Ndugu Michuzi,
Napenda kukusalimia wewe na kikosi kizima cha blog ya jamii. Kupitia blog hii ya jamii, ninapenda kuwajulisha watanzania na watu wote kutoka Afrika ya Mashariki kwamba kuanzia tarehe 4 mwezi huu (Jumamosi), yaani kesho na kuendelea Kanisa letu la Umoja International Outreach limehamisha makao yake kutoka katika jengo la sasa lililopo katika anuani hii:
12727 Hillcrest Rd,
Dallas Tx,
75230

kwenda katika anuani hii:
6411 LBJ Freeway,
Dallas TX,
75240-6406.

Kanisa hili ndilo kanisa linatumiwa na watanzania wengi walioko hapa. Kwa msingi huo bas, shughuli zote za ibada za Jumapili pamoja na zile za kiushauri zitakuwa zinafanyika hapa.Hata hivyo kanisa hili jipya haliko mbali kutoka hili ambalo tunatumia sasa. Kwa watu ambao wanaishi katika jiji hili la Dallas ramani ni kama ifuatavyo;

Ukiwa unatoka 635 W utapiga U turn pale Hillcrest kama unarudi West au maeneo ya Gallaria na kanisa lipo kati ya Hillcrest Rd naPreston Rd kwenye service road. Ukiwa unatoka maeneo ya 635 East au upande wa 75 Hwy uta exit Hillcrest na utavuka taa za Hillcrest na mbele kabla hujafika Preston utaona kanisa mkono wako wa kulia.

Tunaomba kila moja wetu ajitahidi kuhudhuria hii siku ya Jumapili ambayo tutafanya uzinduzi. Ili kuhakikisha siku hii inakuwa ya tofauti, uongozi wa kanisa umemwalika Pastor ERICK MKWENDA pichani kutoka kanisa la Maranatha Arusha kuja kutuhudumia. Pastor Erick na mke wake Elisikia wamekuwa wakimtumkia Mungu sehemu mbali mbali ndani na nje ya Tanzania kwa miaka mingi sasa.Naomba kila moja atakae soma habari hii amjulishe mwenzake.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo:
Pastor Absalom Nasuwa: 214 554 7381
Nicholus Chove: 682 552 6402
Grace Kiango: 405 990 6441
Jesca Kataraihya: 214 773 6697
Tony Kaloki: 817 875 4764

Mungu ambariki kila moja wetu
Pastor Absalom Nasuwa
6411 LBJ Freeway
Dallas Tx,
75240-6406

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...