Home
Unlabelled
WABUNGE WA CHADEMA WASUSIA HOTUBA YA JK
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Chadema sasa wataharibu Nchi yetu soon sioni walichofanya ni cha maana kabisa. angalau CUF wanajuwa nini wanafanya kwa kujali Maisha ya wananchi wa Tanzania Bara na visiwani ni muda wa kukamatana na kuiweka nchi pazuri. MZ
ReplyDeleteHeko CHADEMA. Tuko pamoja.
ReplyDeleteBaker,
London.
CHADEMA hayo ndiyo mambo. Huku Zanzibar tulifanya hivyo watu wakatucheka, sasa si mnaona CUF tumo serikalini. Endeleeni hivyo hivyo. Tanzania siyo ya CCM tu.
ReplyDeleteHuku ndio kukua kwa demokrasia. Chadema awaharibu kitu isipokuwa wanatuma ujumbe kwenye jumuiya ya kimataifa ya kwamba awakubaliani na katiba na sheria zilizopo. CUF wamefanikiwa kuingia kwenye serikali ya Mseto Zanzibar. Naamini Chadema ndio wanakoelekea. If you can't beat them, join them.
ReplyDeleteinawapa faida gani haswa? jiinga chadema!Mnatumikia kwa kuwa bungeni au mnawakilisha majimbo yenu? Hizi form seven bwana taabu tupu.
ReplyDeleteLOSS OF DIRECTION...
tatizo maskini akipaata matako hulia mbwata. chadema wanajiona wamekuwa wengi na spesho. utoto mtupu, eti jumuiya ya kimataifa. wasusie na vikao vya bunge kama wasipate posho. stupid. eti hutambui matokeo turudie na majimbo yao walioshinda. umbeya tu
ReplyDeleteKazi kweli kweli, hivi with all permutations walitegemea wangeshinda 2010?! kweli ngumbalo ni ngumbalo 2!
ReplyDeleteSadiki
Ndiyo hayo mdau mmoja aliyesema katika postings za awali. Dua la kuku halimpati mwewe. Chura hamzuii tembo kunywa maji! Mradi JK anatambulika na overwhelming majority ya Watanzania na anatambuliwa na EAC, AU, Commonwealth, UN, nchi zooooteee duniani, pamoja na African Development Bank, World Bank, IMF, hao wabunge wa chadema hawajafanya kitu. Ndoo moja ya maji haikaushi ziwa. Nina hakika kesho watakuwa wa kwanza kupanga foleni ya posho zao! lol!!!!!!!
ReplyDeleteUtoto mtupu. Asiyekubali kushindwa........
ReplyDeleteNext step in achieving democratic rights: wasusie malipo ya ubunge. Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteRidiculous!!!!! siasa za chuki binafsi hazitawasaidia kyadema.
ReplyDeleteChadema vichwa maji. Waanze kutumia akili badala ya kusukumwa na jazba. Jazba adui ya busara.
ReplyDeleteTWO THUMBS UP UP UUUUP!! chadema awataki kupelekeshwa bwana kinaeleweka kama JK kashinda lakini wanataka number za ukweli.wanataka namber za ukweli za SLAA pia,sio kupunjwa punjwa kura ili ionekane kama JK kashinda kwa kipigo kikubwa.thats not fair at all!
ReplyDeleteNdo maana yake mimi fagilia CADEMA all the way!na kama ni vita iwepo tuu wamezoea CCM mpaka watolewe kwe mapanga hao,wanakuwa kama Mugabe,kushikilia madaraka tu atakama wananchi wamewachoka,GO CHADEMA GO CHADEMA ME LOVE YOU ALL LONG TIME
CHADEMA GOT BALLS! !MWAAAAAHHAAAAA(kissess)
ReplyDeletemi naona ingekuwa pouwa kama mngesusa kila kitu, hata hapo bungeni msingekwenda mkaacha
ReplyDeleteChildish na jazba za kijinga tu hizo.
ReplyDeleteJAMANI WEWE ANO.8.39PM LAZIMA UELEWE NA USOME NINI CHADEMA WAMESEMA. WATAKUWEPO BUNGENI KUWAKILISHA WANANCHI KAMA KAWAIDA KWENYE VIKAO NA MASWALA YA WANANCHI. ILA RAIS AKIHUTUBIA HAWATAKUWEPO KWANI HAWAMTAMBUI RAIS. CHADEMA WANAKUBALI KUWA RAIS AMESHINDA ILA WANACHOTAKA NI HESABU ILIYO SAHIHI NA SIO 61% KAMA WANAVYODAI. KUWEKWA KWA HESABU KAMILI NDIO UKWELI WENYEWE. CUF WAMESUSIA HOTUBA ZA RAIS KWA MIAKA 15 NA HAKUNA MTU ALIEONA SHIDA. HATIMAYE KATIBA IMEBADILISHWA NA WANANCHI KUPATA HAKI YAO. CHADEMA WANAFANYA MAMBO KWA AMANI NA KUPIGANIA HAKI YA WANANCHI. HII NI MESSAGE KWA SERIKALI YA CCM KUWA IS NOT BUSINESS AS USUAL, MACHO YA KWAKO KWENU. THEREFORE WATCH OUT, WATANZANIA SI WADANGANYIKA ANY MORE. GOOD CHADEMA NA WANANCHI TUKO PAMOJA NANYI, WAY TO GO DR.SLAA.
ReplyDeleteyamewafika wenzetu, maji yamewazidi kimo, hawana la kufanya ila vituko kama hiyo ya walk-out. Ama kweli chadema wamefilisika kisiasa na (mbaya zaidi) hawatumii busara.
ReplyDeleteCHADEMA mtindo huu wa Siasa za Shangwe umepitwa na wakati hasa ktk Taifa lenye uchumi unaohitaji changamoto za mawazo ya kusonga mbele.
ReplyDeleteHii ni kushiriki Demokrasia isiyo na NIDHAMU hasa kwa Watanzania waliowatuma kuwawakilisha BUNGENI.
Watanzania mliowachagua hawa ndugu mjue imekula kwenu maana wao mishahara watavuta kutoka kwenye KODI zenu.
Kwa kweli vijana wenzetu bila kujali ITIKADI ya vyama, sikutegemea hata wewe Zitto, Halima Mdee,Mnyika na Vincent Nyerere kuwakebehi wananchi waliowachagua nyinyi na Rais Kikwete kwa kuondika nje ya BUNGE lao tukufu.Hii ni HAKI yenye AIBU.
