Mkurugenzi mkuu wa TBL,Robin Goetzsche akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza kucheki afya yake ikiwa ni siku ya wakuu wa makampuni binafsi kucheki afya zao iliyoadhimishwa katika nchi tano za Afrika Mashariki leo.shughuli hii imefanyika leo hii katika viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB,Dr. Charles Kimei nae alipata wasaha wa kuongea na vyombo vya habari huku akihiza na kuwahamashisha watu mbali mbali kwenda kucheki afya zao mara kwa mara.
Mkurugenzi wa Shirika la ABCT ambalo linajihusisha na mapambano ya Ukimwi makazini hasa kwa Wakuu wa Makampuni,Richard Kasesela akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kongamano lililowakutanisha Wakuu wa Makampuni mbali mbali nchini na kuhamasishwa kupima afya zao,katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar leo.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Charted,Jeremy Awori akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Karimjee katika siku ya Wakuu wa Makampuni kucheki afya zao,iliyofanyika leo katika viwanja vya Karimjee.
Meneja Mkuu wa Konyagi,David Mgwassa akiwa tayari tayari kwa kupimwa afya yake na Dr. Peace Kayoza kutoka Maria Stopers.
Mkurugenzi wa TBL,Robin Goetzsche akichukuliwa damu yake katika chombo cha kisasa kabisa na Dr. Peace Kayoza tayari kwa kucheki afya yake leo ikiwa ni siku ya Wakuu wa Makampuni kucheki afya zao.
Mkurugenzi Mkuu wa CRDB,Dr. Charles Kimei akichukuliwa damu yake tayari kwa kucheki afya yake.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Charted,Jeremy Awori nae akichukuliwa vipimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kupima si kazi. Kufuata majibu bwana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
    rafiki yangu alipima bila shida lakini ilipofika kuchukua majibu mbona ilikuwa ni timbwili. Alifika hadi mlango wa ofisi ya majibu, lakini akatimuka mbio kurejea nyumbani bila hata kuingia. Ninawapongeza kwa kuhamasisha upimaji. Hakuna silaha ya mapambano dhidi ya ukimwi inayozidi mtu kujua hali yake na kufanya ngono salama.

    ReplyDelete
  2. jee kuna walioonekana Positive?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...