Meneja Mkuu wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano wa kutangaza siku ya fainali za mashindano ya BONGO STAR SEARCH uliofanyika mchana huu Savannah Lounge,Benjamin Mkapa Tower.kushoto ni Mkurugenzi wa Benchmark Productions,Madam Ritha Paulsen akifuatilia mkutano huo.Fainali hizo zimepangwa kufanyika Desemba 17,2010 katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,jijini Dar
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi mil. 30 kwa ajili ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya hayo ya Bongo Star Seatch 2010 kwa Mkurugenzi wa Benchmark Productions,Madam Ritha Paulsen.katikati ni Mratibu wa BASATA,Bi. Vicky Temu.
Tano Bora wa Bongo Star Search 2010 wakiwa wameshikilia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi mil. 30 atakayoipata mshindi wa mashindano hayo.wengine ni Mkurugenzi wa Benchmark Productions,Madam Ritha Paulsen (tatu kushoto),Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo,George kavishe (katikati) na kulia ni Mratibu wa BASATA,Vicky Temu.

wadau mmemuona mshindi? ni huyo wa.... kutoka kulia.
ReplyDeleteMadam Ritha, nimeguswa kisawasawa na mvuto ulionao, tafadhali nijulishe umri wako na "marital status" yako.
ReplyDeleteNaahidi sitakuvunjia heshima wala kuchafua hali ya hewa ila nataka tu nijiridhishe nafsi yangu.
Ankal, mara nyingi unanitupa kapuni ila naomba hii imfikie mlengwa.
JAMANI SISI WA WILAYA YA ILALA, TEMEKE NA BAADHI YA SEHEMU ZA KINONDONI (MORO ROAD)MBONA MMETUSAHAU HAMNA VITUO VYA KUPATIA TICKETI ZA BSS??? AU SHINDANO HILI NI LA WATU WA BAADHI YA MAENEO TU??? MUACHE UBAGUZI
ReplyDeleteWote hao 5 wana vipaji lakini ukweli usiofichika ni kwamba Waziri Salum yuko juu ya wote.
ReplyDeleteWataalam & hata wasio wataalam wa muziki wanaweza kuona hili bila shida yeyote. Na hii ndiyo inaipa sifa BSS kuliko mashindano mengine kama ya Miss Tz nk ambapo malalamiko huwa ni mengi sana wakati wa matokeo.
'Mzungu' anamfuatia (#2), tatizo lake ni dogo tu kuto- match beats with movements kama kawaida yao.
Endapo itatokea ukawa hukuchaguliwa (Chini ya Mbingu lolote lawezekana), kweli bro. Waziri, jitokeze hapa kwa Michuzi tuwasiliane, binafsi nitakupongeza kibinafsi na hata Mungu ninayemwamini atakuzidishia!