DADA ZETU CHAMBO CHA KUWAPATIA URAIA WAGENI
Jana nilipata sijui niite bahati au balaa? Call it eye opener. Nilikwenda kweye msiba huko Mbezi ya Kimara. Katika huo msiba, dada yetu (soma mtanzania) alifariki na “mumewe” ni mtu wa Afrika Magharibi, almaarufu kwa kucheza sinema zenye kuvuta hisia za watu wengi.
Idadi kubwa sana ya raia wa nchi hiyo katika huo msiba ilinifanya nijiulize maswali kadha wa kadha. Wanafanya nini wote hao nchini? Wana vibali vya kuishi nchini kihalali? Si vema ku judge mtu kwa sura yake au alivyo ila kwa tathmini ya haraka kuhusu raia hao wa kigeni, wengi wao niwanalekea ni misheni town.
Raia wengi wa kigeni wanaotaka kuishi nchini wanakimbilia kuwaghilibu dada zetu wawaoe na kuwazalisha ili wapate uhalali wa kukaa bila ya kubugudhiwa. Na dada zetu katika harakati za “to make the ends meet” wanaingia katika mitego hii bila ya kujijua.
Akina kaka nao kwa mbalii wanakuja katika huu mtego. Akishampata mke wa kigeni (wakenya wanaongoza), utitiri wa ndugu wanakuja kwa shem!.Halafu? Malizia sehemu ya mwisho waraka huu
Mlango mwingine usiotamkwa sana unaotumiwa kuwaingiza wageni ni kwa kupitia taasisi za kidini. Kuna makanisa mpaka wafagizi wametoka nje. Watumishi wa Mungu wanaokwenda kupata neno la Mungu katika makanisa hayo wafumbue macho na kuhoji uhalali wa kuleta wafanyakazi toka nje! Tena wahubiri ndo wamechachamaa na kufagilia inter marriages eti kuwa zinaleta maendeleo! (Commercialization of religions)
Sina maana ya ubaguzi ila kama ni kuja nchini waje kwa kufuata taratibu zinazotakiwa na muda wao ukiisha waondoke pasi na hodi. Wamejazana huko kariakoo, Kinondoni na kwenye viwanda, magereji na magodown. Jamani mpaka masokoni nako tunahitaji “maexpatriate”?
Mamlaka husika kwa maana ya vyombo vya uhamiaji na vinavyohusika na usalama wa raia, umefika wakati muafaka wa kuamka usingizini na kutuepusha na balaa linalokuja siku za usoni.
Napata maono ya kuwa inabidi hawa raia waliooa dada/kaka zetu wafuatiliwe kwa kina. Ndoa hizi huwa zinaishia vipi? Kwa divorce? Kwa vifo? Na akina nani wanakufa? Sisi au wao? Hatima ya watoto inaishiaje? Wanatelekezwa au wanachukuliwa/toroshwa kwenda “kwao”?
Jana nilipata sijui niite bahati au balaa? Call it eye opener. Nilikwenda kweye msiba huko Mbezi ya Kimara. Katika huo msiba, dada yetu (soma mtanzania) alifariki na “mumewe” ni mtu wa Afrika Magharibi, almaarufu kwa kucheza sinema zenye kuvuta hisia za watu wengi.
Idadi kubwa sana ya raia wa nchi hiyo katika huo msiba ilinifanya nijiulize maswali kadha wa kadha. Wanafanya nini wote hao nchini? Wana vibali vya kuishi nchini kihalali? Si vema ku judge mtu kwa sura yake au alivyo ila kwa tathmini ya haraka kuhusu raia hao wa kigeni, wengi wao niwanalekea ni misheni town.
Raia wengi wa kigeni wanaotaka kuishi nchini wanakimbilia kuwaghilibu dada zetu wawaoe na kuwazalisha ili wapate uhalali wa kukaa bila ya kubugudhiwa. Na dada zetu katika harakati za “to make the ends meet” wanaingia katika mitego hii bila ya kujijua.
