Home
Unlabelled
Mshindi wa Kili Bongo Star Search 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Majaji wa BBS mbona mlionyesha utoto na mzaha katika fainali?
ReplyDeleteMaster J na Salma huyu mzungu kushiriki katika BBS mlikuwa hampendi,mlionyesha ubaguzu wa hali ya juu,ambao kwa wa TZ haupo kabisa
Master J. kumlinganisha huyo mshiriki wa kizungu na mlinzi wako wa nyumbani si ustaarabu.Tujulishe kiwango chako cha elimu.
ReplyDeleteSalma hukuwa pale kulinganisha wanamuzki waliyokuwa nje ya mashindano na hao wa BBS, kwa kuwaponda wana taarabu wengine
ReplyDeleteMaster J kauli zako hazikuwa njema kabisa. Kwa sasa BSS yanakuwa ni mashindano makubwa yanayotegemea kuvuta mashabiki wengi, kama umeamua kumponda mshiriki, usitumie ubaguzi wa wazi na kuishia kuita washabiki washamba.....That was very low and cheap of you...
ReplyDeleteNext time fanyieni kwenye Theater. Ukumbi umekaa kiholela holela. Watu wanatembea tembea ovyo utafikiri bar.
ReplyDeletekwa kweli BSS mwaka huu mmemaliza vibaya sana, angalieni mashindano ya wengine kama huwa wanaponda hivyo washiriki siku ya fainali. kama ushindi ni wa kura basi jaji anatoa pointi then anawaachia wapiga kura bt sio kwa kuwaita wapiga kura washamba! yaani nyie majaji ndio mmeonekana washamba kwa kudhani uzungu ndio unasababisha mtu apigiwe kura, bali watanzania wamempigia kura coz alikuwa anashiriki vzr na kutuburudisha watz. Madame Rita ukiendelea hivyo na BSS hupati tena mashabiki manake inaboa majaji kuongea hovyo hovyo kama walevi!
ReplyDeleteNami nakubalina na waliyotoa maoni,mshindi anatokana na kura,majaji mliifanya fainali ya kitoto au ushamba,hata mbele ya waziri milonyesha kuwa mashindano hayo yana kasoro,muwe mnaangalia wenzenu Kenya Nigeria nk.
ReplyDeleteMariam alitoa show ya nguvu..congrats,you deserved it..hope utatumia hela zako wisely..all the best dear
ReplyDeleteMbona comments za majaji ni za ki racist? majaji wenyewe wachovu, hawana points za maana zaidi ya chuki....ushamba mtupu. Na hao ma director wa ITV wamekaa to watch this and allow it to be aired...bongo bado sana. This is the first time am watching this and never will in the future. Najua Michuzi hutoi hii lakini huo ndo ukweli.
ReplyDeletejamani nyie majaji, naomba niulize huyo mzungu mlipo muweka kwenye hayo mashindano mlitegemea nini? mjue watanzania hawapendi ubaguz, mtu aonewe wala kudharauliwa na nyie majaji mmeonyesha hayo kwa Huyo mzungu ambae nyie mlimuingiza kwenye hayo mashindano na baadae mmoja wenu anamlinganisha na mlinzi wake haipendezi kwa kifupi imetuuzi sana iyo kauli. Next time rekebisheni kasoro zote zilizo jitokeza mwaka huu.
ReplyDeleteMaoni yangu hapa si nani alistahili kushinda. Bali, Kwanza nashangazwa na haya yaliyoibuka ghafla katika kupata washindi. Aibu tupu.
ReplyDeleteTangu awali tulikuwa tunahamasishwa tutume sms zetu, kwamba yule mwenye kura nyingi ndo ataendelea, na atakayepata kura nyingi hadi mwisho ndiye mshindi. Sambamba na haya ndiyo maana wengine walianza kudrop njiani tokana na kukosa kura nyingi.
Nakumbuka hata wakati mashindano yakiendelea siku ile, MC GG (au Godwin Gondwe) alikuwa anahamasisha watu kuendelea kupiga kura kwa kutuma sms. Sasa hayo ya uraia, nk yametoka wapi.
Haya mambo ndiyo yanatupelekea kuingia katika migogoro hata pengine kulazimika kulipa fidia kwa watu/makampuni tokana na kutengua mambo bila utaratibu. Rejea fukuto la Dowans sasa.
