Wachezaji na mashabiki wa timu ya soka kutoka mkoa wa Tanga wakifurahia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga timu ya Mkoa wa Dodoma kwa magoli 2 kwa 1 katika michuano ya michezo ya UMITASHUMTA inayoendelea katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, Mkoani Pwani.
Nahodha wa timu ya Mpira wa Pete kutoka Mkoa wa Dar es salaam Anitha Masanja akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya timu yake kuifunga timu ya Mkoa wa Tanga kwa magoli
18 kwa 13 katika michezo ya UMITASHUMTA inayoendelea katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.
Mratibu wa Taifa wa Mashindano ya UMITASHUMTA bwana Lawrence Madege akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua iliyofikiwa kwa michezo ya UMITASHUMTA ambapo alisema kuwa mwaka huu mashindano hayo pia yalishirikisha michezo > kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...