jiji la Dar leo. hesabu vikwangua anga vipya vinavyochomoza,
na barabara zilizopo kukidhi matakwa
mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
Jamani jiji la Dar ni la kijani


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mbona umepiga upande wa Gymkhana na ocean road tu? piga kuanzia Mnazi mmoja kuelekea Kariakoo uone ukijani wake!

    ReplyDelete
  2. Unachagua sehemu ya kupiga? Onyesha vingunguti, manzese, jangwani, shomo la udongo nk

    ReplyDelete
  3. Unasema kariakoo mbona bado uzunguni? Kwanini asianzie Mwananyamala anakoishi Dr Michuzi kabla ya kupiga Tandale Uzuri na Buguruni kwa Malapa? Hata usifu vipi hii nchi imeharibiwa na Dr Dr Kikwete na mafisadi wenzake

    ReplyDelete
  4. Bongo ni jiji zuri sana na linapendeza ila sema litakiwa kufanyiwa ukarabati majumba yake yote ya mjini, yapigwe rangi upya tu na kutiwa mataa ya njiani vizuri litakua jiji poa katika east africa.

    ReplyDelete
  5. Mweee kamji ketu kanatia aibu ..Kwanini tusianzishe mji mwingine mbali na hapo. Tujenge mji mwingine wa kisasa bwana..Huo hata haueleweki wala haufai kukarabati. Nyumba zimebanana ukitaka kupanua uweke subways, highways huwezi kabisa....

    Tuanzishe mji mwingine bwana ardhi tunayo nyingi hapo tuyaache majumba ya baki na history zao..

    ReplyDelete
  6. MICHUZI, UNAZUNGUMZIA UKIJANI GANI? UKILINGANISHA NA NIGER NI KWELI NI KIJANI LAKINI SI NA SEHEMU NYINGINE DUNIANI.KUNA BARABARA ZIPI HAPO? JE UNAONGELEA HIZO CHACHE ZILIZOPINDA PINDA NA ZINAZOTOA VUMBI NA KUJAA MCHANGA.
    TUNAHITAJI BARABARA NZURI, TANZANIA JUMLA TUNA KILOMITA ZA BARABARA ZA LAMI 4700, UKILINGANISHA NA KENYA BADO TUPO NYUMA SANA, KENYA WANA LAMI KILOMETA 12,000 NA UGANDA KILOMETA 16,000. HIVYO HAKUNA CHA KUJIVUNIA ZAIDI YA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KUACHA UVIVU NA KUKAA VIJIWENI PAMOJA NA KUISHINIKIZA SERIKALI ITIMIZE WAJIBU WAKE.

    ReplyDelete
  7. Ukitaka kuufaidi huu mji chukua Google Earth 6 pro...utashangaa na roho yako...haifichi, haidanganyi ...don't go with the std version chukua pro unangalie kwenye screen ya 1280 by 1024

    home sweet home lakini ukweli ni kuwa hamna mpangilio ukilinganisha na majiji mengine...wee tanzama mwenyewe utajionea..

    ReplyDelete
  8. Si la kijani hapo Ocean Road na Gymkhana ndio dar es Salaam?na kule uswahilini je?nadhani pamoja na flyover za JK patakuwa pa kahawia kama si manjano.
    Pamoja tutafika.

    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  9. Unavizia mvua zimenyesha??

    Gymkana wakati wa nyuma pako kama jangwani, wakati viwanja kama hivyo kwenye dunia iliyostaarabika ni kijani kibichi mwaka mzima!! Na kuhusu usafi, ni ajabu kukuta plastic bags hata Gymkana!! Beach ndio usiseme kabisa.

    Kwa ufupi, sisi wakazi wa Dar na wachafu kupindukia!! Full stop!!

    Halafu siku hizi barabara za Dar zinakatwa katwa, sijui tunarudi wapi?? Ustaarabu wa njia za lami sio sawa na kutembea kwa mguu. Kwamba nikiamua kukata kona upande huu hamna shida kwa mguu. Sasa hiyo ndiyo inaingizwa barabarani, hivi punde itakuwa ni vurugu tupu mjini, ikizingatiwa maghorofa yanavyoongezeka kwa kasi na kuongeza wakazi wengi.

    Mabadiliko ya ghafla Dar roads nimeyaona pale "Pijoti" house, makutano ya Zanaki na Bibi Titi, na Jamhuri na Azikiwe.

