Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akipewa maelezo na wataalamu kuhusu upatikanaji wa makaa ya mawe na uwezekano wa kuzalisha nishati ya umeme katika eneo la Ngaka, Wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara. Mh, Lazaro Nyalandu akipewa maelezo ya hali halisi ya mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka uliopo Mbinga mkoani Ruvuma. Wanaotoa Maelekezo ni waratibu wa Mradi huo.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akikagua mojawapo ya maeneo ambapo utafiti unaendelea kufanyika kuhusu upatikanaji wa makaa yam awe katika eneo la Ngaka, Mbinga, Ruvuma. Wengine ni maafisa kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa NDC, watafiti na waandishi wa Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hongera sana Baba wa Taifa kuhifadhi mali asili zetu. Maamuzi ya kuzuia wezi na mafisadi kuvuna chuma na makaa ya mawe ulikuwa wa muhimu sana sana, leo tungekuwa na mashimo kama ilivyo Buzwagi. Mh Nyalandu na Dr Chami, shirikianeni na Ngeleja, huo umeme upatikane haraka

    ReplyDelete
  2. Huu sasa ni wakati wa kuweka siasa pembeni,tufanye mambo kitaalamu kabisa.Tuvune hayo madini ya chuma na Makaa ya Mawe, tupate umeme na faida nyingine kama ajira, maboresho ya miundombinu, huduma za jamii nk. Hivi kumbe NDC ipo hai? Dr Chami na Nyalandu, chonde chonde shirikianeni kuleta mabadiliko. Taarifa zitoke kwa wingi, naamini hayo mambo hayahitaji kuwa siri tena katika karne hii

    ReplyDelete
  3. Ndc ni shirika lenye majukumu mazito ya kufanikisha mihakato ya nchi kupiga hatua za maendeleo, cha ajabu ni kuwa shirika lipo kimya ziiiiiiiiiii kama halipo. Hongera msafara wa Nyalandu kwa kutujulisha yalkiyojiri huko na hali ilivyo, jitahidini kujitangaza zaidi ili wawekezaji wafahamu, labda watavutiwa na hazina hizo na kuja kuwekeza..

    ReplyDelete
  4. Tatizo Tanzania kila kitu ni SIRI. watu wanafanya mambo makubwa lakini wanafanya kimya kimya ndio maana mara zote serikali inaonekana kuwa ya HOVYO. Nguvu ya habari ni kubwa sana katika dunia ya leo, kampuni na biashara zote zenye mafanikio zimefika zilipo kwa kutoa taarifa na kujitangaza. Vodacom, Zain, Tigo na nyingine, wanajulikana vya kutosha lakini muda wote wapo hewani kupitia matangazo na taarifa mbali mali. NDC na Wizara ya Viwanda, na Wizara ya Nishati na Madini, JITANGAZENI, TANGAZENI NA MAMBO KAMA HAYA YA LIGANGA NA MCHUCHUMA...

    ReplyDelete
  5. Maeneo yenye rasilimali kama hizo huwa ni kichaka cha mafisadi na wezi. Waziri na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ni watu mnaoaminika. Kuweni makini na watendaji walio chini yenu, kwa nini taarifa hizi za rasilimali za Taifa zinakuwa za siri? Kuna tatizo kubwa

    ReplyDelete
  6. Ni gud news kwa nchi kuwa na rasilimali kama madini lakini tusiwasahau wenyeji wa maeneo hayo. wapeni fidia, waondoeni katika maeneo hayo kwa njia bora za makubaliano. Serikali kuweni makini, miradi kama hiyo ni kichaka
    cha ufisadi

    ReplyDelete
  7. Kwa hali halisi ya nchi ilivyo hivi sasa, Umeme ni tatizo kubwa sana. Mi nashauri kuwa ni vyema zikachukuliwa hatua za haraka kuzalisha umeme kwa kutumia hayo makaa ya mawe. Haina logic kuendelea kulalamikia bei kubwa ya umeme na kuutaja umeme kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi wakati suluhisho lipo.

    ReplyDelete
  8. Tatizo kubwa la watanzania ni ufisadi. Makaa ya Mawe, gesi asilia na rasilimali nyingine kibao hazitumiki kwa kuwa bado channel za kuwanufaisha mafisadi hazijawekwa sawa. Hilo shirika la NDC ni mfu kabisa, halisikiki, halijulikani majukumu yake, hata kama mazuri yapo, ni wazi kuwa na madudu pia yapo. Mh Nyalandu tunataka tuone UZALENDO WAKO, kama ni nguvu ya soda, hukumu yako 2015

    ReplyDelete
  9. Wizi mtupu nchi hii, mpaka tunaambiwa kuwa tuna hazina kubwa kama hizo basi ujue wajanja wameshavuna mpaka wamechoka. Haiingii aklini kuona nchi imo katika tatizo kubwa la NISHATI then kuna posibilities za kusolve tatizo. MH JK hebu wape maagizo hawa vijana wako NGELEJA NA MALIMA waache usanii, washirikiane na wenzao akina NYALANDU huo umeme upatikane. Tungefurahi pia kupata full report mtandaoni, Mainjinia si wapo huko Wizarani? Watupe ripoti, tuwe na mjadala wa pamoja.

    ReplyDelete
  10. Nyalandu achana na makaa ya mawe, hangaikia kwanza viwanda vyako vinavyokufa. Najua viwanda vinahitaji sana malighafi na nishati ya umeme lakini huko kwenye nishati si yupo Ngeleja? Mwache aendelee kulala, umma utamuamsha na atajikuta si Waziri wala mbunge. Wewe fufua viwanda. pambana na bidhaa feki, tafuta masoko ya bidhaa zetu na fursa za biashara kimaaifa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...