MAREHEMU DK REMMY ONGALA ENZI ZA UHAI WAKE

HABARI ZIMETUFIKIA KWAMBA MWANAMUZIKI MAARUFU NA KIPENZI CHA WENGI RAMADHANI MTORO ONGARA MAARUFU KAMA 'DK. REMMY' AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO NYUMBANI KWAKE MBEZI.

HABARI ZINASEMA MSIBA UTAKUWA NYUMBANI KWAKE SINZA KWA REMMY JIJINI DAR. TAARIFA ZAIDI ZA MAZISHI TUTAWALETEA KADRI ZITAVYOPATIKANA.

DR REMMY ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WANAMUZIKI MAHIRI WALIOKUWA NYOTA KATIKA TASNIA HIYO KWA MUDA MREFU SANA. MIAKA YA KARIBUNI ALIACHANA NA MUZIKI WA KIDUNIA NA KUOKOKA AMBAPO ALIIMBA NYIMBO ZA INJILI KWA MAFANIKIO MAKUBWA.

DK. REMMY ATAKUMBUKWA PIA KWA KUWA MWANAMUZIKI WA KWANZA ALIYEIMBA HADHARANI FAIDA YA MATUMIZI YA KONDOM KATIKA WIMBO WAKE 'MAMBO KWA SOKSI' AMBAO HATA HIVYO ULIPIGWA VITA SANA KWA KILE KILICHOITWA ATI KUKIUKA MAADILI KIASI HATA UKAFIFIA KWA MSHANGAO WA WENGI.

MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
-AMINA

NENDA BONGO CELEBRITY ILI KUSOMA
MENGI ZAIDI KUHUSU DK REMMY
BOFYA HAPA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. R.I.P Remmy Ongala

    ReplyDelete
  2. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, kweli KIFO hakina huruma.

    ReplyDelete
  3. R.I.P Doctor,imeniuma saana kupata habari hizi,ulikua ni mwanamuziki wa ukweli,msema kweli,asiye kubali hilo,basi ni mtoto wa juzi. mimi binafsi nimelicheza sana talakaka miaka ya 80 Silent inn Mwenge, na Muleba Bar Mabibo,nilikua sikosi. Poleni sana wafiwa na watanzania wote kwa ujumla,kwani kifo chako Doctor ni kifo cha kitaifa,mungu ailaze roho ya marehemu Doctor mahali pema peponi Amen.

    ReplyDelete
  4. R.I.P Dr. Remmy, MUNGU awaongoze wale wote waliokuwa karibu na marehemu na kuwapa nguvu katika maandalizi yote ya kumpumzisha kwa amani.

    ReplyDelete
  5. RIP Dr. Remmy

    ReplyDelete
  6. Dude was a musical genious!! almost as good as Bob Marley. R.I.P Souljah.

    ReplyDelete
  7. RIP DR REMMY,NILIJUA TU SIKU UKIFA HUU WIMBO UTATUACHIA MAJONZI SANAAAAAA....

    ReplyDelete
  8. Bwana alitoa,Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. R.I.P

    ReplyDelete
  9. kweli nimeshtushwa
    RIP Doc u ur a star

    ReplyDelete
  10. R.I.P Remmy,,,,kweli kifo hakina huruma

    ReplyDelete
  11. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI..NIMEPATA MSHITUKO SANA NA KIFO CHA REMMY ONGALA...KWELI KIFO HAKINA HURUMA!!!KAPUMZIKE REMMY,KAPUMZIKE BABA...MWENYENZI MUNGU KESHA KUTANGULIA,ULIJIANDAA VEMA NA KIFO CHAKO KWA KUOKOKA......KIFO KIFO KIFO KWELI HAKINA HURUMA...

    ReplyDelete
  12. R.I.P DR REMMY ONGALA UTAKUMBUKWA KWA MENGI

    ReplyDelete
  13. Oh dear, R.I.P

    ReplyDelete
  14. Od dear, R.I.P

    ReplyDelete
  15. MUNGU ILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU-DAKO

    ReplyDelete
  16. pumzika kwa amani.Dr Remmy...bado tutaendelea kukumbuka kwa mengi hususani nyimbo zako kama sauti ya myonge,dodoma,narudi nyumbani..RIP

    ReplyDelete
  17. Keland Primary SchoolDecember 13, 2010

    Dr.Remmy tutakukumbuka kwa mengi hasa kwa muziki wako uliotulia. Mungu wafaraja aifariji familia yako. Amen

    ReplyDelete
  18. Abiola Jr. New Albany, OhioDecember 13, 2010

    RIP Daktari wa muziki,
    Nitakumbukwa kwa mengi hasa pale uliponyang'anywa ushindi wa wazi kabisa kwenye mashindano ya sura mbaya na akapewa yule "Kisura".

