Lady Jay Dee akionesha maji ya kunywa ambayo yana jina lake yanayotolewa na Mohamed Enterprises Limited, akiwa ni msanii wa kwanza kupata endorsement ya aina hiyo nchini. Hafla hii imefanyika leo katika hoteli ya Paradise City jijini Dar. Akiongea na waandishi katika hafla hiyo Jay Dee pia aliweka wazi mipango yake kwa mwaka 2011 ikiwa ni pamoja na kufungua mgahawa uitwao 'Nyumbani Lounge' karibu na Best Bite Restaurant maeneo ya Ada Estate pamoja na kutoa albamu yake ya tano.
Mamodo Fide Ilanga (shoto) na Flaviana Matata wakiwa na maji ya Lady Jay Dee wakati wa uzinduzi wake leo
Lady Jay Dee na maji yake
Lady Jay Dee akiongea na waandishi. Shoto ni mumewe Gadna G Habash na Christine Mosha wa kampuni ya Rock Star
Jay Dee akifafanua mambo kwa waandishi
Jay Dee akiwa na marafiki zake waliofika
kwenye hafla hiyo. Chini ni video yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Kweli jay dee ni muhangaikaji Mungu azidi kukuinua hadi utimize malengo yako yote, Amen

    ReplyDelete
  2. Big up jidee hiyo ndio inatakiwa wanawake waige sio kutegemee mume,pia wasanii waige kwako.

    ReplyDelete
  3. Whoa....VERY IMPRESSING...GOOD JOB JAYDEE, KAZANA HIVYOHIVYO MUNGU ATAKUSAIDIA...ILA USHAURI WANGU TU NI KUWA, WEWE NA MUME WAKO ACHANENI NA MADAWA YA KICHINA (YA KUPUNGUZA MAFUTA) NA BADALA YAKE FANYENI MAZOEZI,....TUNAWATAKIA MAISHA MAREFU ILI MFAIDI MATUNDA YENU....YOU GUYS ARE WORKING REALLY HARD AND IT WILL PAY. ITATUUMA SANA KUSIKIA KUWA MNAPATA SIDE EFFECTS ZA DAWA ZA KICHINA (AMBAZO UMEKUWA UKIZIPIGIA DEBE KWENYE BLOG YAKO)..WACHINA SIYO WATU WAZURI HATA KIDOGO. JUST IMAGINE WALIVYOFANYA KWENYE MAZIWA YA WATOTO WACHANGA!!...ANYWAY, NDIYO HAYO TU...KEEP IT UP THOUGH !

    ReplyDelete
  4. That dude Gadna G. got quite impressive social skills.His answers are well structured and covers everything in a detailed way than espected.Congrats all.

    ReplyDelete
  5. Jamani Lady J d mbona huna class jamani self esteem ndogo, unashika shika nywele mara hereni si utulie dada? mara maji unakunywa unaegesha chupa ili usitoe lipstick jamani nani mshauri wako kjamani na nimemuona mume wako anakuangalia anatamani kukuuliza unafanya nini nadhani mume wako anajitahidi sana kujieleza na ana class sasa akufundishe.

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Jide. Mungu azidi kukubariki kwa moyo wako mwema na wa kujituma.

    Stay blessed.

    ReplyDelete
  7. well may be i'm just a hater but she should get another name for that water. i don't mind smelling her but not drinking her for the name sake??????
    how does that sound can i have lady jd please, no thank you i'm not thirsty. By law this is .passing off. there is JD liquor already exist. anyway it is TZ there is no property right i guess.

    ReplyDelete
  8. Me too not a hater here but just a word of advice. Next vacation she should take a public speech class and do a dental work. With all the money she makes, I am sure she could easily afford that just b'se Bongo millionaires don't know that to be a public figure comes with lot of responsibilities. You want people to trust you then have a confidence and on what you are selling..She needs a public relation who will guide her on what to say on each and every event. They will do a homework for her and she will be there just to say what they told her to say otherwise doing everything by herself is not good. She is not a superwoman so do all celebrities in the world. They appear in public with confidence and all the info on their hands ready but it takes a whole lot of pp to put that together. Is not a magic shot..They spend money to get money...Otherwise it will be like that all the time touching hair, biting nail, sikia lia cheka etc etc

    ReplyDelete
  9. Mhh those handbags like if they want to carry the whole kitchen sink..

