Mpendwa Mjomba Michuzi,Habari za kazi Mjomba, nimevutiwa sana na picha hii ambayo mama mmoja aliyekuwa anakatiza mitaa ya Tukuyu mjini mchana huu maeneo ya Stendi kuu akiwa amembeba kuku Jogoo mithili ya mtoto mgongoni kwa kumfunga kwa mbeleko. Hii inaonesha ni jinsi gani mama huyu anawajali viumbe vingine. Sifa tele kwake na wengine tuige.
Wasalaam,
Mjomba Juma, Tukuyu


Hakuna upendo ni kitoweo tu hicho babake
ReplyDeleteduh watu weusi vituko !!
ReplyDeletewe unayesema watu weusi vituko, je wale wenye rangi nyingine hujasikia vituko vyao?
ReplyDelete1. kulala na mbwa
2. kulamba kinyeo na kazalika.
huyo mama kabeba kuku kurahishisha mambo badala ya kumning'iniza kichwa chini - kwanza inachosha mikono na (sijui kama alikuwa anawazia haki za wanyama) lakini kampa nafuu kubwa sana huyo jogoo
mmm...nievunjika mbavu.....kweli blogg inatupa rahaa....na aliyesema watu weusi vituko...kanimaliza.....kweli sis mwisho......
ReplyDeletesasa wewe unasema eti tuige mfano wa huyu mama, yaani badala ya kuwasafirisha kuku kwenye tenga eti tuwabebe mgongoni, hata enzi ya kuwabeba watoto migongoni ilishapitwa na wakati eti wewe bado unaongelea kuku, haki za binadamu bado ni ndoto kwa nchi nyingi duniani ati wewe bado unaongelea haki za kuku ahahahaaa!!!
ReplyDeleteUnaweza kabisa kumuona huyo Jogoo amepitiwa na Ka-Usingizi kidogo kwa Raha ya kubebwa. Bi Mkubwa Hongera.
ReplyDeleteWewe unaongelea haki za wanyama, huyu mama hajui hata haki yake ni nini. Hapo amerahisisha tu kwa ajili tayari mkononi ameshikilia hicho chungu. Huyu kuku amechinjwa baada ya masaa kadhaa kwa hiyo mada yako ya haki za wanyama hapa si kweli.
ReplyDeleteHayo macho yako! Sio jogoo huyo, angalia vizuri. Huko ndo kwa wachuna ngozi, kama hujui!
ReplyDelete