Rais wa CECAFA na TFF Leodgar Tenga akikabidhiwa Medali na Aliekua mkuu wa kamati ya maandalizi ya kombe la Dunia 2010 lililofanyika nchini Afrika Kusini,Danny Jordan.
Meneja wa kampeni ya Tuungane Kutokomeza Malaria,David Kyne akizungumza katika Mkutano Mkuu wa CECAFA katika hoteli ya Paradise jijini Dar es Salaam.Rais wa CECAFA na TFF Leodgar Tenga (wapili kushoto) akiwa na Danny Jordan mwenyekiti wa kamati ya FIFA World Cup South Africa (wa kwanza kushoto), afisa wa CECAFA pamoja na Afisa Mtetezi wa UAM,Anna-McCartney Melstad wakifuatilia mkutano huo uliofanyika mchana wa huu katika hoteli ya Paradise City,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar.
Aliekua mkuu wa kamati ya maandalizi ya kombe la Dunia 2010 yaliyofanyika nchini Afrika Kusini,Danny Jordan akimkabidhi medali,Afisa Mtetezi wa UAM,Anna-McCartney Melstad kwa ushiriki katika kombe la dunia kupitia kampeni ya UAM.


Leo tarehe 26 Novemba 2010 hapa Dar es Salaam, katika mkutano wa waandishi wa habari kufungua mashindano ya Tusker Challenge yanayo anza kesho, washiriki na wadau wa kampeni ya “Tuungane Kutokomeza Malaria” - United Against Malaria (UAM) wameungana na wandaaji wa mashindano kumulika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Eneo hili la Afrika watu wapatao Milioni 38.9 huugua Malaria miongoni mwao wakiwa watoto.

Zaidi ya watu 209,000 hufariki kila mwaka ikiwa ni karibu robo ya vifo vyote vya malaria vinavyotokea barani Afrika. Malaria ni ugonjwa unao zuilika na kutibika ilihali kila sekunde 45 mtoto mmoja hufariki kwa Malaria na kusababisha hadithi za huzuni na umasikini.

Rais wa shirikisho la mpira la CECAFA Ndugu Leodegar Tenga alisema,” Mchezo wa mpira wa miguu unataka jamii yenye afya ili uendelee na kukua. Wanahitajika makocha, wachezaji, wasimamizi, marefa na hasa mashabiki wenye afya. Bila watu wenye afya hatuwezi kuendeleza soka. Jamii yenye Malaria haina afya, ndio maana tunaunga mkono juhudi za kutokomeza malaria zinazofanywa na kampeni ya United Against Malaria”

Timu 12 za Afrika Mashariki na Kati pamoja na washiriki wageni kutoka Malawi, Zambia na Ivory Coast zimekusanyika hapa Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano ya CECAFA, uongozi wa juu wa CECAFA umetangaza kushiriki kikamilifu katika kampeni za kutokomeza Malaria na kuhakikisha wanatumia mbinu zote za kuzuia wachezaji kupata Malaria ikiwa ni ahadi yake ya kujiunga na kampeni ya UAM.

“UAM imepata ushirikiano wa hali ya juu kutoka CECAFA, hii inadhihirisha dhamira yao ya kushiriki katika vita dhidi ya Malaria.” kasema David Kyne, Meneja wa kampeni ya UAM. Mashirikisho ya soka, timu za mataifa na wachezaji watatumia umaarufu wao katika michezo kuelimisha jamii zao dhidi ya umuhimu wa matumizi ya njia zote zinazoshauriwa na wataalamu za kujikinga au kutibu Malaria kama vile vyandarua, kupima na kutumia dawa endapo wataambukizwa malaria.

Ili kuthibitisha jitihada za sekta binafsi kuunga mkono kampeni ya UAM, mdhamini wa mashindano ya CECAFA atashawishi makampuni mengine yajiunge na kampeni na kusisitiza umuhimu wa wafanyakazi na wateja wao kuwa salama kwa kutumia kinga ama tiba dhidi ya Malaria.