    ReplyDelete
  19. Kweli kifo hakina huruma. Kati ya wanamuziki waliojua kufikisha ujumbe kwa jamii, Dr Remmy alikuwa ni mmojawapo na alikuwa na namna ya peke yake ya kufikisha ujumbe katika sanaa hii ya muziki. Wakati wengine waliogopa kuzungumzia kifo, remmy alivunja ukimya alipokuwa na Makassy kwa kuimba siku ya kufa, wimbo ambao mpake leo ukiusikiliza utadhani ni ujumbe ulioshushwa na nabii kutoka mbinguni. Baada ya hapo katika bendi yake mwenyewe ya Matimila akatoa kifo hakina huruma. Wengi wanaweza kusema kuwa Dr Remmy alikuwa anakiogopa kifo ndio maana aliimba nyimbo hizo mbili. Lakini mimi nadhani Dr Remmy alikuwa anafikisha ujumbe kwa watu kuwa tuishi Duniani tutakavyo lakini tukubali ukweli kuwa kila mtu atakufa siku moja. Hivyo kila mtu aishi akijua kuwa siku moja atakufa; lini,wapi, namna gani na tukiwa ha hali gani hatujui. Hivyo ni jukumu letu wenyewe kujiandaa na hiki kitu kinachoitwa kifo. Kuna watu mpaka leo ukiwaambia waachike wosia ili watoto wao wasije wakasumbuliwa baada ya wao kufa wanaona kama vile unawaletea mkosi. Matokeo yake watoto, wake wananyang'anywa mali zao bila kupata msaada wowote.
    We will remember you Dr Remmy your legacy to our nation.

    R.I.P Dr Remmy

    Mdau Mbezi Louis

    ReplyDelete
  20. We have lost a truly music champion, but I hope we tender to his many messages left in his music. I think his lately choice of salvation meant a lot to his live. I believe it was about re-discovering and re-searching for a new dimension and comfort ness. Surely you will see that comfort ness in the heaven, Remmy. Sorry for the lost to his family and to everyone who knew this music champ. God rest him in peace. Amen

    ReplyDelete
  21. Kifooo... kifooo.. kifo hakina hurumaaa.. rip dr remmy

    ReplyDelete
  22. Kweli KIFO HAKINA HURUMA.....Kimemchukua na Dr. Remmy jamani (RIP)

    ReplyDelete
  23. Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi Ongala. Awape nguvu na imani familia yake yote.

    ReplyDelete
  24. aliimba wimbowenye maneno yasemayo kwa Mungu kuna giza kwa mungu hatuonani.Alipoulizwa kwa nini anasema kwa mungu kuna giza akajibu kuwa anavyojua jehanamu ndio kuna mwanga kwa sababu jehanamu kuna moto hivyo penye moto ndipo mwanga upo mbinguni hamna moto hivyo hakuna mwanga.

    Mwanga wa milele umwangazie mwanga upi umwangazie atajijua huko aendako.

    ReplyDelete
  25. Ankal, naomba globu yako itupatie link ya miziki yake angalau tuisikilize katika kipindi hiki kigumu cha majozi ya mpendwa wetu, jabali la muziki Dr. Remmy Ongalla - Super Matimila Band.

    R.I.P Remmy!!

    ReplyDelete
  26. R.I.P Remmy!

    ReplyDelete
  27. Kifooo kifoo kifo hakina hurumaa kifo kilimuua Mbaraka Mwinshee kifo ohhh kifo kifo kilimua Hemedi maneti oh kifo shauri yako kifoo Kifo kilimuua Aziza Mbilili wa pale Kino kifoo kifo kikamuua Baamary shauri yako kifoo

    Rest in Peace Mkubwa
    Pah More Jah

    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  28. R.I.P All Tanzanians will miss you your music and the words of wisdom embeded in them

    ReplyDelete
  29. Lets celebrate and give thanks
    For he has not died
    He has just crossed over to the other side
    To join Gabriels big band

    ReplyDelete
  30. Kifo hakina huruma....R.I.P!!

