hawa madereva wa daladala sijui wana aleji na foleni za barabarani??maana huwaga hawataki kabisa kuwa katika foleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. hiyo kazi ya usalama,nadhani wapewe majembe kazi auction kusimamamia.polisi wetu njaa sana kama asubuhi alihongwa ya chai sidhani kama anaweza kumkamata daladala hiyo tena.Sumatra vyazo vingine vya mapato vipo nyingi kwa madereva kama hawa.

    ReplyDelete
  2. aleji??? ndio nini sasa sijakuelewa

    ReplyDelete
  3. Hao Madereva wa daladala wametumwa pesa na wanatakiwa kupeleka hesabu kwa boss . na Boss haelewi cha foleni yeye hesabu yake ipo Constant . Ndio maana madereva hao wanaona wanahaki ya kutanua barabara nzima(Yaani barabara ni yao) Pili wanajua wakikamatwa na Traffic. Issue ni simple kumpa Traffic pesa ya chai(rushwa) biashara imekwisha maisha yanaendelea. Rushwa ni tatizo linalovuruga kila kitu kilichopanga =mfano pale Ubungo daraja daladala zinapark mstari mmoja mpaka darajani na traffic wanaona hawachukui hatua. Siku litazuka balaa pale Lipite Lorry ikusanye daladala zote darajani pale kisa uzembe wa kupark darajani na kuna parking nzuri na maalumu chini pale. sielewi ni kwa nini wanaachwa kufanya vile; RUSHWA RUSHWA Mbaya sana

    ReplyDelete
  4. Tatizo ni mfumo wa barabara zetu unafikiri kungelikuwa na barabara za mabasi pekee (bus lanes). Nafikiri serikali badala ya kufikiria kujenga flyovers wangeliteneza barabara za daladala ili kuwezesha wanaopanda mabasi nao wawahi kazini. Sidhani kama ungeliona takataka hii wacha watanue tu

    ReplyDelete
  5. Fly overs zinakuja - stay tuned.

    ReplyDelete
  6. Picha hii ni ushahidi tosha kwa mamlaka husika kuchukua hatua kwa gari husika lakini hii ni nchi ya "kitu kidogo" hivyo hakuna kitakachofanyika!

    ReplyDelete
  7. namuunga mkono annoy wa hapo juu kusema kuwa ni haki ya daladala kutanua, fikiria mwenyewe basi limebeba watu 60, wengine wamesimama wengine wagonjwa na wengine wana watoto wadogo, huoni kwamba jinsi basi linavyokaa foleni muda mrefu binadamu hawa wanaumia? tofauti na wewe uliye katika gari dogo unakula kipupwe na girl friend wako ndani ya vogue kwenye foleni? ufumbuzi wa tatizo la mabasi kutanua ni kuwa na bus lanes kama ilivyo katika nchi zingine....daladala" kutanua" ruksa !!!!!

    ReplyDelete
  8. TAnzania TAMBARAREEEEEE....

    ReplyDelete
  9. Wewe mdau wa Sat 07:23:00 AM kwani sisi tunaoendesha gari na tukakaa kwenye foleni kwa muda wa masaa mawili na zaidi huwa hatuumii?

    Usilete masababu yasiyokuwa na msingi ya kuvunja sheria kwa hao madereva wa daladala. Afadhali hata ungesema mabasi ya shule ningekuelewa.

    Wengine tukifika ofisini miguu imevimba kwa kukanyaga breki kila baada ya sekunde tano!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...