Siamini kama mlimshirikisha Mhe. Mabere Marando kusaini mishahara yenu na kwenda kupunga upepo kwa ufahari nje ya Bunge wakati linafunguliwa rasmi.Haya yangefanyika kwenye jukwaa la kongamano au siasa za halaiki.
Bila shaka hamkutaka kusikia na kukubaliana na wito wa Rais kuwa nyinyi wabunge mtumie muda mwingi kuwasikiliza wananchi.
Je,mtatoka mara ngapi?.
Na kwa idadi yenu mtaathiri maamuzi ya Bunge kwa utaratibu wake kusaidia wananchi kwa kiasi gani?
Kwa shida na mahitaji ya wananchi bado wana wakati wa kusikiliza utetezi wa ilani ya chama cha siasa au utekelezaji wa Serikali ya Chama kilicho madarakani.
Mhe. Lisu,kaka yangu msomi, hizi siyo mbinu ktk harakati za mabadiliko ya kisasa.Nchi yenu ilizitupilia mbali hata wakati wa kudai UHURU. Nilidhani unazijua na utawaongoza wenzio vizuri kwa mbadala angalau wenye mkakati...
Halima Mdee, nisikilize kwa makini. Tanuru unalopita limeziba mbele na mwanga uonao ni moto mkali. Hujafika mbali Geuza mkakati,maana nyota yako ktk siasa za kitaifa hazifai kuchomeka kizembe kwa kuongozwa na vipofu wa mkakati ulioshindwa kabla haujaanza.
MAINA ANG'IELA OWINO.
Mahatma Ghandi alisema "usimwamini mtu aliye tayari kumwaga damu kwa uchu wa madaraka". Sasa chadema wanaonyesha makucha yao baada ya ngonjera zao za kampeni ya danganya toto kuambulia patupu!!!
ReplyDeleteWatoke tu!!! Haina impact yoyote hiyo!!!! Mwisho wa siku, wabunge wa chadema watapewa malipo yao na wasio na nyumba (wengi tu) watajenga majumba ya kifahari.
ReplyDeleteMimi niko hapa Dodoma. Naapa kuwa nimewaona wabunge wawili wa chadema (nitaminya majina yao) wakila chips na kuku katika hoteli niliyofikia huku wakitazama hotuba ya Mheshimiwa JK kwenye TV. Tena mmoja wao alimwambie mhudumu (waiter) aongeze sauti ya TV. UUUUWWWWIIIIII!!!!!!!!!
ReplyDeleteJamani sasa kama hawamtambui JK kama rais watamsikilizaje? Bado wanastick na msimamo wao. Wangebaki na kumsikiliza JK mngesema hawana masimamo. Hiyo ndio demokrasia. Taka usitake.
ReplyDeleteGo all the way chadema, BOYCOTT YOUR ALLOWANCES. Hapo ndipo tutajua kuwa mko siriaz na mmemin bizness! Tesha78.
ReplyDeleteWANAFIKI TU HAO! Wasiingie bungeni kabisa waende wakafanye kazi kwenye majimbo yao kwa pesa zao. Wakisusa ndio serikali itaacha kufanya kazi? Au Bunge ndio litasimama? Idadi ya wabunge waliobaki wanatosha kupitisha miswada inayotakiwa kupitishwa kususa kwao hakutaathiri chochote!
ReplyDeleteKAMA WASUSAJI KWELI WASUSIE POSHO NA MASHANGINGI YA WABUNGE, SI YANATOLEWA NA SERIKALI YA CCM. SASA WATAPOKEAJI VYOTE HIVYO KUTOKA SERIKALI WASOITAMBUA! HOVYOO!
Tz oyeeeeee!
ReplyDeleteChadema moto chini,msisubiri uchaguzi ujao! mabadiliko yanaitajika mapema iwezekanavyo, CUF walikuwa wagumu mpk wamepata nafasi kwenye serikali visiwani. Bara tunasubiri nini?
CCM madarakani mpk lini? tumechoshwa tunahitaji mabadiliko, vijana tunahitaji nafasi za kazi, Chadema na upinzani kwa ujumla watatuwezesha.
CCM ni mambo ya kurithishana ubunge na uongozi,na kukumbatia mafisadi. Je sisi tusio na wazazi ama ndugu wabunge na viogozi itakuwaje? naona TZ imekuwa aliye nacho uongezewa, na asiye nacho unyanganywa!
Kuna mapungufu mengi TZ, CHADEMA na wapinzani wengine fanyeni kazi ya kutuokoa.
tunahitaji demokrasia ya kweli sio mambo ya undugunaisation
keep it up
Watanzania bwana,hiyo ndo demokrasia!
ReplyDeleteChadema hawajavunja sheria yeyote na sioni lililo haribika,kama ni hotuba ilitolewa na mkasikia bila tabu sasa nini tatizo?
Hata irak juzi walitoka bungeni itakua chadema.
Hiyo ni massege kua hawakubaliani na mambo yalivyo enda.
Saafi sana CHADEMA, mnaendelea kutoa somo kwa Wabongo ambao bado wamo usingizini - eti jazba! Huo ndio ukomavu wa kisiasa - of course itakichukua kizazi kingine kimoja cha wadanganyika kuja kutambua kuwa mnachokifanya ni kwa manufaa ya wanyonge. Wadanganyika wenzagu, jamani hili ni somo, ni mada ya kuendeleza mjadala juu ya demokrasia. Bila malumbano wajanja wachache watazidi kutuweka mifukoni. Wembe ule ule CHADEMA.
ReplyDeleteWAPUUZI KWELI, HIVI WAO WAKATI WA KUHESABU KURA KILA KITU SIWALIKUWA NA MWAKILISHI WAO..SASA WANATAKA WAAMBIWE MATOKEO KAMAYA ZNZ AU....KUJAZA WATU KWENYE MIKUTANO HAIMAANISHI NDIO MMEPIGIWA KURA. KILICHOBAKI NI KUCHUKUWA HIZO POSHO NA KUMCHANGIA SILAHA WENU ILI AWEZE KUISHI MJINI NA MKE MPYA MAANA ANAHITAJI HUDUMANYINGI NA HAJAAMBULIA KITU. LAZIMA AOTE MVI MARA MBILI.HAHAHAHAHHAHA
ReplyDeleteNA TUTAONA KAMA HATA HAYO MAGARI MTAKAYOPEWA MTAYATOA MSAADA KWA WANANCHI WENU WANAOPATA SHIDA. HV NANI HATAKI RAHA...LEO MDEE/ SUGU AU KABWE APEWE GARI NA NYUMBA WAKATAE ETI KISA WATANZANIA NI MASKINI...........THUBUTU YENU
Wajomba wa CHADEMA:
ReplyDeleteKARAGA BAHO NA UBOZI WAKO!!!!