Akina kaka nao kwa mbalii wanakuja katika huu mtego. Akishampata mke wa kigeni (wakenya wanaongoza), utitiri wa ndugu wanakuja kwa shem!.Halafu? Malizia sehemu ya mwisho waraka huu
Mlango mwingine usiotamkwa sana unaotumiwa kuwaingiza wageni ni kwa kupitia taasisi za kidini. Kuna makanisa mpaka wafagizi wametoka nje. Watumishi wa Mungu wanaokwenda kupata neno la Mungu katika makanisa hayo wafumbue macho na kuhoji uhalali wa kuleta wafanyakazi toka nje! Tena wahubiri ndo wamechachamaa na kufagilia inter marriages eti kuwa zinaleta maendeleo! (Commercialization of religions)
Sina maana ya ubaguzi ila kama ni kuja nchini waje kwa kufuata taratibu zinazotakiwa na muda wao ukiisha waondoke pasi na hodi. Wamejazana huko kariakoo, Kinondoni na kwenye viwanda, magereji na magodown. Jamani mpaka masokoni nako tunahitaji “maexpatriate”?
Mamlaka husika kwa maana ya vyombo vya uhamiaji na vinavyohusika na usalama wa raia, umefika wakati muafaka wa kuamka usingizini na kutuepusha na balaa linalokuja siku za usoni.
Napata maono ya kuwa inabidi hawa raia waliooa dada/kaka zetu wafuatiliwe kwa kina. Ndoa hizi huwa zinaishia vipi? Kwa divorce? Kwa vifo? Na akina nani wanakufa? Sisi au wao? Hatima ya watoto inaishiaje? Wanatelekezwa au wanachukuliwa/toroshwa kwenda “kwao”?


Ndugu yangu wewe umestuka leo? Sie wengine tuliowahi kufanya kazi na baadhi ya wageni tulikuwa tunawasikia kabisa wakisema lazima waoe hapa ili wapate kubaki.
ReplyDeleteTatizo tulilonalo Watanzania hatuuoni uzuri na opportunities zilizopo kwetu lakini kwa walio nje wanaziona na wanazitumia kwa kikamilifu. Sisi tuna ardhi isiyo na bughudha achilia mbali madini ya aina mbali mbali. Lakini kutwa badala ya watu kuwahimiza ndugu na jamaa zao kuzitumia hizo opportunities zilizopo tumebaki kulalamika na kusubiri "serikali" itufanyie hiki na kile, sasa kwanini wenye macho wasije kufaidi? Kuanzia rubby na mpaka madini mengine yanayoingiza pesa, na kuanza kujikatia mapori huko vijijini au mke/mume kwenda kununua vyote hivyo vyawavutia watu. Sie kazi yetu kupiga porojo tu na kusubiri tufanyiwe mambo na wanasiasa. Kalaghabaho na ubozi wetu waache Wapopo waje, tena nasikia kipindi hiki ndio wamejaa tele na bado wanaitana, na kwanini wasije wakati nchi imejaa rasilimali tele na wenyeji hawazioni?
Wewe acha ukalulu,tuwache kujidanganya wenyewe,maforeigners wote waliokuja hapa ni wale ambao before walikuwa na economical potential ambayo wapo kwa ajili ya kuinvest na kupanua business,hakuna mtu maskini anayeweza kuja kujaribu kuanzia maisha bongo,na swala la masister zetu kuolewa ni tatizo lao wenyewe kuchachutikia pesa,acha kujiumiza kichwa na foreigners bongo,jiumize na wale wabongo waliokwenda europe na kuukana utanzania na kujiita wasomali au warwanda.
