Nimegongana na hii video kule YouTube ikanikumbusha libeneke la waosha vinywa juu ya ung'eng'e wa kule Big Brother. Wadau wanaojua Kijapani, msaada tutani kama hii mistari imenyooka au ndo vile vile??
Home
Unlabelled
Kwikwi ya salamu za kufunga Mwaka kwa mdau wa Japani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Anajitahidi kwakweli, maana inaonyesha kakaa miaka 2 tu i guess mpaka hapo alipokuwa akiongea. Na pia kwa alivyojieleza kaoa mjapan. Kwa mtu ambaye si lugha yake yuko suppppaaaa!
ReplyDeleteKijapani kajitahidi saaana, anastahili sifa na pongezi, ila wangemwambia aanze na nashibota, wakora na kuchanganya kidogo na kimombo angeenda speed zaidi
ReplyDeleteMWasi uko juu kaka.
ReplyDeleteMdau Uk
wewe ulioleta hii issue whats your point? unachotaka ni nini? Naona lengo lao lote ni umbea tu, Grow up!!!
ReplyDeleteMwasi aminia sana, nimeipenda hii, Yaani bomba sana. Kamua mzee, haya mambo ndo tunahitaji, sio wabongo wanaenda nci za watu halafu wanapotea tu. Nimekukubali mzee.
ReplyDeleteNa mimi namshangaa sana aliyeleta hii post, anaonekana kama kakaa kidaku daku tu, ni ujinga, Kua kijana. Sio kukaa na kukosoa wenzako, sasa kama hujui alichoogea umeileta ya nini hapa. Wabongo mnafikiri Kiingereza tu ndo dili. Acheni ujinga.
ReplyDeleteMdau Netherlands.
KWA KWELI MWANA AMEJITAHIDI SANA KWA KIJAPAN, MAANA TUNA WENGINE HAPA MIAKA 15 HAWAWEZI KAMA HUYU BWANA MWASI ANAYOKIMWAGA KIJEPU ME NAMKUBALI SANA,SAFI MWANA. MDAU JAPENGA
ReplyDeleteBIG UP MKUU MWASI - MDAU UBATANI
ReplyDeleteGood job man!
ReplyDeleteHONGERA !!!Kuna watu kibao wamekaa hapa UK hata kakijisentensi kamoja ka english hawawezi kuandika,Kuongea ndo basi tena kazi yao kuwacheka wabongo walioko home kumbe wenyewe huku ni ZERO.
ReplyDeleteMdau wa UK
Mwasi,
ReplyDeleteBabu kubwa Ndugu yangu.. lazima nii peleke kwa Mwalimu Gora pale Chang'ombe Shule ya Mazoezi apate kuuona vijana wake walivyo jitahidi kuishi vizuri na watu.
Ung'eng'e wa Big Brother unamaanisha Kanumba??
ReplyDeleteHuyu kijana mbona anaongea vizuri tu hicho kijapani.
Ongeza juhudi zaidi kakangu.. utakijua tu fasaha zaidi kama wao.
...ahaa safiiiii..ebana nasubiria nije mwakani najua utanifunza sana kijepuuuu
ReplyDeleteHata nami nashangazwa sana na mleta hii post hususan maneno aliyoyatumia inaonyesha dhahiri ni mdaku wa hali ya juu. Dhamira yake yote ya kuileta hii post ni kutaka watu hapa wamcheke huyo jamaa katika video lakini ime backfire!
ReplyDeleteSafi sana, inatakiwa Watanzania waliopo ughaibuni wajifunze lugha za wenyeji wao kwa bidii na kasi zaidi, ili tuweze kuitangaza Tanzania kwa lugha zote ikiwa pamoja na kuvutia ubia wa kiuchumi kupitia utalii, viwanda, usafirishaji n.k kupitia teknohama na hafla kama hii huko Japan.
ReplyDeleteMdau
JeiKei
mdau alieleta post ni mjinga sana.yani unataka watu wakuambia kama jamaa anapatia wakati unaona wa japan wenyewe wanamuelewa?
ReplyDeleteget a life.
aliyeleta hii post atakuwa anatafuta pa kuficha sura yake.hakuna hata aliyemsapoti na UDAKU wake.sidhaki kama ushawahi kuwacheka/dhihaki wageni wanaoishi bongo huku kiswahili kikiwasumbua.hao wanamuziki wa kikongo na nyimbo zao za kiswahili mbona zinafagiliwa ingawa lugha imepinda?
ReplyDeleteGrow Up!!!!
cha msingi ni kwamba wenye lugha wanamuelewa, hiyo si lugha yake ya asili hivyo kinachotakiwa ni kueleweka tu
ReplyDeleteSikielewi alichokuwa anasema jamaa huyu lakini kwa kutumia tu akili yangu inaonekana jamaa ni mkali kijapani anakijuwa si mmeona mpaka wenyewe wanacheka kwa kuwa wameelewa anachosema big up do wewe wa japan
ReplyDeleteamajitahidi, unajua hata wazungu wakija bongo hawaogopi kuchekwa ndio maana within a short period wanakua wameshajua kiswahili. kuogopa kukosea ndio kunaturudisha nyuma. tusipende kuchekana bali kupeana moyo
ReplyDeleteKwa kweli sijui huyu kijana anaongea nini lakini hata kama anakosea kama mtuma post alivyoandika sioni cha ajabu. mi nafikiri ni kupungukiwa na mawazo kuanza kutafuta amechapia wapi...hakuna mtanzania aliyezaliwa akijua kijapan au kiingereza...wengi lugha hizi za kigeni ni za tatu au wengine ni za nne...sioni ajabu mtu akichapia. kwa kweli watanzania mnatia aibu...si ajabu hadi leo mkawa mnaongea lugha yenu ya taifa tu eti kwa kuogopa mtachapia...mawazo mgando kweli kweli...
ReplyDeleteNingependa niangalie post hii kwa jicho la tatu. wengi tumemlaumu aliyeleta post hii na kumwita mdaku n.k Wote tumesahau mwenye kura ya turufu ya kuaomua ni post gani iende hewani ni Bw. Michuzi mwenyewe, kama post ni ya kijinga basi ilitakiwa isipate mpenyo kwenye blogu...kinyume chake, imepata. Nafikiri ni kulemaa kwa mkito wa fikra za Bw. Michuzi, kama post ni ya kipuuzi, inayorudisha juhudi za watanzania kujifunza jinsi ya kushiriki vyema kwenye utandawazi, basi na isiwekwe...kama ningekuwa natakiwa kuipa kura blogu hii kwa hii post, ningeipokonya kura moja...Bw. Michuzi, tafadhali onyesha frika zilizokomaa.
ReplyDeleteNIMESIKILIZA SIJAELEWA KITU
ReplyDeleteKijana yuko juu ameongea vizuri mno, nimependa anavyozungusha vidole na mikono yake. waooo very nice.kwanza mcheki anavyopresent anavyoweka mikono na vidole vyake, anapendeza kweli.Pili anajiamini na anachokiongea watu wanamuitikia vizuri hawaguni.nimependa sana .Uncle asante kwa changamoto hii uliyotuletea wengine tujifunze,kupanuka kifikra na mtazamo. Kujifunza lugha za watu popote pale hata ukipostiwa kwenda umakondeni kikazi jitahidini kujifunza japo maneno wawili matatu. Nimepostiwa Dodoma lol.. kikazi walau najua maneno mawili matatu hivi ya KIGOGO.tehetehteht....
ReplyDelete