. Rais wa Shirikisho la Masumbwi Nchini (PST), Emamanuel Mlundwa akimwonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Emmanuel Nchimbi uliongo wa masumbwi masumbwi uliotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya Bold Air, Bw. John Nduguru (Kushoto) kabla ya kuuzindua wikiendi ilopita.
Faraji Sayuni akipokea masumbwi kutoka kwa Ramadhani Kumbele wakati wa pambano la utangulizi katika hafla ya kukabidhiwa kwa ulingo wa masumbwi uliotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya Bold Air, John Nduguru Shirikisho la Masumbi nchini (PST) na kuzinduliwa na Wazir wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, Keko jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Michael Matemanga



Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na michezo Emmanuel Nchimbi amewataka watanzania kujitolea vifaa vya michezo ili kusaidia kuinua vipaji vya vijana nchini.

Akizungumza jijini Dar alipozindua ulingo wa ndondi aulitolewa ana Mkurugenzi wa kampuni ya binafsi ya ndege ya Bold Air, Bw. John Ndungulu, Waziri Nchimbi alisema yuko tayari kushirikiana na kusaidia watu wanaojitolea kwa ajili ya kuendeleza michezo.

“Nimefurahi sana kuona ulingo ni mzuri na unafaa kwa ajili ya kuandaa vijana wetu. Naomba usiishie hapa tu bali waeleze watanzania wengine waishio marekani na nchi nyingine wajitokeze kusaidia michezo” alisema.

Nchimbi ambaye alishuhudia mapambano ya ndoni ya watoto na vijana katika viwanja vya Keko Mambembea alisema wizara yake inaweka mikakati ya kuitangaza nchi kwa kupitia michezo.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Masumbwi laTanzania (PST), Emmanuel Mlundwa alisema kuwa kupatikana kwa ulingo huo utasaidia si tu ngumi za kilipwa bali hata za ridhaa kwani ulingo uliokuwepo ulinunuliwa miaka ya sabini.

Alisema pamioja na kutokuwepo kwa ulingo bora kwa kipindi chote lakini watanzania wameweza kufanya vyema na kuwepo kwa mabingwa wadunia katika ngumi za kulipwa na kick boxing.

Nae Mkurugenzi wa Bold Air, Bw. Ndungulu alisema kuwa amejitolea ulingo huo ukiwa ni mwanzo tu katika kusaidia michezo nchini na yuko tayari kusaidia nyanja nyinge za michezo ikiwemo ngumi.

“Tanzania hatujulikani sana kama wenzetu Kenya kwa sababu katika michezo tuko nyuma. Hata kule Marekani wanashangaa ukiwaambia u Mtanzania kwa kuwa wanawajua wakenya kutokana na Marathon” alisema na kuongez akuwa kama watanzania wakijitolea katika michezo nchi itanufaika kiuchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...