ReplyDeletemdau Istanbul
watanzania pia wanafanya wanachofanya wao
ReplyDeletenchi yetu mgao wa umeme kutwa unataka kumnyima nani kuishi tz? kuna nini cha kujivunia zaidi ya kuwa hakuna war? na umadikini umejaaaaaaaaaaaaaaa? hata efcc hawawezi weka
kama mwanamke anaolewa na wanje acha aolewe hata wa tz wanafanya hivyo
kama hautaki waolewe na wa nje basi muache tabia mbaya wanaume nyie wa ki tz pia muwaoe
mie nimeshangazwa na wewe kulalamika, fuatilia maisha yako hakuna nchi duniani watu hawaishi bila kutafuta njia ya kujiendeleza au kupata kitu
na hao wa magharibi wanajua sana kulea mwanamke na kupendaaaaaaaaa
Swala la kufuata utaratibu ili watu waingie na kukaa nchini halina ubishi, ni wajibu wa mamlaka husika kuhakikisha wale wote wanaoingia nchini wanakuja kwa sababu zilizo ndani ya utararibu na kama wanabaki basi iwe ni kwa tija ya taifa na kama haieleweki wanafanya nini warudishwe makwao. Hata watanzania wako nchi nyingi duniani kwa madhumuni lukuki, si jambo la busara kuanza kuwasimanga ilhali wameenda huko kihalali kwa kufuata taratibu, wanafanya kazi kihalali, wanalipa kodi ma hawajihusishi na uhalifu. Tusije tukatamani kuona vigogo kwenye macho ya wenzentu wakati kwenye macho yetu kuna vibanzi.
ReplyDeleteInaelekea wewe mtoa mada hufahamu kabisa sheria za uhamiaji za Tanzania. Ningekushauri ukazisome kwanza kabla hujaendelea kuropoka kama ulivyo fanya. Mwanaume hapati uraia kwa kuoa mwanamke mtanzania. Uraia wanapewa wanawake walio olewa na waTZ tu! Nenda kaulize uhamiaji.
ReplyDeleteTatizo lenu wanaume watanzania hamjiamini. Oh dada zetu, oh bla bla. Acha dada zako watafute maisha kama unavyo yatafuta wewe.
Get educated, then talk!
Yup! umesema mwenyewe, mbaguzi wewe. Jinsi tu ulivyoyapanga maneno yaonesha wewe roho inakuuma saana kuona wageni wakija nchini na kutumia mianya iliyopo na kufanikiwa kimaisha. Tanzania wapo wabaguzi wengi sana na jinsi walivyo insensitive wanajionea sawa tu kuongea mambo ambayo yanaumiza roho za wenzao. Majina kama Bagacholi, Mmangakoko, wapopo n.k those are racial slurs. By the way....hata baadhi walioishi mamtoni ati huwaita African Americans Panyabuku, ama Wanugu! REALLY?? Stop. Please, have compassion for other people. Wanaokuja nchini wanakuja kutafuta maisha bora...that's our common purpose as human beings. Everyone of us wants what's best for us and our families, kama wamevunja sheria kuingia kinyume cha sheria hawajavunja sheria ya Mungu. Have mercy People!!. Kama hawakudhuru.....chuki ya nini?. Ukiona mwenzio anafanikiwa be smart, ask them what they do and how they do it...they might teach you something. By the way, hii inajumuisha immigrants wote wakongo, somalia, rwanda, na hata kutoka mabara mengine. Treat these people as decent human beings!!! Do you know that tens of thousands or even a hundreds of thousands of Tanzanians are in foreign countries illegaly right now??. Do you think they feel good seeing comments like yours in the newspapers where they are living?.
ReplyDeleteStop!. Just Stop! Let them be!. Na hao madada hawajalazimishwa kuolewa, huenda wamekubaliana.
Swali langu ni kuhusu Watanzania walioko nje ya nchi: Je nao wamekwenda kutafuta nini kama si riziki zao. Nakubaliana na hoja ya kwamba kila mtu mgeni aingiapo ndani ya nchi yoyote ile iwe kwa kujitafutia riziki basi afuate taratibu halali za UHAMIAJI.