“Kama wadhamini wa CECAFA Tusker Challenge Cup 2010 tunaungana na kampeni ya United Against Malaria kwa kuhakikisha wafanyakazi wetu wanapata kinga na tiba dhidi ya Malaria kwa muda wote.” Alisema Caroline Ndugu, Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Limited. Aliongeza ”Leo hii tuna ahidi kununua vyandarua vyenye dawa ya kuzuia mbu wa Malaria kwa wafanyakazi wetu wote hapa Tanzania”

Njia mbalimbali za kufikisha ujumbe wa malaria kwa jamii ambazo zitatumika muda wote wa mashindano ni pamoja na matangazo yatakayorusha katika vyombo vya habari kama redio, runinga na mtandao wa internet, mabango yenye ujumbe wakati wa kila mechi na nguo za mazoezi ya awali kwa timu kabla ya mechi pamoja na ujumbe kwenye programu ya mashindano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bw. Michuzi salamu zangu zikufikie hapo Dar. Jamani hebu tujiulize maendeleo ya soka ya TZ yanaenda wapi? Kuandaa mashindani tu bila ya kuwa na mikakati mizuri tutafika kweli. Naamini kule Zanzibar wangepata robo tu ya udhamini unaopata TFF basi wangefika mbali. Mimi naona sasa ule ule ukweli kwamba Tenga ni sawa na Kalusha Bwalya. Sioni jipya kwake . Na hiyo formula maendeleo katika timu ya taifa tu si maendeleo kwani hebu niambieni kama kuna back up team kocha angemuita tena Mwaikimba? Ni kwamba hana wachezaji. Leo tunajionea Ancelloti anavyochomekea vijana Chelsea, ona Liverpool ona Arsenal pamoja na timu nyingi ambazo zina vijana wengi. Tunaposema vijana hatuna maana tayari mchezaji ana umri wa miaka 18 au zaidi ndio unaanza kusema kwambandio programu. Sio. Tuanataka kuona vijana miaka 10-12 wakipewa mafunzo mahususi na kuandaliwa mapema. Kweli leo tuwaweke vijana aina hiyo na kuwaandaa tutakosa timu ya taifa? Kocha wa taifa wa Mauritius aliyetimuliwa amenena kwamba hakuna wachezaji wa kutosha kuwa na timu imara ya taifa wakamuona mnoko. Wamekwenda Senegal wamepigwa 7-0. Sasa na Tenga wakati umefika wa kupata mpinzani. Uchaguzi uje tupate mabadiliko hatutaki mambo ya PR kupiga picha na huyu na yule lakini substance hamna. Tenga ni kama Kalusha na chama cha soka cha Zambia utata mtupu.

    ReplyDelete
  2. Duh. Huyu mdau kiboko. Mimi naungana nae kwamba kabla ya kukurupuka kuandaa mashindani tujiandae vizuri. Tenga na na kina Kayuni na zamani Kaijage ni kashfa tupu. Unakimbilia CECAFA kutaka ulaji hana chochote cha maana. Na sasa Mwakalebela ameondoka tutajionea madudu mengi. Mwakalebela kama Mtendaji Mkuu alimbeba sana Tenga sasa Kayuni anashika wadhifa huo nyufa zinaonekana. Wanafungia wachezaji bila ya mantiki na ushahidi tata. Nadhani kuwa Administrator wa mpira si lazima ucheze mpira. Muhimu uwe na timu ya washauri wazuri basi mambo mbele kwa mbele.Mpaka leo najiuliza rafiki yangu Magori kilichomkimbiza TFF ni nini na yeye alikuwa mtu very ambitious? Hatupati jibu. Mpira wa Bongo shaghala balak uongozi bado tatizo.

    ReplyDelete
  3. gud chest.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...