Ankal pole na majukumu.
Ndugu wadau nihitaji msaada wenu katika hili; Kwa sasa niko masomoni Algeria. Lugha inayotumika kufundishia ni Kifaransa. Kwa bahati mbaya Lugha inayotumika nje ya darasa(yaani, mtaani) ni kiarabu.

Kama mnavyo fahamu, ili uweze kuelewa mambo mengi huna budi kuwa mahiri wa lugha. Kusemaukweli level yangu ya Kifaransa bado ni ya chini, nahitaji kuimprove haraka iwezekanavyo. Nimepanga kwenda France Summer ijayo, na sina mtu yeyote ninayemfahamu huko. Kwa heshima na taadhima ninaomba Mtanzania yeyote anayeishi France kama ataweza kuniaccomodate angalau kwa wiki 6, tuwasiliane.
Natamani sana kuongea Kifaransa fluently.

Tafathali niandikie kupitia anuani hii;
frenchboytanzania@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Rudi Tanzania unafikiri lugha unajua siku mbili tatu?? hata ukienda huko utajua cha kuongea basi ila cha kuelewa masomo ni kigumu kaka ina bidi ujiandae kwa lugha miaka 2 hivi au mmoja ndio uwe fiti kwa darasa, rudi Tanzania tuu kaka usome kwa kiswahili.

    ReplyDelete
  2. sasa wewe unaenda ufaransa,shule si itakuwa imekupa pesa za accomodation?acha ubahili bana panga hotel then uyo rafiki atakua anakuja hapo hotel au wewe ukawa unakwenda kumtembelea.msipende kubebeshana mizigo isio na maana.unakwenda sama france inamaana chuo kimekupa kila kitu sasa iweje utake mtu akupe accomodation?

    ReplyDelete
  3. Algeria wanazungumza kifaransa, tafuta wanafunzi wa nchi za 'francophone'(kama Guinea, Cote D'ivore, Congo Brazza/DRC, Comoro n.k) wawe ndiyo marafiki zako hapo chuoni, usiwe kutwa unashinda na 'waswahili' wenzio tu huku mnazungumza kiswahili ka vile mpo Kariakoo.

    Pia wewe na waswahili wenzio mfanye uamuzi mgumu wa kuzungumza kifaransa wakati wote hapo chuoni. Hiyo safari yako Ufaransa uende baadaye sana kujipima kama kweli unakimanya Kifaransa cha Paris.

    ReplyDelete
  4. Nakushauri uagize audio cassete/dvd/cd za BBC zinazotoa maelekezo za kiingereza kufundishia kifaransa. Ziko clear kabisa na zina exercise za kukufanya uweze kuongea na kuandika kifaransa. Zimewasaidia watu wengi sana. Penye nia pana njia.

    ReplyDelete
  5. Anon wa kwanza kama huna ushauri wa kutoa bora unyamaze. Si lazima u-comment kama huna kitu cha maana cha kusema. Ni kama mtu amekuuliza "mbili na mbili ni ngapi?" halafu wewe ukamjibu "karanga".

    ReplyDelete
  6. Waandikie ubalozi wa Tanzania Paris. Mara nyingi kuna watu wanakuja TZ likizo June-July- August na wanatafuta watu wa kukaa katika vyumba au fleti zao. Najua hilo maana nilikuwa Paris nasoma kwa miaka mitatu na nusu. All the best.

    ReplyDelete
  7. Ndg yangu rudi bongo kajiandae na lugha yalinikuta mm nilipoenda germany nilishindwa kabisa kusoma ,nilirudi home na kujifunza lugha kwa miaka miaka miwili dear wangu ndio angalau naweza elewa itakumbua sana lugha

    ReplyDelete
  8. Spear your money ...huwezi kwenda kwa week sita na kuelewa kitu...Kam una hea chukua hii software hapa itakusaidia sana lakini inauzwa doal $600 http://www.rosettastone.com/holqb3?pc=sehol10&cid=se-gg&gclid=CPjs8Lm_0aUCFcfe4AodOl4Xlw

    ReplyDelete
  9. Nenda France lakini usifikie kwa wabongo wenzio haitakusaidia utaishia kuongea kiswahili na kula ugali tu. Ninachokushari nenda ubalozi wa France hapo Algeria wakuunganishe na programme za kujifunza lugha kwa kuishi na familia za kifaransa tena nje ya Paris, ukirudi huko baada ya wiki sita utakuwa umeambua, maana huko hakuna kiswahili wala kiinglishi utakuwa forced kuwasiliana kwa kifaransa. Pia soma vitabu na uangalie sinema za kifaransa kwa sana, wakwepe wabongo wenzio hapo Algeria hii itakuforce kujua lugha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...