ReplyDeletemdau hapo umesema kweli wacha wapopo waje tu bongo maana sisi wenyewe tumelala. pili masister zetu wakijua wewe foreigner basi hata kama huna pesa au mapenzi basi twendetu kisa mgeni.Watanzania wengine wapo mamtoni wanajihita wanyarwanda au wasomali na wengine wanaoa wa east euprope kuata uraia kwa hiyo yote ni maisha tu
ReplyDeleteHamna lolote wanakujaga mikono mitupu wanaondoka matajiri, kwanini Watanzania wanathamini wageni zaidi kuliko wazawa, Ulaya hawawezi kumudu maisha wanayoishi bongo, na kwa vile bongo zetu zimelala waona wanatuzidi spidi halafu unasema economic potential my foot! Wabongo wanaokwenda kuzamia kwa watu ni kama hao wanaokuja kuzamia kwetu tu hakuna tofauti, ila wa kwetu wanakimbia shida kwa kukosa msaada kwao. Subirini mje muone machotara wa Kichina watavyo waongozea nchi siku za usoni ...lol
ReplyDeletemkuki kwa nguruwe...... mbona wa tanzania wengi nje ya nchi wanatafuta makaratasi kwa njia hio hio ?
ReplyDeleteMtu wangu hilo ni swala la Ulimwengu mzima nchi zilizoendelea kubwa tu zimeshindwa mie mwenyewe Mbongo mwenzako nipo nche nyengine ya na nilipewa mwezi mmoja wa kuondoka kilichofwatia nikaoa sasa nina miaka 16 nimekomaa tu usiwe na wivu kama ulichukuliwa demu wako na wageni najua huwezi wapenda kabisa lakini sie wote ni waafrika hakuna kubaguana kama unataka wewe nenda Upoponi kajichukulie jana dume manake hawanasura wanajidai kwa dada zetu hapo Bongo na kwa upunda hahah wanaongoza.
ReplyDeleteRoho za kutu hizi,kwa nini usianze kuhesabu watanzania wanaopata uraia nchi za ulaya kwa kujiita wasomali,warundi,wanyaru,na wengine kuoa wazungu wazee.jamani tuache mtima nyongo,sasa hivi katika vijana 10 walipo ulaya watano wake zao wazungu,kisa kupata uraia wa nchi hizo.waache dada zako waoe wamtakae kama wameridhika.
ReplyDeleteKama hilo lipo hapo tz inabidi Home office wapambane nao kiukweli.
ReplyDeletesisi watz wanje mbona tunakimbizwa sana tusipokua na vibali vya kufanya kazi nje.Mbona nchi nyingine ziko makini sana na immigration?sisi kwanini tusiwabane wageni waje kihalali na kuondoka wamalizapo kazi zao?
Hao jamaa wa west africa kwao hakukaliki na hata mTz akiishi kwao wan ubaguzi wa hali ya juu.
Sio tu ukiwa nao africa,hata mfano hapa UK wao wakiwa na kazi wanaitana wenyewe na ikibahatika kupata kazi hapo basi ni ubaguzi kwa kwenda mbele.
Chekini hii jamani mamlaka husika.
Nyie wote hapo juu sababu zenu ni sawa lakini kitu kikubwa kinachowafanya watake kupata uraia wa hapa kwetu ni kuwa watakuwa na urahisi wa kupewa visa ya kwenda nchi yoyote bila ya kusukumbuliwa haswa marekani na UK.
ReplyDeleteJe, tukiwachunguza wabongo waliopo nchi za nje utakubali kuwa wengi wamefinga ndoa feki na kujiandikisha vyuo ambavyo hata sifa havina ili mradi waweze kuishi huko? Mim naishi nje na ninaweza kukuhakishia kuwa 90% ya wabaongo waliopo nje ni wale wa kudanganya hivo ng'oa kisiki kwenye jicho lako kwabla -----
ReplyDeletena dada zako na kaka zako kule ng'ambo wanafanya hivyo hivyo,sasa sijui na wao warudi?eti?
ReplyDeleteMtoa maoni nadhani kusema Wakenya au "wageni" wasioe wabongo ni fikra potofu. Zamani Wachaga, Wahaya, Wasukuma n.k wafanyabiashara na wafanyakazi waliingia Dar na wengi wao walioa nje ya makabila yao. Kwa kifupi waliobaki Makwao walibaki na fikra finyu na kuona kwamba kuoa lazima mtu aoe kutoka kabila lake na wapo watu wa namna hii mpaka leo... Mtu kuoa au kuolewa anaweza kuoa yeyote ilimradi wanaelewana. Ukisema kwamba wageni wanaoa wabongo kwa sababu ya kuishi nchini, je Wabongo waliooa Kenya wao tusemeje? Kazi kweli kweli... hivi hivi tutavunja ndoa za watu wengi kwa kigezo kwamba waume zao ni wageni. Tuende taratibu mchangia hoja. Dada zetu kama wanataka kuolewa na wageni na wamependana shida ikowapi? Wenye ajenda zao wapo hata wabongo kwa wabongo kuna wanaochagua kuolewa na matajiri....