HONGERA CCM HONGERA!!
Watainama watainuka CCM tuuuuu!
Hivi wanataka kuwadanganyana nani hao CHADEMA?
Wameshindwa Makaburu, wameshindwa Wareno, wameshindwa kila aina ya takataka itakuwa wao!!
Wengi Nchi hii bado wajanja wanatambua nani anafaa kuwa Kiongozi wao!
NI JK!!!!!!
WE MTOTO WACHA KULIA WEE WAACHE WATU WAONE WENYEWE!!!
Na Watu wameona.....NI CCMM TUUUU!
HONGERA JK, MTU WA WATU, MWENZETU USIE NA MAKUU ULIEBARIKIWA KULIONGOZA TAIFA LETU!!!
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!
Amina.
Mrudishe posho yenu ya siku au mshahara mzima wa mwezi, pengine!
ReplyDeleteLakini hatukuwapeleka huko Bungeni kufanya hayo majambo!
---
Mwana-Chadema
Mimi kwa kweli mmenishanngaza sana Chadema mlisubiri kuapishwa kama wabunge na kujionyesha kwenye magazeti kuwa mmekuwa tayari wabunge,sasa kwanini msinge pinga matokeo siku yanatangazwa mbona mlisaini ,sasa kama hamumtambui rais na baraza lake akichagua msilitambue muwe mnatoka nje kila siku mawaziri wakiwa wanajibu hoja halafu tuone,na leo 18Nov mheshimiwa spika wasisaini posho iwe imekula kwao,asiyekubali kushindwa si mshindani kwanza wengine hapo wa Chadema shule haijapanda mnafuata tu mkumbo kwa vile kasema mwenzetu tutoke bila kufikiria madhara yake,sasa kwa hili ndo mmesha kosa na kura za 2015,maana mnakuwa kama watoto eti baba kaja mnajificha uvunguni hamtaki kumuona,kwa sasa siasa zimekomaa kama humtaki mtu si unasubiri uchaguzi ujao,haooooooo
ReplyDeleteIMEKULA KWENU LEO YUHUUUUUUUUUU;POSHO POSHO TAMU BWANA
Bravo Chadema,
ReplyDeleteMimi napenda wapinzani wanaoiga mbini za wapinzani wenzao hasa wapinzani wakongwe. Unajua CUF ndio walioanzisha mbinu hii katika siasa za Tanzania. Sasa kule visiwani walianza kumsusia Salmini na baadhi yao wakatiwa ndani na kupigwa na baadae akaja Karume pia wakamsusia mpaka mwisho ukapatikana muafaka na sasa CUF wameingia serikalini. I hope baada ya kustahamili muda hivi Chadema watafanikiwa kama CUF. Lakini kuna uwezekano ususiaji huo ukawa na athari katika jamii kama ilivyokuwa kule Visiwani. Ususiaji wa visiwani haukuishia kwa Raisi tu bali kwa shughuli za serikali na hadi watu mitaani kususiana kama wanachama wa CCM kutouziwa vitu madukani na hata ndoa kuvunjika.Pia wawakilishi wa CUF walisusia miradi ya serikali majimboni mwao. Kwasababu ilikuwa haiingia akilini kumsusia raisi lakini mkaipenda au mkashirikiana na serikali yake. Sasa itakuwa busara pia kama Chadema watasusia shughuli zote za serikali ya Kikwete. Hapo watakuwa wamekamilisha mbinu zote walizozifanya CUF. Short of that wanaweza wasifanikiwe.
Once again. Big up Chadema. Kwa nyongeza wangemsusia na Mizengo Pinda ambae ndio mkuu wa serikali ya JK na bila shaka Pinda kachaguliwa na JK.
Michuzi siamini kwamba umetoa mawazo yote. Nahisi unavutia upande wa akina yahe wa CCM ambao hawafaidiki na chochote cha CCM. Haiwezekani kwamba Watanzania wote hawa wakawa na mawazo kama haya uliyotoa. Ukimnya ya kwangu basi, poa, tu. Najua uko serikalini na wewe.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba Chadema wanahitaji kutoa somo kwa vyombo vya serikali na CCM yenyewe. Kilichofanyika hakikuwa sahihi. Kura zilichezewa na ushahidi wanao.
Watanzania wanaoitukana na kudharau Chadema bado wako kwenye usingizi ama wana jambo jingine kabisa hapa ambalo hawawezi kulitaja. Wangeweka majina yao tungefurahi zaidi.
Chadema wameonesha ukomavu mkubwa kwa sababu hawakuita maandamano ili watu wapigwe; wala hakuanzisha fujo. Waliilalamikia NEC na wakapuuzwa, sasa mlitaka wakae kimya?
Hizi ni zama za ukweli; huna sababu ya kujificha. Kugomea hotuba ya JK ni kutuma ujumbe na haina uhusiano na uwakilishi wa wananchi wala uhudhuriaji wa vikao vingine vya Bunge na masuala ya posho.
Eleweni, hii ndiyo njia bora zaidi ya kutuma ujumbe, hata kama JK alipata asilimia 99 kama alizokuwa anapata Saddam.
Tanzania oyeeee! Idumu amani.
Hata mkisusa wenzio wala!!!!!!!!!
ReplyDeleteUNATAKA KUJUA UKWELI KUHUSU KELELE ZA CHADEMA KUIBIWA KURA???
ReplyDeleteUKWELI NI HUU!
1. Chadema inaongozwa kwa rimoti na watu wachache ambao wako nje ya nchi, hawa kwa kuwa wanachangia pesa zao huko basi kila wanalosema wanasikilizwa.
2. Hawa wanaaminiwa sana na Chadema kwa sababu wanaonekana wasomi na ndio waliokuwa mstari wa mbele kutuma sms na email za kashfa na matusi kwenye mitandao na hata kwenye simu.
3. Kundi hili la vijana hawa wachache ambao walikuwa na mategemeo makubwa ya kushika dola na kuingia ikulu kwa mgongo wa Chadema lilifikia hatua hata ya kudai kuwa mikutano ya CCM haikuwa na watu wengi ila ni photoshop ya kina Michuzi na si wingi wa wafuasi wa CCM.