    Planners wa awali walikuwa na maana yao kujenga vile barabara, sasa ujinga wetu na haraka sijui ya kuelekea wapi tunaanza kuzidi kuharibu mji.

    Idumu Tanzania!!

    ReplyDelete
  10. Dar kwa mbali bomba ila mvua inyeshe kidogo tu, mavi yote uhindini yanatapakaa kila kona jijini. Very sad, na huko uswahilini kwa kina Michuzi ndo usiseme. Yaani hili jiji lione kwa macho tu ni la kihovyo mno.

    ReplyDelete
  11. wacheni jealous wabongo jamani hata huku ulaya kwenyewe wakionyesha miji yao hawaweki sehemu chovu, hebu kwa waliopo holland naombeni mseme lini wadachi waliionyesha amsterdam wakapaweka picha ya balmer kule kwenye uozo? nynyi watu wa marekani new york hivi yote iko kama manhattan? vipi queens, vp bronx na harlem? wacheni hizo huu ushamba wenu umepitwa na wakati. jifunzeni kupenda vya kwenu

    ReplyDelete
  12. Ukisoma komments za Wabongo hapa ndo utajua kwamba kamwe hatuwezi kuendelea! Always Negative! Kila kitu..mara Jirani kala nyama sisi dagaa, mara mtani ana khanga mpya! ..na ni ndiyo wasomi wetu hao!

    ReplyDelete
  13. wote hamjagundua ankali alikuwa na intention gani? View kama hiyo ni kawaida kabisa kama utakuwa unatoka JNIA ukikata mawingu kuzitafuta dunia nyingine(sio lazima Nje).Usiombe uwe unatua usiku ndugu zangu,utaliona jiji si ndo hili,mitaa imejipanga vizuuri kabsia kumbe wapi bana,hamna kitu!

    ReplyDelete
  14. Ukiona plan ya mji wa Roma kwenye karne ya 3 AD huwezi kulinganisha na huu mji. Tatizo letu ni Mipango miji imekufa kabisa na sio swala la vikaanga jua. Matatizo mengi ya kwetu ni ya kujitakia na yanatokana na ukosefu wa mipango miji bora. Magonjwa kama kipindupindu, malaria, TB, n.k yanakuwa magumu kutokana na vurugu iliyopo. Sijui na hili tunahitaji wafadhili.....lakini kama hata katika level ya juu Mkullo anakuwa msanii kwa kutengeneza bajeti mbili du hata hao wahisani wameshatuchoka.

    ReplyDelete
  15. jay hapo juu umesema kweli, hapo dar mvua inyeshe nusu saa mfululizo tu hapo ndio utalijua jiji,nimafuriko kila sehemu, foleni,maji machafu ya chooni ndio wajanja wanayafungulia barabarani, umeme unakatika, mabasi hayapandiki,watu na suti zao wanabebwa kwenye mikokoteni utadhani mizigo we acha tu!!!!!

    ReplyDelete
  16. WOW TANZANIA WE GOT BIG CITY WITHOUT ROADS, SIONI BARABARA MIE ATI, HAO WAISHIO NA KUFANYA KAZI HAPO WAPITISHA WAPI MATOKARI???? AU WATEMEBEA KWA KUKATISHA NYUMA YA NYUMBA ZA WATU???
    VIONGOZI TUNAITAJI INFRASTRUCTURE AND MAPS. TUJENGE KWA MPANGO HATA RADAR ZIKIPITA JUU MITAA IONEKANE NA BARABARA NA SIYO MAJENGO MAFUPI NA MAREFU BILA NJIA. WATANZANIA TUACHE KUJISIFU SANA NDIYO MAANA VIONGOZI WETU HAWAFANYI KAZI, MNAPOSEMA JIJI LIMEJENGEKA BASI LIONEKANE KWA KILA KITU NA SIYO MAJENGO TUU TENA YANAYOJENGWA KWA PESA ZA WIZI, HAO WATU HAWAFIKIRII WATAPTISHA WAPI MAGARI NA UTALII UTAIMARIKA VIPI AU MAMBO YA NDEGE, ZENYEWE ZITAPITAJE MAJENGO HAYANA RAMANI ???GROW UP TANZANIA NA JENGA JIJI LENYE KUONEKANA, REMEMBER I WANT TO USE MY GPS WHEN I GOT THERE, OK....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...