WAZIRI WA VIWANDA,BIASHARA NA MASOKO MH. CYRIL CHAMI AKIPATA MAELEZO YA BIDHAA MBALIMBALI KUTOKA KWA AFISA MASOKO WA TAASISI YA UTAFITI WA KIINJINIA NA MAENDELEO(TEMDO), BW. SIGSBERT MMASI MARA ALIPOFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA TAASISI HIYO KUANGALIA SHUGHULI ZAO MBALIMBALI.
WAZIRI CHAMI AKIPOKEA MAELEZO YA MASHINE YA KUKAMULIA MAWESE KUTOKA KWA MKURUGENZI WA TEMDO BW. KALUTU KOSHUMA ALIPOFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA TAAISISI HIYO ILIYOPO JIJINI ARUSHA.
WAZIRI CHAMI AKIPOKEA MAELEZO YA MASHINE YA KUKAMULIA MAWESE KUTOKA KWA AFISA MASOKO WA TAAISISI YA TEMDO BW. SIGSBERT MMASI ALIYE KUSHOTO KWAKE JANA ALIPOTEMBELEA KUANGALIA SHUGHULI MBALIMBALI NA DHANA ZINZOTENGENEZWA NA TAASISI HIYO.

HABARI NA PICHA NA WOINDE SHIZZA
WA GLOBU YA JAMII, ARUSHA

WAZIRI wa viwanda,biashara na masoko nchini,Cyril Chami jana alianza “kutema cheche” kwa kuwaambia watumishi wa idara mbalimbali katika wizara hiyo ya kuwa hatakuwa na msalie mtume kwa mtumishi yoyote ambaye ataonekana kulegalega katika utendaji wake wa kazi pamoja na wale wanaoendekeza tabia ya uvivu.


Alitoa karipio kali kwa watumishi wa wizara hiyo hususani wale wenye tabia ya kufarakanisha,wavivu pamoja na wale ambao huendekeza majungu na kuwatamkia ya kuwa ni vyema wakapisha mapema kabla ya kusubiri kuondolewa ama kufukuzwa.

“Kwa kweli wale watumishi ambao ni kikwazo cha maendeleo ndani ya wizara yetu, wenye kufarakanisha watu,wavivu na wanaopenda majungu huu sio muda wao naomnba watupishe sisi tufanye kazi”alisema Mh. Chami

Mh. Chami alitoa angalizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya siku moja jana jijini Arusha ambapo alitembelea taasisi ya utafiti wa kiinjia na maendeleo(TEMDO), Kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini(Camartec) sanjari na shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO) mkoani Arusha.

Akizungumza na wafanyakazi wa taasisi ya Utafiti wa Kiinjinia na Maendeleo(TEMDO) waziri Chami alisema kuwa watumishi hao hawana budi kuacha tabia ya uvivu ikiwa na badala yake kuwa wachapakazi hodari na wabunifu katika shughuli zao mbalimbali.

Aliuambia uongozi wa taasisi hiyo ya kuwa sasa ni muda wao kutangaza bidhaa zao ili kumudu soko la ushindani duniani kote huku akitoa ahadi ya serikali kuisadia taasisi hiyo kutangaza bidhaa zake.

Awali akitembelea kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini(Camartec), waziri huyo alishuhudia matrekta mbalimbali yanayotengenezwa katika kituo hicho huku akkiupongeza uongozi wa kituo hicho kwa kubuni mradi wa gesi ya kinyesi cha binadamu .

Waziri Chami alihitimisha ziara yake kwa kutembelea shirika la kuhudumia viwanda vidovidogo nchini(SIDO) mkoani Arusha ambapo alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa idara hiyo sanjari na uongozi wake ambapo alitoa pongezi kwa shirika hilo kwa kutoa mikopo mbalimbali kwa wajasiriamali wadogowadogo.

Naye mkurugenzi wa shirika hilo mkoani Arusha, Bw. Isdori Kayenze alimwambia wziri huyo ya kuwa pamoja na changamoto lukuki wanazokabiliana nazo lakini uongozi wake umefanikiwa kutoa jumla ya mikopo 156 kwa wajasiriamali wadogowadogo mkoani hapa yenye gharama ya sh,280,512 milioni kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka jana.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...