Ankal,
Pole na majukumu na asante kwa kutupa updates...
ninapoandika warakaa huu ankal mpaka machozi yananitoka nimefikiria mahali pa kuyasema haya matatito yanayojitokeza nkaona bora niyafikishe kwako.
Kilio changu ni huduma mbovu hapo Muhimbili kwenye kituo cha walioathirika na maambukizi ya Ukimwi, kwa kweli huduma iliyopo hapo ni mbaya sana isitoshe na majibu yao hayaridhishi hata kidogo.

kama utakuwa na nafasi naweza kukuonesha mgonjwa wangu wewe kwa macho tu hata kama si daktari utaweza kutabiri kama kweli huyu mgonjwa anaweza kuwa naCD4 NGAPI? LAKINI CHA AJABU PALE MUHIMBILI KILA TUKIFANYA VIPIMO TUNAPEWA TAREHE YA MBALI KUJA KUFUATA MAJIBU NA TUKIJA TUNAAMBIWA FAILI HALIONEKANI!

Sasa ni mara ya 3 bado tunapima tu na majibu ya leo ndo ilikuwa funga kazi maana si alipochikuliwa vipimo vilikuwa vingi majibu tunayopewa leo ni ya CD4 count tu tena tunahisi ni ya kubuni maana hayaendani na uhalisia wenyewa na file halionekani tukijaribu kuwauliza ma nurse majibu yao yanakatisha tamaa!na wanakuambia kwa jeuri huyo mgonjwa wako akiwa anakohoa afunge mdomo wake sasa maskini mgonjwa mwenyewe hiyo nguvu ya kufunga mdomo hana na sisi tulienae hatujui muda gani atakohoa tungeweza kumsaidia kuufunga maana ni kero kwa manurse mgonjwa wetu akikohoa...

Ankali michizi roho inauma sana hasa pale RAIS wetu aliposema watu wajitokeze kupima, dawa zipo na huduma ni nzuri lakini sidhani kama yeye binafsi au WAZIRI wa Afya anahabari na kinachoendelea pale maana hizo dawa zote mabazo ni za bei kubwa unaambiwa ukanunue pharmacy pale unaambulia septrine tu....Ankali tumechoka sasa tunataka tujaribu kituo kingine cha Afya lkn Muhimbili pametushinda!

Salaam zangu ni hizo,
km utaweza kuzifikisha panapohusika tutashukuru...

Wasalaam Auty Yanina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Serikali yetu kwa kweli "ZILONGWA MBALI ZITENDWA MBALI"

    ReplyDelete
  2. naomba umwahishe kwa Dr Katondo 0652960055 ili ku-rise Cd4, kama hakuna mabadiliko utarushiwa pesa yako asante.

    ReplyDelete
  3. pole sana ndugu yangu yaani hao wamekalia rushwa tu ndio wanayoona ya msingi

    ReplyDelete
  4. Jamani na hii muhimbili(hospitali ya taifa)kwa nini inakuwa na matatizo na huu uozo wa huduma mbaya usioisha???kila siku matatizo na huduma mbovu,dharau kwa wagonjwa !!je??wizara husika au viongozi serikalini tuseme hawayasikii haya ???kwa kweli inachefua sana kusikia matatizo na bugudha za manesi na madaktari kila siku.Tunaomba viongozi katika wizara ya afya wafuatilie swala hili kwa karibu na ikibidi hao manesi wenye dharau kwa wagonjwa waripotiwe haraka na ikibidi wawajibishwe.Tunalalamikia ufisadi sana na huu pia naona ni aina ya unyanyasaji na kiburi kilichopo kwa baadhi ya maanesi na madaktari muhimbili.tumechoshwa saana.
    mtoa maioni Dar.