Mambo haya ya utatanishi yalianza kujitokeza ndani ya ukumbi, kila kijana wa watu alipokuwa akiingia, majaji mlikuwa mkimkandia ile mbaya, tena bila aibu. Na kilichonisikitisha na kuniudhi jamani ni pale Master J alipotuita WASHAMABA live dunia nzima ikiangalia!! Anasahau kuwa washamba ni wao ndio waliohadaika kumchagua Pyne kuingia kwenye BSS. Kwani hamkujua kuwa Joseph ni mzungu? Nani alipiga simu au kutoa tamko Pyne aingizwe kwenye kinyang'anyiro. Ni ninyi majaji ndio mlikubali uwezo wake. Halafu leo mnaleta mambo ya UBAGUZI. Hamkuyajua hayo tangu mwanzo? Hatari sana hii. Mnabagua nini, wote ninyi Washamba vile vile ndiyo maana mlitetemeka mlipoona ngozi nyeupe mkamteua.
Yote tisa, kumi ni kitendo cha kuwaita watu washamba kwa ajili ya kumshabikia mtu ambaye ninyi ndo mlimleta mbele za watu si cha kiungwana, kinastahili kukemewa na isitoshe, mnatakiwa kutuomba radhi kwa kututukana kuwa Sisi ni washamba tunamfurahia mzungu kwa kuwa ni mzungu. Master J, ulipomchagua alikuwa mwafrika? Wewe si ulishiriki tangu mwanzo, kipengere hadi kipengere. Nakumbuka siku moja Rita alimwambia, nafurahi sana unavyoperform, najua hata sisi siku moja tunaweza kushiriki nanyi kuimba kwenu. Yalikuwa maneno ya kukubali uwezo wake. Leo akishabikiwa, watu tunaitwa washamba. Natamani kumwona Master J live ili nimpashe juu ya jeuri yake. Sii mwungwana hata kidogo.
Huyo Salama ndo bure kabisa. Hana hata kauli njema ya kuwatia moyo washindani. Kwani uwezo wake ni wa kiasi gani katika fani ya muziki hata anaponda kiasi mtu unaweza kuomba ardhi ipasuke ikufiche?
JIPANGENI SAWA SAWA MSILETE UBABAISHAJI. MNAIAIBISHA BENCHMARK.
ATI MAJAJI PIA TUNA NAFASI YETU, KAMA NDIVYO, HAKUNA HAJA YA KUHAMASISHA WATU KUTUMA SMS ZAO. NINYI JOPO LA MAJAJI MNATOSHA. MBONA KUPATA MA-MISS KUNA JOPO JA MAJAJI? BADILISHENI NJIA. MSITUIBIE PESA ZETU KUPITIA SMS.
NAWASILISHA.
Huyo Master J ndo mshamba namba MOJA. UNA NINI WEWE HATA UMLINGANISHE MWANADAMU WA WATU KUWA SAWA NA MLINZI WAKO. KWANZA HIYO NI DHARAU KUBWA SANA, SIYO KWA HUYO MZUNGU BALI KWA HUYO MLINZI WAKO. INA MAANA MLINZI WAKO HUMTHAMINI? MAANA KULE KUMWITA MZUNGU UNAMWONA KAMA MLINZI WAKO MAANA YAKE HANA LOLOTE. LAKINI MLINZI ANA LOLOTE NDIYO MAANA UMEMWAJIRI ILI AKULINDE. KWA HIYO KUKULINDA, TAYARI UNAONA SI CHOCHOTE. UNAMWONA KAMA MBWA SIYO? NINGEKUWA MIMI NDO HUYO MLINZI WAKO, NINGEACHA KAZI SASA HIVI.
ReplyDeleteMBONA MASTER J, UNA MDOMO MCHAFU KAMA TUNDU LA CHOO CHA SHIMO???
I DOUBT YOUR LEVEL OF KNOWLEDGE.
HAKIKA MASTER J HAJAKOMAA KIMAADILI. NAWEZA KUSEMA HANA HATA ADABU. ANAWATUKANA WATU/MASHABIKI KUWA ETI WASHAMBA MBELE YA WAZIRI??
ReplyDeleteHALAFU ITV MMEKAA KIMYA BILA KUKEMEA, WAKATI YALE YALIKUWA YANARUSHWA LIVE, DUNIA NZIMA IKIANGALIA NA KUWASIKILIZA PALE MLUPOKUWA MNAKASHFU NA KUTOA MANENO YA UBAGUZI. HASA MASTER j NA SALAMA. SIJUI WANA UWEZO GANI??
..wadau mimi nilibahatika kuishuhudia Bongo Star Search (BSS) -fainali kupitia television.. Kwa kweli mwaka huu 2010, BSS ilikuwa na wafuatiliaji na watazamaji wengi zaidi ukilinganisha na miaka iliyopita (kuonyesha kwamba BSS inakua kila mwaka)..pia inanifurahisha kabisa kuwa na sisi watanzania tuna chombo ambacho kinaibua vipaji vya muziki ktk Tanzania kama ilivyo nchi zingine.
