Mtaalam wa Magonjwa ya Saratani katika Hospitali ya African Medical Investments ya jijini Dar es Salaam,Dkt. Rajiv Rao akifafanua jambo mbele ya wanahabari waliofika leo katika mkutano uliofanyika kwenye hospital hiyo,iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Dharula katika Hospitali ya African Medical Investments ya jijini Dar es Salaam,Dkt. Sabrina Kazia akifafanua jambo kuhusu ugonjwa wa Saratani ya Matiti leo katika mkutano na waandishi wa habari.
Baadhi ya wanahabari pamoja na madaktari wa Hospitali hiyo wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

Kwa kipindi cha miaka mingi, dhana ilijengeka kwamba saratani ya matiti lilikuwa ni jambo ambalo liliwaathiri zaidi wanawake kutoka bara ulaya ambao walikuwa kwenye umri wa miaka ya kati kutoka kwenye familia tajiri katika nchi zilioendelea, na kwa muda Fulani, dhana hii ilikuwa sahihi.

Hata hivyo, sura ya saratani ya matiti inabadilika kwa kiwango cha waathirika kuongezeka kwa takriban mara saba katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

“Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kiwango cha saratani ya matiti ni asilimia 16 ya waathirika wote wa saratani duniani ambao ni wanawake, jambo ambalo linaifanya kuwa saratani iliyoenea zaidi ambayo si saratani ya ngozi, miongoni mwa wanawake wote duniani,” anaelezea Dk. Amit Thakker, Afisa Mtendaji Mkuu wa muda wa African Medical Investments plc (AMI).

“Hii ni saratani inayoongoza katika kuwaathiri wanawake kwenye nchi zinazoendelea na zilizoendelea, huku saratani ya shingo ya kiazi ikifuatilia kwa karibu, na kuchukua nafasi ya pili. Takriban matukio milioni 1.3 hutokea na kutambulika kila mwaka, duniani.

Barani Afrika, takriban waathirika wapya 20 kwa kila watu 100,000 yanasajiliwa na kiwango hiki kinaongezeka,” aliongeza Dk. Thakker.

Kwa mujibu wa WHO, takriban wanawake 87.9 kwa kila wanawake 100,000 nchini Uingereza walibainika kuwa na saratani ya matiti mwaka 2008, ikilinganishwa na kiwango kidogo cha wanawake 19.3 kwa kila wanawake 100,000 kwenye nchi za Afrika Mashariki. Hata hivyo, WHO inafanua kwamba idadi hii inatokana na kiwango kikubwa cha uelewa wa utambuzi wa awali nchini Uingereza, jambo ambalo si la kawaida kwenye nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania.

Dk. Nimfa Ranido, daktari mkazi wa magonjwa ya wanawake kwenye Hospitali ya AMI, jijini Dar es Salaam anaunga mkono hoja hiyo na kusema “Saratani ya matiti inatibika lakini mara nyingi zaidi tunapata wanawake wanaofika kutibiwa huku athari za ugonjwa zikiwa zimefikia hatua za mbele zaidi.

Barani Afrika, uelewa wa saratani ya matiti na utambuzi wa awali ni muhimu sana katika kupambana nayo; iwapo saratani ya matiti itabainika mapema, itakuwa rahisi zaidi kuitibu katika hatua hiyo. Wanawake wengi wa Kiafrika hawana ufahamu wa kujifanyia utambuzi wao wenyewe au jinsi ya kuwezesha matiti yao kukaguliwa, hivyo, elimu na kuongeza uelewa ni muhimu sana.”

Kwa kuwa mwezi Oktoba ni mwezi wa kuhamasisha uelewa juu ya saratani ya matiti, AMI wameamua kuendesha kampeni ya uelewa huo kupitia Hospitali na Zahanati ya Mwanamke Mwenye Afya Njema (Well Woman Clinic) jijini Dar es Salaam, Tanzania.

“Sio tu kwamba mtazamo wetu ni kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa wetu, lakini tunataka kuwawezesha na kuwaelimisha juu ya afya zao ili waweze kubakia na afya njema kila wakati,” aliongeza Dk. Ranido.

Dk. Ranido anaeleza kwamba wanawake walio katika umri wa kati ya miaka 20 na 30 wanapaswa kuwa na ukaguzi wa matiti wa kitaalam (clinical breast exam – CBE) kama sehemu ya kawaida ya ukaguzi wao wa afya wa mara kwa mara, ambao unafanywa na mtaalam wa afya, angalau kila baada ya miaka tatu.

Wanawake ambao wana zaidi ya umri wa miaka 40 wanapaswa kushauriana na daktari wao juu ratiba ya kufanya kipimo cha afya cha matiti (mammogram).

“Licha ya hayo yote, ukaguzi wa matiti unaofanywa na mwanamke mwenyewe ni (breast self-exam-BSE) ni muhimu sana kwa wanawake walio katika miaka 20.

Kama utakuwa na utaratibu wa kujikagua mara kwa mara, utatambua jinsi matiti yako yanavyokuwa na jinsi unavyoyahisi yakiwa katika hali ya kawaida, na utaweza kutambua dalili zozote zilizo tofauti mapema ili uweze kuzungumza na daktari wako mapema iwezekanavyo,” alisema Dk. Ranido.

Kuna dalili mbali mbali ambazo wanawake wanapaswa kuzitambua, kama vile uvimbe ndani ya matiti, mabadiliko ya umbo na ukubwa wa titi, na ni muhimu sana kuongea na daktari wako iwapo utakuwa na shaka au maswali yoyote kuhusu afya ya matiti yako.

“Katika jitihada zetu za kuongeza uelewa wa saratani ya matiti miongoni mwa wanawake barani Afrika, Zahanati yetu ya Mwanamke Mwenye Afya Njema itatoa huduma zilizopunguzwa gharama kwa kipimo cha mammogram kwenye miezi ya Oktoba na Novemba mwaka huu.

African Medical Investments ni wabia na washirika wako katika vita dhidi ya saratani ya matiti,” anahitimisha Dk Thakker.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. VIWANGO VYA MAAMBUKIZI YA SARATANI YA MATITI VYAONGEZEKA - AMI??????

    Saratani ya matiti inaambukiza...I didn't know!

    ReplyDelete
  2. Saratani(Kansa) huambukiza??!!

    ReplyDelete
  3. Inaonyesha uelewo mdogo wa mada hii kutoka kwa mwandishi, andika kichwa cha habari kutoka kwenye maelezo na si kutoka kichwani kwako.Na pia ukubali kukosolewa.

    ReplyDelete
  4. Ndugu mwandishi wa maada: Maambukizi kwa lugha ya kiingerenza Infection or can also be loosely referred as transmission. Inaamaana ugonjwa unaweza kuenezwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia ya ute-mwili, hewa, kugusana and kujaamiana au pia kupitia wanyama na wadudu yaani Vectors. Sasa ndugu Mwandishi tunashukuru kwa taarifa lakini kichwa cha habari kina walakini. Saratani ya matiti... haimbukizi.

    ReplyDelete
  5. madaktari wa AMI ni mabingwa au?

    I am not sure if AMI have Oncologists hope nobody gets infected by cancer.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...