Mwanamitindo wa Kimataifa,Flaviana Matata akiwa na zawadi ya ua alilopewa na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha TMH wakati alipo wasili katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere mchana wa leo akitokea nchini Marekani.
Watoto wa Kituo cha THM wakimpatia zawadi ya ua Mwanamitindo Flaviana Matata aliewasili leo nchini akitokea Marekani.
Wadau wa Mitindo Nchini toka TMH wakiwa katika picha ya pamoja na Flaviana Matata pamoja na Watoto wanaolelewa katika kituo cha TMH nje ya uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Karibu nyumbani dada yetu Flavian......mmoja wa Watanzania wachache maarufu duniani wanaojua na kuelewa maana ya uzalendo. Tunajua ulikuwa na uwezo wa kwenda mapumzikoni sehemu yeyote maarufu hapa duniani, lakini kitengo cha wewe kuamua kuja nyumbani ni cha kuigwa na Watanzania wengine waliolowea ughaibuni. Vilevile nikupongeze kwa jitahada zako za kusaidia watoto yatima. Karibu nyumbani na ujisikie uko nyumbani. Nimefarijika mno!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...