HABARI ZIMETUFIKIA KWAMBA MWANAMUZIKI MAARUFU NA KIPENZI CHA WENGI RAMADHANI MTORO ONGARA MAARUFU KAMA 'DK. REMMY' AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO NYUMBANI KWAKE MBEZI.
HABARI ZINASEMA MSIBA UTAKUWA NYUMBANI KWAKE SINZA KWA REMMY JIJINI DAR. TAARIFA ZAIDI ZA MAZISHI TUTAWALETEA KADRI ZITAVYOPATIKANA.
DR REMMY ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WANAMUZIKI MAHIRI WALIOKUWA NYOTA KATIKA TASNIA HIYO KWA MUDA MREFU SANA. MIAKA YA KARIBUNI ALIACHANA NA MUZIKI WA KIDUNIA NA KUOKOKA AMBAPO ALIIMBA NYIMBO ZA INJILI KWA MAFANIKIO MAKUBWA.
DK. REMMY ATAKUMBUKWA PIA KWA KUWA MWANAMUZIKI WA KWANZA ALIYEIMBA HADHARANI FAIDA YA MATUMIZI YA KONDOM KATIKA WIMBO WAKE 'MAMBO KWA SOKSI' AMBAO HATA HIVYO ULIPIGWA VITA SANA KWA KILE KILICHOITWA ATI KUKIUKA MAADILI KIASI HATA UKAFIFIA KWA MSHANGAO WA WENGI.
MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
-AMINA
NENDA BONGO CELEBRITY ILI KUSOMA
MENGI ZAIDI KUHUSU DK REMMY
BOFYA HAPA
DR REMMY ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WANAMUZIKI MAHIRI WALIOKUWA NYOTA KATIKA TASNIA HIYO KWA MUDA MREFU SANA. MIAKA YA KARIBUNI ALIACHANA NA MUZIKI WA KIDUNIA NA KUOKOKA AMBAPO ALIIMBA NYIMBO ZA INJILI KWA MAFANIKIO MAKUBWA.
DK. REMMY ATAKUMBUKWA PIA KWA KUWA MWANAMUZIKI WA KWANZA ALIYEIMBA HADHARANI FAIDA YA MATUMIZI YA KONDOM KATIKA WIMBO WAKE 'MAMBO KWA SOKSI' AMBAO HATA HIVYO ULIPIGWA VITA SANA KWA KILE KILICHOITWA ATI KUKIUKA MAADILI KIASI HATA UKAFIFIA KWA MSHANGAO WA WENGI.
MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
-AMINA
NENDA BONGO CELEBRITY ILI KUSOMA
MENGI ZAIDI KUHUSU DK REMMY
BOFYA HAPA



R.I.P Remmy Ongala
ReplyDeleteMungu ailaze roho yake mahala pema peponi, kweli KIFO hakina huruma.
ReplyDeleteRIP REMMY
ReplyDeleteR.I.P Doctor,imeniuma saana kupata habari hizi,ulikua ni mwanamuziki wa ukweli,msema kweli,asiye kubali hilo,basi ni mtoto wa juzi. mimi binafsi nimelicheza sana talakaka miaka ya 80 Silent inn Mwenge, na Muleba Bar Mabibo,nilikua sikosi. Poleni sana wafiwa na watanzania wote kwa ujumla,kwani kifo chako Doctor ni kifo cha kitaifa,mungu ailaze roho ya marehemu Doctor mahali pema peponi Amen.
ReplyDeleteR.I.P Dr. Remmy, MUNGU awaongoze wale wote waliokuwa karibu na marehemu na kuwapa nguvu katika maandalizi yote ya kumpumzisha kwa amani.
ReplyDeleteRIP Dr. Remmy
ReplyDeleteDude was a musical genious!! almost as good as Bob Marley. R.I.P Souljah.
ReplyDeleteRIP DR REMMY,NILIJUA TU SIKU UKIFA HUU WIMBO UTATUACHIA MAJONZI SANAAAAAA....
ReplyDeleteBwana alitoa,Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. R.I.P
ReplyDeletekweli nimeshtushwa
ReplyDeleteRIP Doc u ur a star
R.I.P Remmy,,,,kweli kifo hakina huruma
ReplyDeleteMUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI..NIMEPATA MSHITUKO SANA NA KIFO CHA REMMY ONGALA...KWELI KIFO HAKINA HURUMA!!!KAPUMZIKE REMMY,KAPUMZIKE BABA...MWENYENZI MUNGU KESHA KUTANGULIA,ULIJIANDAA VEMA NA KIFO CHAKO KWA KUOKOKA......KIFO KIFO KIFO KWELI HAKINA HURUMA...
