Uongozi wa CCM Tawi la Uingereza unayofuraha kubwa kuwajulisha watanzania wote na wakereketwa wa CCM waishio Luton na Dunstable kwamba tutakuwa na Ufunguzi Rasmi wa shina la CCM LUTON.

Sherehe za Ufunguzi zitafanyika Jumapili tarehe 12.12.2010 kuanzia SAA SITA KAMILI MCHANA - CHILTERN HOTEL LUTON - WALLER AVENUE – POSTCODE LU4 9RU.

Kadi za Uanachama zitakwepo kwa wanachama wapya, pia tutakuwa na chakula cha pamoja na vinywaji kwa kuchangia £10 tu siku ya ufunguzi.

Pia kutakuwa na Uchaguzi wa Viongozi wa shina.

Tafadhali wasilisha (confirm) ushiriki wako kwa Mwenyekiti wa maandalizi katika shughuli hii ABRAHAM SANGIWA kwa kutuma ujumbe kwenda namba 07833571100 au Katibu ALBERT NTEMI namba 07506719300.

Asante na Karibu sana.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. jamani mi naomba kuuliza kwa uzuri , hivi hayo matawi ya ccm kila sehemu ya ugaibuni ni kwa ajili gani na yanasaidia nini , kwnai naona sikuizi watanzania wanaona bora kufungua tawi la ccm kuliko kufungua ummoja wa watanzania uko nje ! Au ndo njia ya kulaji tu!


    Mdau PAris

    ReplyDelete
  2. watoto wa Mujini wanasema....IMEKULA KWAO!!!!ahahaaha hampati kitu hapa Luton.

    ReplyDelete
  3. kweli kabisa ndugu,hata kura hawaruhusiwi kupiga hapo sielewi,mimi naona wengi wao ni usanii wa aina fulani.

    ReplyDelete
  4. Fanyeni kazi huko, wacheni siasa.

    Nafasi zote za kugombea na kuteuliwa zimeshajaa.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  5. Paris hakuna ulaji ila vyote ni part ya community,vyama au jumuiya zina saidia sana hasa kwenye misaada.Jiunge

    ReplyDelete
  6. Tupo pamoja na jamaa hapo juu Sat Nov 27, 05:37:00 PM, kwamba watz waliopo majuu wanafurahisha sana, badala yakujiunga pamoja kutokomeza umaskini vijijini na kuwapa maisha bora ndugu, jamaa, watz wenzetu walipo kwenye hali mbaya hasa vijijini sisi tunakimbilia kuanzisha matawi ya ccm kwajili ya nani?
    Hili jambo linaniumiza sana kichwa kwan kwamtajii huu tz kuendelea ni majaliwa ya mungu. Embu watz tubadilike achana na mambo ya chama majuu tuchape kazi kama kusoma tusome tuchangishane tutowe mawazo, tukasaidie nyumbani jamani.

    Mdau France.

    ReplyDelete
  7. Haloo haloo watu wataumwa sana mwaka huu na ujao, matawi ya CCM yatafubguliwa kila pembe ya dunia. Cha ajabu wanachama wa vyama vingine wana matawi nje na kutwa wanakutana lakini ikiwa kwa ccm ndio nongwa!

    ReplyDelete
  8. Kwa maoni yangu, haya matawi hayana mpango wowote wa kuisaidia nchi mbali na kutafuta connection na viongzi wakubwa wa ccm,, waseme wamefanya kitu gani ambacho kinawasaidia huko ughaibuni au hapa nyumbani.

    ReplyDelete
  9. Only folks with small mind and time to waste will even think about doing this bs about opening up CCM branches overseas. Civilized and smart folks with critical thinking will NEVER do this bs.-Tanzanian in U.S.

    ReplyDelete
  10. We michuzi kichwa kama chupi ya kimasai kwa nini imebana meseji yngu?? shetwan adualahu wahed shwain!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...