    ReplyDelete
  5. ple sana kaka , mi nahisi wewe unajua hali halisi ya bongo kama hukutoa hela a.k.a rushwa hakuna kitakachoenda, lakini ukifanya hata mgonjwa wako watambembleza na kumpuliza otherwise utachukia madokta bure na manes/ pole sana nchi yetu haiendi bila rushwa

    ReplyDelete
  6. Pole sana dada kwa kero hiyo. Binafsi nakushauri uende kwenye kituo kingine kinachotoa huduma za watu wanaoishi na VVU na kuugua UKIMWI.
    Muhimbili naelewa wameelemewa na wagonjwa wengi ukijumlisha na tabia kwa ujumla.
    Kwa faida yako na wengine, wagonjwa hawa hupewa dawa ya septrin kama kinga ya magonjwa nyemelezi, halafu kama ana dalili za magonjwa mengine hupewa dawa nyingine.
    Majibu ya CD4 yakitoka pia na kuonesha kuwa anapaswa kuanza dawa, itampasa kupewa ushauri mara tatu kabla ya kuanza matumizi ya dawa kwani dawa hizi ni za kumeza kila siku iendayo kwa Mungu!
    Pole sana usikate tamaa, jaribu kwingine pia kwa huduma bora!

    ReplyDelete
  7. Maisha bora kwa kila Mtanzania. Jana kulikuwa na mdau akilalamikia Benki, juzi uchafu Sinza, leo huduma Muhimbili. Tutaona mengi mwaka ujao.

    ReplyDelete
  8. Mtoa maoni anayesema kwamba viongozi wa Wizara ya Afya washughulikie anacheza na nadhani anaota, au haijui Bongo!!. Unawajua viongozi wa Wizara au unawasikia??? Ni ukweli ulio mchungu kuumeza lakini aliyeleta malalamiko nampa pole lakini kilio chake ni kama tone la chozi katika maji ya bahari - atalalama tu na hakuna lolote litakalofanyika na Muhimbili itaendelea kuwepo kama Hospitali ya Taifa.Kama hana fedha za kutoa rushwa au kumpeleka mgonjwa katika hospitali za binafsi (FEDHA) asitegemee matokeo mazuri kutoka hapo alipo. Tena wakimgudnua kwamba ndiye aliyeleta malalamiko haya hapa, hali itakuwa mbaya zaidi. KELELE ZA MPANGAJI HAZIMZUII MWENYE NYUMBA KUNYWA MAJI

    ReplyDelete
  9. Mimi nitakusaidia mawazo wewe na wengine wote wanaotaka kupandisha CD4 zao. Tumia diet hii hapa kwa muda na wengi imewasaidia maana lishe nayo hupandisha CD4.

    1. Mgonjwa akiamka tu mpe chai ya mlonge uliokaushwa, unauzwa hapo hapo Muhimbili au karibu na CBE kuna kontena pembeni wanauza mboga nmboga kavu. Chukua kijiko kidogo cha chai tumia mkono wa hicho kijiko kupata kiasi kidogo cha mlonge, tia kwenye kikombe kisha weka maji ya moto kama unatengeneza chai, acha kwa muda ikolee kisha mpe anywe.

    2. Baada ya hapo mpe kifungua kinywa chenye virutubisho kama uji wa lishe au vyovyote uwezavyo lakini vizuri mpe mgonjwa uji wenye virutubisho vyote, kama anaweza ulezi sawa kama hawezi mpe wa mtama uliochanganywa na unga wa soya.

    3. Ikifika saa tano asubuhi waweza kumpa supu yoyote ya mboga mboga yaweza kuwa mchicha, spinach, karoti au hata viazi na karoti na hoho, ikiiva kabla ya kuipua weka mlonge kijiko kidogo cha chakula kwenye hiyo supu, mpe mgonjwa anywe.

    4. Saa sita asubuhi mpe juice ya ubuyu, tafuta ubuyu safi ambao haujafunguliwa maana huu una virutubisho vingi, ukikosa basi tumia huo huo wa sokoni Kariakoo. Na kama hawezi ubuyu basi mpe juice yoyote ile fresh iwe ya mboga au matunda mfano nyanya, embe, passion au tunda lolote lile, usichanganye matunda na isikae muda mrefu inatengenezwa na kunywa hapo hapo. Unapoiblend weka mlonge kidogo kwa kutumia ncha ya kijiko cha chai kwa glass moja ya juice. Waweza kumpa pia juice ya Rozella kama unaweza kununua utaipata hapo au Kariakoo sokoni wanaita Choya, hii mpe kila siku glass ndogo 2 au 3 yaani asubuhi mchana na jioni.