ReplyDeleteR.I.P DR REMMY ONGALA UTAKUMBUKWA KWA MENGI
ReplyDeleteOh dear, R.I.P
ReplyDeleteOd dear, R.I.P
ReplyDeleteMUNGU ILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU-DAKO
ReplyDeletepumzika kwa amani.Dr Remmy...bado tutaendelea kukumbuka kwa mengi hususani nyimbo zako kama sauti ya myonge,dodoma,narudi nyumbani..RIP
ReplyDeleteDr.Remmy tutakukumbuka kwa mengi hasa kwa muziki wako uliotulia. Mungu wafaraja aifariji familia yako. Amen
ReplyDeleteRIP Daktari wa muziki,
ReplyDeleteNitakumbukwa kwa mengi hasa pale uliponyang'anywa ushindi wa wazi kabisa kwenye mashindano ya sura mbaya na akapewa yule "Kisura".
Kweli kifo hakina huruma. Kati ya wanamuziki waliojua kufikisha ujumbe kwa jamii, Dr Remmy alikuwa ni mmojawapo na alikuwa na namna ya peke yake ya kufikisha ujumbe katika sanaa hii ya muziki. Wakati wengine waliogopa kuzungumzia kifo, remmy alivunja ukimya alipokuwa na Makassy kwa kuimba siku ya kufa, wimbo ambao mpake leo ukiusikiliza utadhani ni ujumbe ulioshushwa na nabii kutoka mbinguni. Baada ya hapo katika bendi yake mwenyewe ya Matimila akatoa kifo hakina huruma. Wengi wanaweza kusema kuwa Dr Remmy alikuwa anakiogopa kifo ndio maana aliimba nyimbo hizo mbili. Lakini mimi nadhani Dr Remmy alikuwa anafikisha ujumbe kwa watu kuwa tuishi Duniani tutakavyo lakini tukubali ukweli kuwa kila mtu atakufa siku moja. Hivyo kila mtu aishi akijua kuwa siku moja atakufa; lini,wapi, namna gani na tukiwa ha hali gani hatujui. Hivyo ni jukumu letu wenyewe kujiandaa na hiki kitu kinachoitwa kifo. Kuna watu mpaka leo ukiwaambia waachike wosia ili watoto wao wasije wakasumbuliwa baada ya wao kufa wanaona kama vile unawaletea mkosi. Matokeo yake watoto, wake wananyang'anywa mali zao bila kupata msaada wowote.
ReplyDeleteWe will remember you Dr Remmy your legacy to our nation.
R.I.P Dr Remmy
Mdau Mbezi Louis
We have lost a truly music champion, but I hope we tender to his many messages left in his music. I think his lately choice of salvation meant a lot to his live. I believe it was about re-discovering and re-searching for a new dimension and comfort ness. Surely you will see that comfort ness in the heaven, Remmy. Sorry for the lost to his family and to everyone who knew this music champ. God rest him in peace. Amen
ReplyDeleteKifooo... kifooo.. kifo hakina hurumaaa.. rip dr remmy
ReplyDeleteKweli KIFO HAKINA HURUMA.....Kimemchukua na Dr. Remmy jamani (RIP)
ReplyDeleteMwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi Ongala. Awape nguvu na imani familia yake yote.
ReplyDeletealiimba wimbowenye maneno yasemayo kwa Mungu kuna giza kwa mungu hatuonani.Alipoulizwa kwa nini anasema kwa mungu kuna giza akajibu kuwa anavyojua jehanamu ndio kuna mwanga kwa sababu jehanamu kuna moto hivyo penye moto ndipo mwanga upo mbinguni hamna moto hivyo hakuna mwanga.
ReplyDeleteMwanga wa milele umwangazie mwanga upi umwangazie atajijua huko aendako.
Ankal, naomba globu yako itupatie link ya miziki yake angalau tuisikilize katika kipindi hiki kigumu cha majozi ya mpendwa wetu, jabali la muziki Dr. Remmy Ongalla - Super Matimila Band.
ReplyDeleteR.I.P Remmy!!
R.I.P Remmy!
