Na Mwandishi Wetu
Polisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo wamelazimika kutumia ujuzi wa ziada baada ya washtakiwa watatu wanaokabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha walipoamua kubaki uchi ndani ya Mahakama hiyo wakipinga kukamatwa tena baada ya kuachiwa huru.
Zogo hili lilizuka mnamo saa sita mchana baada ya Hakimu Mkazi Mh. Ritha Tarimo kuwaachia huru washtakiwa hao chini ya kifungu cha 225 (4) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA) cha mwaka 1985 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, inaruhusu mshtakiwa kukamatwa tena na askari polisi endapo wataona kuna sababu ya kufanya hivyo.
Hakimu Tarimo aliiwaachia huru washtakiwa hao, chini ya kifungu hicho , baada ya kutoa ahirisho la mwisho katika kesi hiyo iliyokuwa katika hatua ya usikilizwaji wa awali, baada ya Wakili wa Serikali, Leonard Chalo kudai kuwa hawana jalada la polisi la kesi hiyo.
Baada ya washtakiwa hao kuachiwa huru, askari walitanda nje ya mahakama hiyo kwa lengo la kuwakamata. Ndipo washtakiwa hao walipostukia dili wakaamua kuvua nguo kupinga kukamatwa kwao tena.
Askari hao walianza kuwalazimisha wavae nguo , lakini washtakiwa waligoma kata kata kuvaa nguo zao huku wakilia na kupiga kelele, wakisema jela kuna hali mbaya na hawataki kurudi tena huko.
Ikabidi askari polisi kama 20 hivi waje kuwadhibiti kwa kuwafunga pingu na baadaye kuwakokota kwa nguvu huku wakiwa uchi hadi Mahabusu ya mahakamani hapo.
Washtakiwa hao waliovua nguo ni Samuel Joseph, Said Zacharia na Said Idd ambao wote kwa pamoja walikuwa wanakabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha namba 184 ya mwaka 2010.
Katika kesi hiyo, wanadaiwa kuwa Juni 4, mwaka huu , saa 9:00 jioni huko maeneo ya Mchikichini waliiba vitu mbalimbali vikiwemo simu mbili za mkononi aina ya Sumung na Nokia pamoja na nyaraka tofauti tofauti vyote vikiwa na thamani ya Sh 467,000 mali ya David Mkombozi.
Ilidaiwa kuwa kabla ya kufanya wizi huo, walimjeruhi Mkombozi kwa kumkatakata kichwani kwa Panga ili waweze kujipatia vitu hivyo kwa urahisi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...