Mtangazaji wa siku nyingi wa redio na TV
Jimmy Kabwe anachukua nafasi ya Afisa Masoko wa TFF.
Mwandishi mkongwe Angetile Osiah amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka (TFF) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Frederick Mwakalebela ambaye muda wake uliisha. Angetile, maarufu kama 'Ngeta' anaingia TFF akiwa na uzoefu wa siku nyingi katika medani ya soka baada ya kwua mhariri wa michezo kwa miaka kibao akiwa Nipashe na baadaye Mwananchi ambapo alikuwa msanifu mkuu gazeti hilo. Rais wa TFF Sir Leodegar Chilla Tenga anatarajia kutangaza rasmi uteuzi huo leo
Boniface Wambura anachukua nafasi ya Afisa Habari wa TFF baada ya aliekuwa anashika nafasi hiyo Florian Kaijage kutimuliwa baada ya kuboronga. Kabla ya kushika wadhifa huo Boniface alikuwa mhariri mkuu wa Jambo Leo







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Yaani mhariri wa michezo au msanifu anapewa kazi ya utendaji mkuu wa TFF, shirikisho lenye bajeti kubwa, malengo, n.k. kweli? Usaili umefanywa na KPMG au na Tenga mwenyewe? Ah. All the best Ngeta, unajikwaa unaanguka kwenye sinia la pilau?

    ReplyDelete
  2. Mungu mkubwa jamani,huyu Jimmy Kabwe kafanana na Bw.Uhuru Kenyata ! kweli watu ufanana!

    ReplyDelete
  3. Give him time.
    Kinachohitajika ni team work spirit. Huyu ni Mtanzania ambaye hisia na upendo wake katika soka huwezi kuzitilia shaka hata kidogo. Msimhukumu. Hongera Mwananchi Ngeta.

    ReplyDelete
  4. Swala siyo kuwa Mtanzania. Swala in Uwezo. Uzalendo na uraia ni vitu viwili tofauti. Kuna raia wa nchi za nje wengi waliyofanya makubwa kwa nchi yetu. Hivyo tukiangalia "uraia" tu.. tutaungua...

    ReplyDelete
  5. I am not sure if this appointment will resolve any long term development hurdles between TFF and other interested parties in sports circles.
    For sure it will improve the working relationship between TFF and the media.
    We sports people we propose the following from Mr Osiah:-
    1-Trancparancy within TFF activities.

    2-Equal budget for national mens and women teams, so they can have the same resources.

    3-A proper TFF website with all the information/records of players/Statistics for all clubs, players,leaders and history of the football in our country.

    ReplyDelete
  6. Kweli kabisa, ni aibu kuwa site ya TFF haina hata live results za mechi za ligi . Jamani akina Jimmy Kabwe mlifanyie kazi hilo tuwe na live results za ligi kwenye site,kwani zitakuwa ni official zaidi, siyo mpaka kipindi cha michezo radio One. Ni vitu vidogo lakini vitaonyesha umakini wenu. Ni ushauri wa bure.

    Mimi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...