ReplyDeleteKifooo kifoo kifo hakina hurumaa kifo kilimuua Mbaraka Mwinshee kifo ohhh kifo kifo kilimua Hemedi maneti oh kifo shauri yako kifoo Kifo kilimuua Aziza Mbilili wa pale Kino kifoo kifo kikamuua Baamary shauri yako kifoo
ReplyDeleteRest in Peace Mkubwa
Pah More Jah
ZAUNUNU-AMSTERDAM
R.I.P All Tanzanians will miss you your music and the words of wisdom embeded in them
ReplyDeleteLets celebrate and give thanks
ReplyDeleteFor he has not died
He has just crossed over to the other side
To join Gabriels big band
Kifo hakina huruma....R.I.P!!
ReplyDeleteKweli:
ReplyDeleteTULITOKA KWA UDONGO NA TUTARUDI KWA UDONGO!
Pumzika!
Brother Remmy Ongala R.I.P
ReplyDelete/Vumbi Dekula Sweden
R.I.P DR.REMMY KIFO HAKINA HURUMA TANGULIA MBELE YAKO NYUMA YETU.MUZIKI NA USIA WAKO HAKIKA KWA WANAOTHAMINI WATAUUWENZI NA KUWA FUNDISHO KWA VIZAZI VIJAVYO
ReplyDeleteMENGI YA KUANDIKA LAKINI POLENI SANA
TUKO PAMOJA KWENYE KIPINDI IKI KIGUMU
MPILI ALHAJI MPILI
mhghhhfff!!! mbele ya kifo hautambi ...
ReplyDeletejamaa anastahili hiyo hadhi ya udaktari wa muziki, we acha tu.
unajua nini? alikuwa na dizaini fulani ya upigaji wa muziki ambayo ni ya pekee, yaani ukisikiliza muziki kwa sekunde tano utajua huyo ni Remmy
kali zaidi ni ujumbe wake, ingawa wafanyasiasa walimleteaga zengwe wakati fulani lakini this guy has left some legacy
hivi ule mtaa bado unaitwa jina lake kule sinza?
Dr Remmy, RIP. Umetutoka lakini bado utakuwa nasi kwenye miziki yako ya busara na ukweli. Mungu aipumzishe roho yako mahali pema Peponi. Amin.
ReplyDeleteUlimwengu bila watu si ulimwengu tena,RIP tutakukumbuka daima milele.
ReplyDeleteRIP daktari kimwili umetutoka lkn kiroho tuko pamoja na wewe, amen
ReplyDeleteRIP Dr. Remmy,
ReplyDeleteUtakumbukwa daima.
R.I.P.DOCTOR TUTAKUKUMBUKA SANA KWA NYIMBO ZAKO.PROFESSOR SEATTLE WA
ReplyDeleteSitosahau one day nilikuwa kwenye duka moja la vitabu hapa Marekani na kwenye spika nikasikia wimbo wa Dr. Remmy unapigwa. Pia one day nilikuwa naendesha gari na kusikiliza NPR na nakasikia wimbo wa Dr. Remmy.
ReplyDeleteRest in Peace TZ Legend.Mchango wako ulikuwa mkubwa sana kwenye jamii yetu.
R.I.P. Dr. Remmy. You're gone but your music will last forever.
ReplyDeleteR.I.P kawasalimie majabali wa muziki wenzio; Mbaraka Mwinsheh, R Marijani, Ndala Kasheba n.k.
ReplyDeleteMdau
London
NDIYO ALIKUA MGENI, NDIYO ALIOA MGENI LAKINI KWA KAZI YAKE YA SANAA, RAMADHANI MTOLO ONGALA ALICHANGIA KUIWEKA TANZANIA HAPA ILIPO.
ReplyDeleteUTAMADUNI NI SEHEMU KUBWA YA KUIFINYANGA JAMII.
TUMSHUKURU MUNGU S.A.W KWA MAISHA YA REMMY NA TUIOMBEE FAMILIA YAKE AMANI NA MOYO WENYE KURIDHIA. AMEN
MAINA ANG'IELA OWINO.
KWA KWELI TUNA MAJONZI SANA, TULIKUWA TUNASUBIRI KWA HAMU KIBAO CHAKO KIPYA ULICHOSEMA UTAWATUNGIA WAUGUZI! LAKINI KUMBE MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI AKAKUITA KWAKE. R.I.P DR.
ReplyDeleteR.I.P DR REMMY!
ReplyDelete