyi, 10 mkapa , 10 kikwete na labda kumi zijazo ni mkiristo. Ama Chadema ina weza kubadilisha hiyo kwa kuleta udini wake. Mnao bisha mbona Chadema wengi wao ni washungaji?????

    ReplyDelete
  36. kama hoja ni elimu, mbona 70% ya wabunge wa chadema wa viti maalum hawana digrii?

    ReplyDelete
  37. Tutaibomoa chadema kama tulivyoibomoa nccr mageuzi kwa kuwa chadema si chama cha watu wenye busara. Let the countdown begin!!!!! I'm loving this!!!!!!

    ReplyDelete
  38. na bado....si mlikuwa mashabiki wa CCM, mtalia sana mpaka ifike 2015....mimi sioni umuhimu wa hivi viti maalum...tulihitaji mtu ambaye angeenda kutetea mabadiliko ya katiba!

    ReplyDelete
  39. Viti maalum vilichagizwa na CCM, na wao ndio wanaofaidika zaidi kama ilivyo kwenye ruzuku ya Wabunge(angalia wake zao, washirika na maveteran)! Kwa kuwa ni viti vya upendeleo,ugawanyaji wake lazima utakawa na maswali mengi. Chadema walizuia uteuzi, wakaomba ushauri jinsi ya kuvigawa. Ukaskazini/Udini......!naamini nchi yetu hakuna mtu amewahi kufaidika kwa udini au ukabila(ni KINYAGO tu, tunatishiana kwamba kinang'ata), mwenye mifano na atowe! Cha kujiuliza!....watu wa kaskazini wamejitolea kiasi gani(hali na mali) kuisimamisha CHADEMA hapo ilipo!!? NI ASKARI GANI AENDAYE VITANI KWA GHARAMA YAKE MWENYEWE?..........JE? ASIYE FANYA KAZI NAE ALE?

    ReplyDelete
  40. Bwana asifiwe/A/w. Nijuzeni kazi za wabunge maalumu mjengoni ni nini?

    Wanawakilisha nini je wanakuwa na sifa gani hadi wachaguliwe.

    Mbona wengi mno sana, vipi posho zao ni sawa na za wabunge? kama hivyo basi serikali ina fedha isitudanganye wananchi ituboreshee huduma za kijamii yaani 104, wabunge, na wengine kibao?

    ReplyDelete
  41. huna akili wewe unayesema ni mkoa mmoja, ungewaambia babu zako wasome tokea zamani sio kulaumu mkoa mmoja, kama umetumwa na ndugu zako CCM kutoa comment zisizokua na maana bora ukae ufanye shuhuli zingine. Pschs.

    ReplyDelete
  42. JAMANI NAFASI ZA MAJIMBO MENGI ZILIKUWA WAZI KWA CHADEMA HATA KUSHINDWA KUSIMAMISHA WAGOMBEA, MLIKUWA WAPI KUWASHAWISHI WAGOMBEA WA DINI ZENU WAZIBE NAFASI ZILIZO WAZI? AU NYINYI WENYEWE KUGOMBEA? ACHENI SIASA ZA UDINI.. NADHANI NI ELIMU TU YA URAIA MMEKOSA. NYINYI NDIO MSIOPIGA KURA HALAFU MNALALAMIKA MGOMBEA WENU HAJACHAGULIWA. NI HAYO TU

    ReplyDelete
  43. MNISAIDIE KUPATA DATA KAMILI JUU YA WABUNGE WA VITI MAALUMU WA CHADEMA NA MIKOA WANAYOTOKA NA MAJINA YA WAUME ZAO KAMA WAMEOLEWA."NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK" MAO

    ReplyDelete
  44. Ile kiukweli kabisa wabunge wa kuteuliwa ni wengi mno, wengi wao hawana mchango wowote wa maana, ni mzigo mkubwa sana kwa walipa kodi wa nchi yetu.

    ReplyDelete
  45. wabunge wa kuteuliwa ni wengi mno. Siamini kama wana mchango wowote wa maana. Nawaoana ni mzigo kwa walipakodi wa Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...