4. Kundi hili ambalo lina mategemeo kuwa wataingia ikulu kwa nguvu yao hiyo ya kutokukubali matokeo linaamini kuwa DR SLAA ALISHINDA UCHAGUZI WA RAIS KWA KUTUMIA KIGEZO CHA IDADI YA WAISLAM NA WAKRISTO.
5. KWA KUTUMIA KIGEZO HICHO CHA IDADI YA WAISLAM NA WAKRISTO Na kwa kutumia takwimu za CIA ambazo wao wanaamini kuwa ni sahihi (Sijui ni lini hao CIA walikuja kufanya sensa ya kuuliza dini za watu TZ) wanaamini kuwa Wakristo ni wengi kuliko waislam. Kulingana na takwimu zao wanaamini kuwa Tanzania waislam ni 30% na Wakristo ni 70% hivyo basi kutokana na ufinyu wao wa mawazo na kuwa kwao nje ya nchi muda mrefu ndio maana walitumia kampeni zenye mrengo wa kidini zaidi (rejea email/waraka wao wa kugawanyika kura za waislam kati ya CCM na CUF)hivyo basi wanaamini kuwa JK hawezi kupata kura zaidi ya 30% ya kura zote. NA WANAAMINI KUWA DR SLAA KWA KUWA NI MKRISTO NA MCHUNGAJI atakuwa amepata kura za wakristo ambazo kwa mtazamo wao bapa ni 60% asilimia 10% wape vyama vingine vyote. Hayo ndio mawazo mgando ya hao vijana wanaojiita ni wanaharakati na ndio wanaowapeleka puta viongozi wa Chadema na kufanya maamuzi hayo mnayayoyaona Chadema wanayafanya. NA HUO NDIO UKWELI HALISI WA MAMBO INGAWA WENGI HAWAUJUI NA WANAOUJUA WATAUKANA KWA SABABU WANAFIKIRI WATU WOTE NI WAJINGA HATUJUI NINI KINACHOENDELEA!
This what they call democracy you ignorant people. They have a right to walk out. Chadema juu kwa juu!
ReplyDeleteNonsense! CHADEMA wamedisappoint sana. wasuse allowances kweli na wasipewe madaraka yeyote.This is childishness na contempt ambayo havumiliki. Why did they bother to swear at accepting na kulinda katiba etc. JK is their boss..full stop. if they don't like it , watoke bungeni and wajaribu tena in 5 years .Shame on them all , wanataka kuvuruga amani yetu kwasababu ya ubinafsi na uchu wa madaraka nyooooo! hatudanganyiki! this is nothing but a cheap publicity stunt .CCM hoyeeee!
ReplyDeleteChadema Tupo Pamoja. You will never walk alone.
ReplyDeleteMdau USA
yoooote yamezungumzwa ila mie nashangaa CHADEMA nilidhani wataleta mabadiliko ya kweli ktk bunge letu lakini tangia walivyoingia bungeni wako mstari wa mbele kuonyesha makeke sasa sijui wanataka kuonyesha wanajua sanaaaaa "MUCH KNOW" sisi wananchi hatutaki kuona mbwembwe zenu hapo bungeni suala ambalo nataka kulizungumza hapa ni kwamba kama uliangalia juzi kulikuwa na wabunge ambao wananadi sera zao ili waweze kuchaguliwa na bunge wawakilishe tanzania ktk bunge la SADC mimi nakuita bwana huo uheshimiwa wako siuoni TUNDULISU pamoja na ZITTO walikuwa wanawacheka wabunge ambao walikuwa wanatumia lugha ya kiingereza sasa unamcheka nani????? nadriki kusema nyie ni wapuuzi ZITTO NA TUNDULISU.....na TUNDULISU kumwuuliza mbunge swali halafu akashindwa kujibu sababu kubwa iliyokufanya umcheke ni nini?????? Nilifikiri mtakuja na busara lakini mnapoelekea Mh.ANNE MAKINDA anatakiwa awe macho na hao wenye kauli ya Pamoja tunaweza, mpaka kieleweke! inaamanisha nini mpaka kieleweke????? Ni maswali ya mimi mwananchi wa kawaida najiuliza najutia kura yangu kuipa CHADEMA najuta nimefanya kosa.....
ReplyDeleteNajuta kwa kweli kupoteza kura yangu kwa CHADEMA
One question to those who walked out of parliament, for real:
ReplyDeleteWHOSE INTERESTS ARE THEY LOOKING OUT FOR?
Dr. Slaa, katika ukurasa wake wa Facebook, leo ametoa sababu za wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK. Mimi kama raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa nangojea wahusika wajibu hoja hizi:
ReplyDelete-------------------------------
Wabunge wetu wamechukua uamuzi mgumu sana, uamuzi ambao unataka ujasiri na uthubutu wa vitendo. Ni lazima tuelewe kuwa mgogoro uliopo siyo na Kikwete kama Kikwete, la hasha bali na mfumo uliomuingiza madarakani safari hii, mfumo ambao tunautuhumu kuwa haukuwa huru na wa haki. Uamuzi huu haukuwa wa chuki binafsi au kisirani dhidi ya Kikwete kama Kikwete, bali dhidi ya mfumo ulioundwa na kulelewa na CCM na ambao umetuonesha kuwa hauwezi na haupaswi kulelewa kwa muda mwingine wowote ujao.
Kuanzia wakati wa kutangaza matokeo tulitoa malalamiko yetu kwa Tume ya Uchaguzi ili waweze kuyafanyia kazi ili mshindi apatikane katika mazingira ya haki na uwazi. Tume haikusikiliza na ikaendelea na mfumo wake mbovu wa kutangaza matokeo bila kujali malalamiko yetu. Tukazungumza hadharani juu ya kutopatana kwa matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa na tume na yale yaliyoko majimboni na kuomba tume wasitishe ili waangalie ushahidi tulio nao, tume haikusikiliza na matokeo yake wakamtangaza Kikwete kuwa Rais licha ya kwamba matokeo majimboni yalikuwa yanaashiria vinginevyo.