    ReplyDelete
  10. Lady Jay Dee, ujumbe wako umenigusa sana. Hii falsafa kwamba maadam mtu umejaliwa mengi na jamii nawe urudishe fadhila kwa jamii ni falsafa ambayo inahitaji kufundishwa kwa watoto wetu.

    Ni tofauti na falsafa ya mafisadi wanaoimaliza nchi yetu, ambao wazo lao ni kuhamisha hata kile kidogo ambacho kingeweza kuleta nafuu fulani kwa watoto yatima, watoto wanaoshi katika mazingira magumu, wanaosoma kwa shida, wakulima wanaokosa pembejeo, wafanya kazi wenye maisha duni, wananchi wasio na ajira, na kadhalika.

    Mungu akubariki na kukuzidishia maisha marefu na mafanikio.

    ReplyDelete
  11. ASANTE SANA MICHUZI KUTUONYESHA MAMBO HAYA MI NI MDAU MTANZANIA NIPO SEOUL KIMSINGI NDUGU ZANGU WATANZANIA BADO TUNA WAKATI GUMU WA KUELEWA KUWA KUNA JAMBO MOJA MUHIMU SANA LIFANYIKE KUWEZA KUWAMAGE WANAMZIKI WETU GADNER AMEJITAHIDI KUMSAIDIA JAYDE SIO TU KAMA MUME WAKE LAKINI KAMA MENEJA WAKE KIMSINGI WASANII WETU WAFUNDISHWE KUWAPA NAFASI WATAALAM WANOWEZA KUMZUNGUMZA -AU LA KUJIFUNZA KUNZUNGUZA KATIKA WATU, SWALI LA MAJI YANOTOKA WAPI HALAFU JAY DEE ANAJIBU VISIMA BALAA

    ReplyDelete
  12. ushauri mwingi uliotolewa humu ni wa kumjenga zaidi lkn nina hakika haya yatapomfikia mlengwa majibu yake itakuwa ni HATERS ukweli nakwazika sana na neno hili hatukotayari kukosolewa, Jide hana comfidence wala convincing power ya kuniuzia hayo maji yake kwa kumsikiliza tu, ukiachia Jina ambalo sidhani kama walilifanyia utafiti kama litauza, kwenye biashara jina huuza zaidi kuliko bidhaa yenyewe,ndio maana wachina wanatuuzia majina makubwa kama LV, Nike, na mengine lkn fake nasi tumo tu kwa ajili ya jina. tusikurupuke, Gari aina ya Benz ilitengenezwa lkn haikupelekwa sokoni kwa miaka kadhaa wakitafuta jina, Mzee huyu wa kijerumani alikuwa na bint yake mrembo sana aliyeitwa Mercedes,aliwasiliana na wataalamu na kutaka kujua je akiita gari yake mercedez itauza? pamoja na uremboa alionao bint yake na shauku yake kuita hiyo gari mercedez lkn bado aliwaita ili wafanye utafiti kama jina hilo litauza, kwa bahati nzuri watalamu walikubali na alitumia pesa nyingi sana kuitangaza ile gari kabla haijatoka kwa mara ya kwanza na ilipotoka ilikuwa ni gumzo na mpaka sasa benz hata pekosi unatesa mjini,

    ReplyDelete
  13. NASHUKURU WOTE KWA MCHANGO WENU BUT MIMI NIKO TOFAUTI KIDOGO THOUGH JD NDIYE MJASIRIA MALI MKUU LAKIN HAIKUA SAHIHI KWA YEYE KUZUNGUMZIA CHOCHOTE, ANGE-DELIGATE EVERYTHING TO HER MANAGER USHIRIKI/UWEPO WAKE HAPO KWENYE HIGH TABLE ULIKUA UNATOSHA KABISA KUONYESHA YEYE NDIYE OWNER

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...