    5. Mchana mpe ugali usiokobolewa na kama hutaweza kupata huo unga basi mpe ugali wa sembe lakini changanya unga wa ugali pamoja na unga wa soya wakati wa kupika. Angalizo usimpe nyama nyekundu kwa kuwa mfumo wa mgonjwa hauna nguvu ya kusaga nyama nyekundu, tumia nyama nyeupe au dengu au maharage na jamii zake kama njegere. Choroko ni high protein waweza kusiotesha kisha kimea chake ukachanganya kwenye supu yake au ukampikia zenyewe tu kama mboga.
    Kwenye mlo wake uwe na mboga yoyote ya majani kama matembele, bamia, mnafu, au spinach, ukikosa hata mchicha utasadia.

    6. Mpe mgonjwa snack baina ya mlo wa mchana na jioni na hakikisha mlo wa jioni anaupata mapema masaa 3 kabla hajalala. Na kwenye mboga uwe unamwekea mlonge vile vile.

    Kisha uwe unampa kijiko kikubwa cha asali na haba soda au asali na mdalasini. Usimpe mgonjwa chai wala kahawa kwa kipindi hicho unachompa hiyo diet.

    Fuata huo mpangilio bila kukosa kwa muda wa wiki 2 mfululizo. Kisha nitumie majibu hapa kwa Michuzi ili nikuongezee vitu kutokana na maendeleo ya mgonjwa. Lakini wakati unafanya hayo endelea na matibabu kama kawaida hospitali kwani hiyo hapo juu ni mlo tu na si tiba.

    Subira

    ReplyDelete
  10. pole sana ndugu yangu kwa yote hayo.Nadhani wanasiasa wengi akiwemo raisi wanasera nzuri sana lakini tatizo kubwa ni ufuatiliaji,huu ni ugonjwa au ukoma kwa serikali yetu,wafuatiliaji hakuna.viongozi wetu wanaweka posho mbele,kama kungekuwa na posho ya ufuatiliaji basi tanzania ingekuwa nchi mojawapo duniani kwa kutoa misaada badala ya kupokea.tunahitaji viongozi kama Mama Tibaijuka,jinsi anavyofuatilia mambo,kwa hiyo tunahitaji mtu kama huyu wizara ya AFYA maanake imeoza hakuna mfano,hasa ukiwa mlalahoi ndiyo basi tena.Wizara ya ofyo haifai,wanatahabika ni walalahoi.

    ReplyDelete
  11. mATATIZO YA VIONGOZI WETU BONGO,WAKATI WA UCHAGIZI WALIKUWA NA MIDOMO MITAMU,SASA WAMESHA CHAGULIWA,SHIDA YAO IMEISHA NA LIBENEKE LA SHIDA KWA WAAAAAAANANCHI NI KAMA KAZI !!!KANGA,VITENGE,KILO ZA SUKARI MLIZOHONGWA ZIMEKWISHA NA WAO WAMESHINDA SHIDA PALE PALE,HAKUNA WA KUMLAUMU MLIYATAKA WENYEWE,MUHIMBILI NI JAHANAMU !!!
    RUSHWA KWA KWENDA MBELE !!!
    OMAR CHUWA,DAR.

    ReplyDelete
  12. using'ang'anie muhimbili bila sababu, hiyo huduma inatolewa hata ktk hospitali za pembezoni na fastafasta, vipimo na dawa ni zile zile, huko umekimbilia msongamano na matatizo.

    ReplyDelete
  13. Wakirekebisha katiba waseme Viongozi wote wa serikali na familia zao watibiwe katika hospitali za serikali. Iwe lazima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...