Ni muhimu kutambua kuwa ni rahisi kukubali matokeo ya Ubunge kwa sababu yanarasimishwa majimboni na yanaweza kupingwa mahakamani. Katika urais kimsingi ukiangalia Katiba utaona kuwa haijalishi nani kashinda kwenye kura, bali nani katangazwa mshindi. Tunachotuhumu sisi ni kuwa matokeo ya Uchaguzi yangetangazwa kama ilivyoahidiwa na Tume mwezi Machi yangeonesha wazi mshindi ni tofauti na yule aliyetangazwa. Lakini wao tume wakijua kuwa mara wakishatangaza hakuna mahakama inayoweza kuhoji wakafanya hila na haraka ya kutangaza matokeo ya Urais kwa kumtangaza Kikwete kuwa ni Rais.
Kama toka siku ya kwanza tulitoa malalamiko na zikapita siku tano bila kujibiwa wala kusikilizwa na baadaye tunatakiwa tukubali tu kwa vile "keshatangazwa" katika dhamira safi tunaweza vipi kufanya hivyo? Ugomvi wetu wa kisiasa (na siyo chuki wala uhasama binafsi) hauko zaidi na Kikwete bali natume iliyomtangaza. Na kwa vile yeye mwenyewe haoni matatizo katika tume au mfumo wetu wa uchaguzi tunaona kuwa aidha alitoa baraka zake au alikubali kunufaishwa na mfumo huo mbovu.
Hivyo, wabunge wetu kutoka nje ni kutuma ishara mbili: Kwanza, tunapinga mfumo wa kichakachuaji wa tume ya Uchaguzi uliomtangaza Kikwete kuwa Rais, na pili kwa vile Tume imeshindwa kutuonesha uwazi wa ushindi wa Kikwete tunashindwa kukubali kama ni mshindi halali. Ni mpaka pale uchunguzi huru wa kura utakapoonesha kuwa Kikwete kashinda kihalali ndipo tutakuwa tayari kumtambua ukiondoa uwezekano mwingine wa kuelewana.
Tukumbuke kuwa, kama uchaguzi huu ungeendeshwa katika hali ya uwazi, haki na ufanisi tusingefika hapa. CHADEMA siyo wa kulaumiwa katika hili wala wabunge wetu wasibebeshwe mzigo kwa hili; watu waliotufikisha hapa ni Serikali ya CCM na vyombo vyake ikiwemo Tume ya Uchaguzi. Wangeonesha weledi na kutokupendelea kwa wazi tusingefikia mahali pa kutulazimisha kuchukua hatua hizi ambazo kwa kila kipimo ni za wastani sana ukilinganisha na hatua ambazo tungeweza kuzichukua.
Nawasihi tuwaunge mkono wabunge wetu na uongozi wetu kwa kuwatia moyo kwani uamuzi waliouchukua ni uamuzi wa kijasiri lakini ulioweka historia katika Tanzania kuwa hatuwezi tena kusukumwa na kuburuzwa kwa kutumia nguvu ya taasisi au cheo cha mtu. Tuwatie shime na tusimame nao katika wakati huu wa kihistoria.
Pamoja tunaweza, mpaka kieleweke!
Kuna mdau amesema Michuzi anachakachua comments na kuonesha zenye mwelekeo fulani. Nina mawazo kama hayo.
ReplyDeleteHaya mambo CUF walipoyafanya ilionekana sawa tu. Leo Chadema wakiyafanya inaonekana ni tatizo. Suala la Chadema sio kusema kwamba hawakubali kushindwa, wanachotaka ni kushindwa kwa haki. Kama Kikwete amepata ushindi wa asilimia 41 dhidi ya 40 za Slaa basi na iwe hivyo. Kama mbunge wa CCM ameshinda kwa kura 2 basi na iwe hivyo.
Methali ya asiyekubali kushindwa si mshindani haipaswi kutumika hapa. Methali hiyo hutumika pale mnaposhindana katika mazingira yasiyo na upendeleo.
Chadema wanalalamikia NEC kutoa matokeo yanayoipendelea CCM. CCM wanaona NEC inafanya kazi safi. NEC kuna kosa angalau moja wamekubali kulifanya huko Geita. Ukifikiria kidogo inaonekana kama makosa yanayofanywa ni ya makusudi. Kama ni makosa ya bahati mbaya yangekuwa yanakula huku na huku, mbele na nyuma.
HEEE NDUGU ZANGU MSIOELEWA: CHADEMA WAMETOKA KATIKA HOTUBA YA RAIS TU NA SIO KUSUSIA BUNGE. WATAENDELEA NA VIKAO KAMA KAWAIDA, WATANZANIA WENGI BADO HAMELEWI PROTOCAL ZA KISIASA KWAHIYO NI HELI MKAE KIMYA. CHADEMA HOPE YOU TEACH YOUR PEOPLE AND LOTS OF WADANG"ANYIKA KWAMBA KUWALK OUT IS FULL DEMOCRASIA NA SIO KUWAACHA WANANCHI. NI KUONYESHA KUWA HAMKUBALIANI NA MAMBO YANAVYOENDA NCHINI!!! KI AMANI BADALA YA VITA. MNAONYESHA NI JINSI GANI MMEKAKAMAA KISIASA. KEEP IT UP, WORK HARD WORK HARD CHADEMA, WANANCHI TUSIODANGANYIKA TUKO NYUMA YENU NA NI VIZURI KUWAELIMISHA WADANG"NYIKA PIA.
ReplyDeleteThat is democracy ... They have a right to walk out.
ReplyDeleteI don't think so. The walk-out was a very classless act and prank on the part of CHADEMA's MPs.
Simply because there are many other ways in which they could have registered their discord, disgust, opposition, displeasure or whatever cheap political point they wanted to score.
Unfortunately, this was not the place and time for their brand of politics.
I guess the citizenry will now begin to see them for who they really are in terms of their true colours.
FYI, even the Republican Party (in the USA) and it's far right wing politicians who so much hate President Obama due to his paternal African (black) ancestry, didn't walk out on him when he first addressed law makers (senators and congressmen) on Capital Hall.
CHADEMA should start learning one of the first lessons in multi-party politics, which is, politics is a game of loosing today and winning tomorrow (if the get majority votes), learning from past mistakes and doing better in the next elections, give and take, and being ready to compromise on matters that concern the common good as well as the greater good of the nation at large.
Such juvenile political antics, pranks and tantrums will not get them far nor win them any national appeal that they are so desperately after.
Politicians come and go, and they will continue to do so in every election cycle.
However the nation of Tanzania is far more important than a single (particular) party, single individual, or oen group of inviduals with a warped sense of political entitlement.
What sort of example are they setting for the rest of the nation and future generation of politicians?