ReplyDeletenchi ya ukoo wenu? mbona mchungu hivyo?
ReplyDeleteWewe kinakuuma nini kama watu wanaamua kuolewa? Hilo ni swala la binafsi, kwa sababu wewe hautaishi nao ndani ya nyumba. Wewe ni sawa na wale wazazi wanaowatafutia watoto wao wakwe wakati watoto ndio wataishi wenyewe kwenye nyumba. Mambo ya ndoa ni kati ya watu wawili, wewe waache wenyewe.
ReplyDeletekwa sheria zetu makini za uhamiaji ya mwaka 1995 mtu yeyote akioa mtanzania hapati uraia anatakiwa aende nae kwao hata kama ataishi hapa ni lazima awe na kibali cha kufanyia kazi hakuna favor hapolabda hao jamaa wanaishi kwa visa au vibali
ReplyDeletewewe mtoa maada ni bonge la mshambaa!!!!!!
ReplyDeleteEe bwana huu ni ubaguzi tu. We ukiibiwa mke na mtu aliyetoka Nigeria, utawalaumu wanigeria wote. Nafikiri hata mi mmbulu nikikuibia mke utatulaumu wote. Shida sio watu waliotoka nje. Shida ni fikra zako potofu.
ReplyDeleteWewe tatizo lako nini. Dalili ya wivu hiyo. Na wewe kaolewe basi
ReplyDeleteMsimlaumu mwenzenu hayajui maisha huyo. Wanawake wanataka wanaume wenye uwezo wa kuwaendesha. Hapa UK sasa mwanamume wa kiafrika ndio dili kwa taarifa yako, na kila ukiwa jitu la miraba minne basi unanyanganyiwa wa wanawake wa kizungu. Kwa sababu wewe ni mchapa kazi, utaweta pesa mke atumie.
ReplyDeleteNADHANI WENGI HAWAJAELEWA LENGO LA MTOA MADA; HOJA NI KWAMBA WANAOKUJA KUFANYA KAZI JE, NI KWAMBA NAFASI HIZO HAZIKUPATA WATANZANIA WA KUZIFANYA? JE, TARATIBU ZA UHAMIAJI ZINASEMAJE KUHUSU IDADI YA WAFANYAKAZI WA KIGENI KTK KAMPUNI AU SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI? NI VYEMA KAMA NI UCHUNGUZI UANZE NA NGO'S NYINGI ZINAINGIZA WAGENI KWA NAFASI ZINAZOWEZA KUSHIKWA NA WAZAWA.MNAKUMBUKA MPAKISTANI ALIYECHANA NOTO YA SS.5,000.00 MWANZA AIRPORT? NAFASI ALIYONAYO INGEWEZA KABISA KUSHIKWA NA MTZ. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI IPO?
ReplyDeleteKwa ufupi hizi ni fitna bin giliba, sasa sie tulio ughaibuni nao waanze kutuuliza mbona wabongo wanatuchukulia dada zetu na kaka zetu?
ReplyDeleteMdau
Makaratasi.
Tatizo letu wabongo (wa kawaida na watawala) tunaimba kwa sauti kubwa UTANDAWAZI, lakini vitendo vya kiutandawazi vinapotokea tnavilaani. mfano ni haya malalamiko ya watu kuoa au kuolewa na watu wa nchi nyingine. Vivyo uraia wa nchi mabili au tatu unapingwa na wabongo wa kawaida na baadhi ya watawala, nk. Huwezi kukumbatia utandawazi, kisha ukampinga haya yote.
ReplyDeletemhh!! tembea uone,ng'ambo wanaofanya hivyo ni wengi kama vinyweleo vya ng'ombe,wake kwa waume.
ReplyDelete