    ReplyDelete
  31. Kweli:

    TULITOKA KWA UDONGO NA TUTARUDI KWA UDONGO!

    Pumzika!

    ReplyDelete
  32. Brother Remmy Ongala R.I.P
    /Vumbi Dekula Sweden

    ReplyDelete
  33. R.I.P DR.REMMY KIFO HAKINA HURUMA TANGULIA MBELE YAKO NYUMA YETU.MUZIKI NA USIA WAKO HAKIKA KWA WANAOTHAMINI WATAUUWENZI NA KUWA FUNDISHO KWA VIZAZI VIJAVYO
    MENGI YA KUANDIKA LAKINI POLENI SANA
    TUKO PAMOJA KWENYE KIPINDI IKI KIGUMU
    MPILI ALHAJI MPILI

    ReplyDelete
  34. mhghhhfff!!! mbele ya kifo hautambi ...
    jamaa anastahili hiyo hadhi ya udaktari wa muziki, we acha tu.

    unajua nini? alikuwa na dizaini fulani ya upigaji wa muziki ambayo ni ya pekee, yaani ukisikiliza muziki kwa sekunde tano utajua huyo ni Remmy

    kali zaidi ni ujumbe wake, ingawa wafanyasiasa walimleteaga zengwe wakati fulani lakini this guy has left some legacy

    hivi ule mtaa bado unaitwa jina lake kule sinza?

    ReplyDelete
  35. Dr Remmy, RIP. Umetutoka lakini bado utakuwa nasi kwenye miziki yako ya busara na ukweli. Mungu aipumzishe roho yako mahali pema Peponi. Amin.

    ReplyDelete
  36. Rehema KileleDecember 13, 2010

    Ulimwengu bila watu si ulimwengu tena,RIP tutakukumbuka daima milele.

    ReplyDelete
  37. RIP daktari kimwili umetutoka lkn kiroho tuko pamoja na wewe, amen

    ReplyDelete
  38. RIP Dr. Remmy,
    Utakumbukwa daima.

    ReplyDelete
  39. R.I.P.DOCTOR TUTAKUKUMBUKA SANA KWA NYIMBO ZAKO.PROFESSOR SEATTLE WA

    ReplyDelete
  40. Sitosahau one day nilikuwa kwenye duka moja la vitabu hapa Marekani na kwenye spika nikasikia wimbo wa Dr. Remmy unapigwa. Pia one day nilikuwa naendesha gari na kusikiliza NPR na nakasikia wimbo wa Dr. Remmy.

    Rest in Peace TZ Legend.Mchango wako ulikuwa mkubwa sana kwenye jamii yetu.

    ReplyDelete
  41. R.I.P. Dr. Remmy. You're gone but your music will last forever.

    ReplyDelete
  42. R.I.P kawasalimie majabali wa muziki wenzio; Mbaraka Mwinsheh, R Marijani, Ndala Kasheba n.k.

    Mdau
    London

    ReplyDelete
  43. NDIYO ALIKUA MGENI, NDIYO ALIOA MGENI LAKINI KWA KAZI YAKE YA SANAA, RAMADHANI MTOLO ONGALA ALICHANGIA KUIWEKA TANZANIA HAPA ILIPO.

    UTAMADUNI NI SEHEMU KUBWA YA KUIFINYANGA JAMII.
    TUMSHUKURU MUNGU S.A.W KWA MAISHA YA REMMY NA TUIOMBEE FAMILIA YAKE AMANI NA MOYO WENYE KURIDHIA. AMEN

    MAINA ANG'IELA OWINO.

    ReplyDelete
  44. KWA KWELI TUNA MAJONZI SANA, TULIKUWA TUNASUBIRI KWA HAMU KIBAO CHAKO KIPYA ULICHOSEMA UTAWATUNGIA WAUGUZI! LAKINI KUMBE MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI AKAKUITA KWAKE. R.I.P DR.

    ReplyDelete
  45. R.I.P DR REMMY!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...