They will never win the hearts and minds of Tanzanians if they want to change political voting patterns, and above all, the hearts and minds of the ever watchful Watanzania.
I wonder what became of statesmanship? Let alone remaining graceful after one has been dealt a severe political defeat at the polls?
Inaonyesha ulimbukeni wenu!! Hawa ndio walitaka tuwape nchi ??? Leo wanajiona wao ni bora kuliko vyama vingine vya upinzani....Hata mkitoka, hampunguzi kitu, mnaonyesha ni watu wenye jazba, msiokubali kushindwa, na msiotambua demokrasia...Mshindwe na njama zetu za kutaka kuleta vurugu!!! Hatudanganyiki
ReplyDeleteKama ni kweli chadema wanafikiri wameshinda kwa kutumia idadi ya wakristo kama alivyodokeza mchangiaji. Basi imekula kwao.
ReplyDeleteAccording to CIA world facts book:
Religions:
mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim
https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html
KWANINI UDINI UMEZIDI KIPINDI HICHI CHADEMA WANAOGOZA UPINZANI ?????
kweli shule muhimu,bunch of ignorant katika blog hii,nendeni shule,hiyo ndiyo demokrasia ya kweli walionyesha chadema,na mtaaibiwa sana na hao mafisadi wa ccm,nyambafu wakubwa nyie,watu wenyewe mnashindia mlo mmoja,!
ReplyDeleteSafi sana CHADEMA , mwendo ni huohuo mpaka kieleweke, maana mwamba ngoma huvutia kwake... ccm MTAJIBEBA
ReplyDeleteUNAKUBALI KUAPA KWA KATIBA ILIYOMWEKA MADARAKANI UNAYEMSUSIA JE HIYO AKILI AU MATOPE?
ReplyDeleteHAWA NI NJAA TU, WALIONA WAKISUSIA BUNGE KWA UJUMLA WANGEKOSA MISHAHARA NA RUZUKU.
Majority ya mliochangia hapa hamjui siasa, ni mashabiki tu na tukiwaweka bungeni hamtajua hata mfanye nini. Dhuluma ya nchi hii lazima isemewe. CHADEMA hawasemi Kikwete asingeshinda hila wanasema kila kitu kingefanywa kihalali asingepata 61% angepata less. Mnajua effect yake? Ya kwanza rahisi kabisa ni viti maalumu ambavyo hugaiwa kutokana na kura za urais na ubunge. Huoni kwamba CHADEMA wangepata zaidi ya viti walivyonavyo? Kuna mambo mengine mengi ambayo walioenda shule wanasema yo must be able to think outside the box or see the other side of the coin to understand. Msipende kuangalia tu plain na kufikia conclusion. Demokrasis haikuzwi na CCM hata siku moja. CCM wangependa wakae madarakani milele. TAFAKARI CHUKUA HATUA!! ndicho walichofanya CHADEMA.
ReplyDeleteNawakilisha - MCHAMBUZI WA SIASA ASIYE NA CHAMA
Tatizo la watanzania ni wajinga wengi na hawajui lolote si mkae na wanasheria muulize kama chadema imefanya vibaya kutoka hiyo ndio demokrasia mnaosha tu vinywa kwa uvivu wenu wa kusoma we realy need to work up tuko nyuma kwa ujinga mno someni sheria mjue ukweli chadema wanadai haki itendeke kidemokrasia na hakuna damu itakayomwagika hapa
ReplyDeleteIn this world of sin and sorrow there is always something to be thankful for; as for me, I rejoice that I am not CHADEMA
ReplyDelete......Hivi yale matokeo ya kusubiria kwa mawe na kuziba njia kwa siku zaidi ya tatu ndipo yatangazwe, watu wanategemea uwe ndio mtindo wa kudai haki? hivi utawezaje kuwajulisha wenye akili zao kuwa kuna tatizo mahali? watu waingiao kwenye blog (waliofuta ujinga)wanaweza kuwa na uwezo mdogo namna hii wa kutokuelewa? au kuna mkono wa mtu? amaziiing!!!
ReplyDeletehongera chadema kwa kweli tumechoka sasa tunahutaji mabadiliko kidogo maana watu ni haohao tangu uhuru na watu wanakufa njaa hakuna maendeleo yoyote ya jamii nafikiri mseto unaweza kuleta changamoto kuinua watu waliojisahau na kazi zao za kuihudumia jamii
ReplyDeleteCHADEMA bwana mmeamua kujitangaza (kutafuta umaarufu) kwa njia isiyo, jaribu kifikiria tena. Rais Dr. Kikwete hamtambui lakini serikali inayoongozwa na yeye kama Rais mnaitambua!!!
ReplyDeleteWHOSE INTERESTS ARE THEY LOOKING OUT FOR? Chadema hawaendi bungeni kumsikiliza Kikwete bali wanakwenda kuwawakilisha wananchi kwenye serikali yao. Matakwa ya wananchi lazima yazingatiwe hivyo kura lazima zihesabiwe kwa uwazi tusitumie njia ya kuwekana madarakani kwa kuweka sheria inayozuia matokeo ya uraisi kupingwa mahakamani, mbona nchi nyingine za kiafrika wanaruhusu kwenda mahakamani? JK alilishukuru jeshi kwa kazi nzuri liliolofanya lakini hakutoa shukurani kwa polisi sasa tujiulize ni kazi gani nzuri? Wel done Chadema hata mimi sipendi kupigishwa kura ambayo mwisho wa siku haitahesabiwa.
ReplyDeleteCHADEMA wana protest kwa amani, je mngefurahi wangeingia msituni na kuanzisha vurugu? Wala CHADEMA hawakuwahikusema
ReplyDeleteHili ni suala la kuwa na PRINCIPAL iliyosimama na isiyopinda panda kufuata upepo. Eti, kwa sababu tu fulani ameshatangazwa kuwa Raisi basi kila mmoja asiwe na haki ya kuhoji!!
ReplyDeleteCHADEMA wanaamini na wanao ushahidi unaonyesha kuwa kura za mgombea wao “zilichangachuliwa”...sasa nyie mnaowapinga mlitaka wakubali tu..ili iwe nini?
Hiyo ingekuwa nidhamu ya woga na Wananchi wengi wanaotegemea CHADEMA isimame kwenye ukweli na haki wangekidharau chama.
Siasa ina risk zake na hii ni mojawapo ya hizo.
