Baada ya kutoka mkoani Arusha katika shughuli za Jamii, Warembo wa Miss Tanzania leo hii wamewasili mjini Moshi Kilimanjaro na kuendelea kutoa misaada katika vituo viwili vya Kao la Amani centre, pamoja na kituo cha Fountain Zoe vyote vipo eneo la Bomang'ombe nje kidogo ya mji wa moshi. Pichani juu ni Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel [kati] mrembo wa Kanda ya Ziwa Buduri Ibrahim [kulia] pamoja mrembo wa Kanda za nyanda ya juu kusini, Furaha David [kushoto] wakiwa wamebeba watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Fontain Zoe kilichopo Bomang'ombe nje kidogo ya mji wa Moshi. Warembo hao pamoja na wengine wapo katika shughuli za jamii katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, ambapo pamoja na shughuli zingine walikabidhi vifaa mbalimbali kama vile vyakula, vyandarua, sabuni, mafuta ya kupikia kwa kituo hicho ambacho pia kinalea watoto wachanga kabisa, ambao wazazi wao wamewatupa au kufariki.
Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel akikabidhi misaada mbalimbali kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Fontain Zoe mama Grace Shoo mara baada ya kutembelea kituo hicho. ujumbe wa Kamati ya Miss Tanzania ulipewa mavazi maalum kabla ya kuingia katika kituo hicho ambacho pia hutunza na kulea watoto wachanga kabisa wa umri wa siku moja na kuendelea.
Juu na chini misaada ikigawiwa kwa watoto yatima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...