Nasita kuamini Wasomi wetu humu mnasema CHADEMA wasingegoma, sababu; wametumwa kuwawakilisha Wananchi!!! hao wananchi wakati sasa umefika waelewe kuwa HAKI kwenye hizi CHAGUZI ni lazima zitafutwe kwa njia nyingine. CHADEMA wanaonyesha ni dhahiri njia ya sanduku la kura inasimamiwa vibaya au inakipa kipaumbele Chama fulani.
Haya ni mapambano ya fikra, hoja za kuunga kuunga mkono na kupinga zote zina mantiki. Cha msingi hapa na ambacho binafsi nawapongeza Chadema ni kule kuonyesha MSIMAMO.
Hakuna shaka kabisa kwa kitendo hiki Wananchi waliowachagua Chadema watakuwa wameelewa ni wapi CHADEMA imesimama; HAWAKUBALIANA NA MATOKEO YA URAISI (it's that simple).
Nidhamu ya WOGA na iwe MWIKO huko tuendako, kama unapinga tumia HAKI YAKO KIKATIBA kusimama na kusema NAPINGA...SIO, NAPINGA LAKINI...Namtambua Raisi!!!
Soames Phares,
Dar es salaam.
hao chadema ni wa2 wasiofaa kabisa,yaani wanalazimisha ushind,kila mtu anajua kuwa walishindwa uchaguz na kila mwananchi anajua JK alikuwa anashinda tu,sasa wakimkataa rais wetu wakatae na kura za wabunge wao pia.tofaut ya kura ni zaid ya million3 eti umeibiwa?
ReplyDeletemdau wa tbc
Kweli siasa ya chama kimoja imeshika hatamu, sasa watu wanawalaumu CHADEMA wa nini? Ina maana ndio mara yenu ya kwanza kuona wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa bunge wasipokubaliana na kitu? Kweli maji ya kijani tuliyokunywa hata kutapika haiwezekani tena!
ReplyDeleteUnayejutia kura yako kwa kuipa CHADEMA, nenda NEC kaichukue, mbona inawezekana! Tena watatangaza upya na matokeo.
ReplyDeleteHizo ni jazba za kitoto na chuki za kijinga tu. Chadema tumieni akili na busara na si hemko za kichuki.
ReplyDeleteNakubaliana kabisa na mdau aliyesema kitendo hicho cha kijinga cha chadema hakitakuwa na impact ng'oooo!!!!!
ReplyDeleteSikio la kufa halisikii dawa. This is the beginning of the end of kyadema. Eben-E. Kunduchi, DSM.
ReplyDeleteKweli chadema hawako siriaz. Meku wa CCM.
ReplyDeleteTatizo la watanzania ni uelewa wao mfinyu, na hawafuatilii mambo, watu wanaochangia mada nyingi na hasa hizi za wabunge wa chadema kutoka bungeni hawana taarifa kamili na hawapendi kujishughurisha kujua habari wala si wafuatiliaji, suala hapa si urais wa JK, suala ni jinsi alivyofika kwenye urais system iliyotumika kumpa urais sasa ukisoma hata hapa michuzi utaona watu hawaelewi halafu wanataka kuchangia ukisoma tu michango yao unaona kuwa wanachangia kitu ambacho hawakijui, hawakijui tu kwa vile ni wavivu wa kutafuta habari. Narudia hasa vijana tena wameenda shule vizuri tuu ni wavivu wa kufuatilia habari kucha kutwa muziki/dili halafu unataka kujadili jambo huwezi majadiliano yako yatakuwa na mwelekeo negative na hutaeleweka!
ReplyDeleteThe Minister of Science & Technology 2015
wahenga wamesema 'usikatae mwito, kataa maneno'. hawa chadema wanaanzisha siasa za chuki ambazo hawataweza kuzidhibiti.
ReplyDeleteUSITUPE JAMVI LAKO KWA GODORO LA MWENZIO, SIASA ZA ZANZIBAR NI TOFAUTI KABISA NA SIASA ZA TANGANYIKA , CUF KWA ZANZIBAR NI NUSU KWA NUSU NA CCM HIVYO ZANZIBAR HAITAWALIKI BILA SERIKALI YA PAMOJA, KWA TANGANYIKA CCM NI WENGIM NA WANAWEZA KUENDESHA SERIKALI BILA KUMSHIRIKISHA MTU, MIFANO MMEIONA KWENYE KURA ZA USPIKA, UNAIBU SPIKA, KUMPITISHA WAZIRI MKUU, NA HIVYO NDIVYO ITAKAVYOKUWA KATIKA MASUALA MENGINE YOOOTE YATAKAYOINGIA BUNGENI, KWA HIYO KUTOKA NA KUSUSIA HOTUBA YA RAIS HAKUWASAIDII WAO KAMA WABUNGE NA WANANCHI KAMA WALIOWAFIKISHA BUNGENI, BUSARA ITAWALE KULIKO JAZBA, MHE. JAKAYA KIKWETE ATAENDELEA KUWA RAIS NA MHIMILI WA PILI WA BUNGE BILA KUTAMBULIWA NA CHADEMA AU TAASISI NYINGINE YEYOTE IWAYO
ReplyDeletewoote nyie ambao mnasema kwamba they are mnamatatizo..that is one of the things that is lawful to try and prove a point lkn bcoz wabongo matatizo kichwani evryone is saying eti cause they lost..hivi,logically,mtu huwezi kujiuliza certain questions ambazo no one has an answer?!..alafu why did watu wa CUF wakaenda kukaa their seats,what does that imply in the back of ur minds?so much for democracy!!people need to open their eyes and start listening closely sio kupuuzia tu
ReplyDeleteYaani sijaona watu wapumbavu kama hawa! Wao kama wamekubali kuwa wawakilishi wa watu aatika majimbo yao, iweje sasa mnasusa? Hivi wanamsusia nani na kwa faida ya nani? Upuuzi mtupu!! Upinzani haujengeki kwa kususa bali kwa hoja na sera thabiti. Watu wazima ovyo!!! Sasa endeleeni kususa tuone mwisho wake nani atakuwa wa maana.
ReplyDeleteKususa kunamsaidiaje mwananchi wa kawaida kijijini ambaye anataka kusikia na kuona matatizo yake yakitatuliwa hususan, shida ya maji, elimu, afya, usafiri na maisha bora n.k.? Acheni hizo, kubalini yaishe kwani kushindwa ni kushindwa tu hata mkisusa. Haya waswahili wanasema "Mkisusa siye twala." Kalaga baho!!!
michuzi tumekustukia!!
ReplyDeletehuwezi amini, sangara aliyeitafuna sisiemu sasa muda mfupi attanza kazi tena sasa hivi vijijini na kwenye ngome zao!!! CHADEMA OYEEEE!!
alafu wengine waliobaki when others are going out eti they are booing..heh!thts a parliament jamani,ai!yani,Tanzania its not wat is good for the country,mtu anafikiria wat is good for me,ndio maana hatuendelei,..we need change kwa kweli,inauma sana
ReplyDeleteNdugu zangu, wabunge wa Chadema kutoka nje bila vurugu ni ustaarabu wa kutosha. Mabunge ya NDIYO MZEE hayapo duniani, tena wanachapana Bungeni. Angalieni walioendelea wanachapana ngumi bungeni - UKRAINE, URUSI, MEXICO, NIGERIA, ALABAMA SENATE, INDIA, UK, KOREA KUSINI, ETC...... Siyo kwamba nahalalisha watu kupigana. Lakini Nafikiri CHADEMA ni wastaarabu kuliko mnavowafikiria. Tuache unafiki wa kivyama.
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=cD0XZlxKuig&feature=related
http://www.youtube.com/watch?v=mZGaaqH2o6I&feature=related
http://www.youtube.com/watch?v=vlXKBribICs&feature=related
http://www.youtube.com/watch?v=TsAa9VmwOaI
http://www.youtube.com/watch?v=5Pqhnf6XKC8
Hii ndio democracy ya kweli, hawamtambui rais, sasa kwann wasitoke? wanamuonyesha kivitendo kuwa hawamtambui... Keep it up guys!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMmmmh mimi mwenzenu nikiliona jitu linajiita mfuasi wa Chadema namuona kama hajavaa nguo vile
ReplyDeleteMCHAKACHUAJI
Mungu si athumani. Anaona yote yaliyo mioyoni mwa wanadamu. Wezi, Waongo, Wanafiki wanaweza kujificha popote wanapopenda.
ReplyDeleteMatusi, fitina, Majungu, Kebei, Dharau zitasemwa lakini siku ya mwisho nafsi zetu zitahukumiwa mbele ya Mungu.
Busara ni kuuliza kwanini tumefikia sehemu watu wenye akili timamu waliochaguliwa watoke Bungeni?
Busara ni kuuliza kwanini watu waliokulia ndani ya CCM watoke na kuanzisha vyama vyingine kama CCM kweli ni chama safi na kitakatifu?
Busara ni kuuliza kwanini kuwe na asilimia au sehemu ya jamii ichukie kabisa chama fulani au watu fulani na kuwaita majina kama mafisadi?
Mimi binafsi ningalipenda sana kuwe na chama kimoja, kurahisisha utendaji wa shughuli za wananchi na maendeleo ya taifa. Lakini nyakati zimetuleta hapa kwenye vyama vingi.
Kipimo cha demokrasia yetu itakuwa utoaji fursa sawa na haki sawa. Na usawa maana yake kukubali kuwajibishwa au kuchukua hatua za kuwajibika pasipo kulazimishwa.
Ukweli utajulikana katika historia.
Tuwe makini kulinda heshima ya taifa letu, sio kwa kuficha ukweli unaotuumiza tulio madarakani, bali kwa kujisahihisha!
CHADEMA. CCM. CUF. NCCR. TLP. APPT. UDP. Kueni katika hofu ya Mungu. Fanyeni kazi kwa kumuogopa Mungu. Mwisho wa siku wote ni wanadamu. Tutakufa na kuzikwa.
wabongo bwana. Nimeangalia hizi comments na analsisy yaonyesha fourty percent hawana uelewa wa mambo. Kwanza wanabisha na kulalamikia chadema bila kuwa na hoja. Wabongo tuna tabia ya kurukia mada tu na kuandikaa bila hata kuwa na evidence. Mi naona watu wangekuwa wakitoa comment kwa kurefer vipengele vya katiba/vitabu na hata research zilizopita hapo ndo tungejifunza na kupata ufahamu. Lakini kwa kuwa si tabia ya wabongo kutafuta details kabla ya kucomment basi ni blah blah bla bh blah blah zinazoendelea humu. Badilikeni.
ReplyDeleteMdau anaependa maendeleo ya kweli na sio ubabishaji unaoendelea.
Waache unafiki na nyie wanafiki mnasojidai sijui vipengele vya katiba sijui nini kwani katiba inasemaje tume ikashamtangaza rais? Mnaleta ujuvi wakati ni njaa tupu. Serikali iliyoko madarakani ni serikali halali, pelekeni upuuzi wenu huko hamna cha nini wala nini ni udini tu ndio unawawasha na kuwasumbua. Ishatoka hiyoo mlituimbia mapambio wee wakati wa kampeni sijui sauti ya watu sauti ya mungu, sasa hamuamini kuwa sauti ya watu imeongea kwa kumchagua JK? Kwa mtaji huu subirini kura 5% mwaka 2015. Na hivyo mmeonyeshwa live kwenye luninga ndio kabisaa watu watawakacha sasa, huyo alowashauri alikwishaua vyama vingine huko nyuma kwa hiyo hesabuni kuwa HIYO IMEKULA KWENU.
ReplyDeleteKweli kazi ipo. Kama huyu mdau wa Tarehe Fri Nov 19, 07:27:00 PM, anaonyesha kabisa ni Mtanzania hasilia.
ReplyDeletemwenzenu sielewi. yaani chadema wanakubali wameshindwa ila hawakubali marks? kwani inaingia akilini chama kimepata majimbo 25 na wenzao zaidi ya 270 kingeshinda? au assumption ni kwamba wale waliochagua wabunge majimbo 270 walichagua wabunge ccm na raisi slaa?!
ReplyDeletendugu zangu chadema ni chama cha watu wa jazba. hivi mshawaona hata wanavyozungumza jukwaani?
mi nadhani wale wote wanaosupport chadema ni watu frustrated na very bitter.
ingine. wanatula
tatizo watu walishajiandaa kuingia ikulu. wakasome theory za kuwa na higher expectations kwenye chochote results frustration kama hakikutimia ulichotaka.
hatuwasupport hata kidogo. watafute njia nyingine. wanatulazimisha tupiganie mabadiliko ya katiba, mi mwenyewe hapa sijui katiba yenyewe na nini kibadilishwe. wangeanza kutueleza na kutufundisha katiba yenyewe