ReplyDeleteKwa hiyo, napenda pia kuchangia na kukosoa vitu vichache ili wahusika waweze kuviangalia vitu hivyo na kuvifanyia kazi na kuzidi kuiboresha BSS zaidi na zaidi:
KWANZA: Napenda kuwaasa majaji kuangalia swala zima kabisa la mashindano na kutoa maoni yao kwa washiriki bila kuangalia UBAGUZI iwapo watakuwepo washiriki ambao wana asili ya nchi ya kigeni. Pia katika kujaji sio vizuri kutukana, kudhihaki washiriki au watazamaji.. Hapo Master Jay alikosea sana kwa kitendo cha kutoa matusi na maneno ya dhihaka kwa watazamaji na mshiriki wa kizungu. Kwa wale tuliokuwa tukitazama TV tuliona wazi kuwa baadhi ya majaji walionyesha waziwazi kabisa kuwa hawakutaka mshiriki Joseph Payne awe mshindi (maana jaji Salama Jabir alisema angejiua kama Joseph Payne akishinda "wewe ushindi, mimi I will shoot myself" - Hivyo ndivyo alivyosema Salama J).. Very disappointing.. Tunaomba ustaarabu na professionalism zitumike sana ili BSS iweze kufika mbali na kuwa na heshima hata kimataifa.
PILI: How come Rita Paulsen (one of the judges) anakwenda kushika kura stejini then badala kumpa mtangazaji azisome, anazifunuafunua kuangalia majina yaliyomo na kuzichanganyachanganya..halafu funny enough anamwambia mtangazaji aanze kusoma jina la mshindi wa PILI.. halafu baadae ndio amsome mshindi wa TATU..then mshindi wa KWANZA !! Hiyo tayari inaonyesha kuwa kuna kitu Rita alikifanya hapo stejini.. Hata hivyo hakutakiwa kuwepo stejini hapo kabisa na kwamba yeye ndio anaetoa hizo karatasi za majina ya washindi na kumpa mtangazaji aszisome..(yeye alikuwa jaji, na zaidi ya hayo alikuwa ni kati ya majaji waliokuwa wanamchukia mshiriki mmojawapo waziwazi!!). Hiyo tu tayari ilituonyesha picha tofauti ya jinsi washindi walivyosomwa.. Na hata alivyosomwa mshindi wa PILI na wa kwanza alikuwa akifurahi sana na kulia hapo stejini na kuwakumbatia kwa muda mrefu..Rita kama jaji asingepaswa kutuonyesha picha kama hizo za kiupendeleo!! Naomba maswala kama hayo yaangaliwe kwa undani ili kuondoa dhana ya mashabiki tuliokuwa nayo miaka ya nyuma kwamba matokeo ya BSS huwa yanakuwa yameshapangwa.
Master Jay umemuaibisha Waziri aliyekuwa mgeni rasmi kwa kuwatukana watu waliokuwemo humo ndani kuwa wote ni WASHAMBA kwa kumfurahia Joseph Payne anavyoperform (maana na waziri alikuwa akifurahia na kutabasamu)..Mwandikie barua special ya kumuomba Waziri radhi, vilevile na sisi utuombe radhi kupitia radio station na TV..maana mle ndani tulikuwepo watu wengi wastaarabu, wasomi, wafanyabiashara wakubwa tena tunaheshimiwa na jamii na familia zetu.. tunashangilia tumeacha kupumzika nyumbani usiku huo saa 7 na nusu halafu Master jay anatuita washamba hivi hivi.. Kwanza hiyo peke yake inaonyesha ufinyu wa akili, elimu ndogo na uhaba wa ustaarabu.. JIFUNZENI KUTOKA KWA WENZENU - Tusker Project Fame, American Pop Idol, America Got Talent, Naija Sings, You Think You Can Dance, n.k - Majaji ktk kutafuta talent wakiwa watatu basi majaji WAWILI watakuwa wakichambua uwezo na vipaji vya washiriki wakati JAJI wa tatu atakuwa kapewa jukumu la kukosoa (critisize) hivyo vipaji na uwezo. Hiyo inasaidia washiriki waweze kujituma zaidi na zaidi jinsi mashindano yanavyoendelea..na hata kama wasipoendelea na mashindano, basi watakwenda kurekebisha na kujiendeleza kwa kusahihisha kutokana na walivyojifunza kutoka kwa utaalamu wa majaji nk. Lakini BSS haikufuata hivyo hasa kwenye fainali, mfano; majaji wawili walionyesha wazi kutukana na kudhihaki (Master Jay na Salama J). Msanii atajifunza nini kutokana na hayo matusi na dhihaka? Na sisi jamii tutakuchukuliaje wewe jaji kutokana na kutukana jamii na kumdhihaki kibaguzi mshiriki? Kumbuka hii ni Tanzania, hata serikali yetu kuna watanzania wenye asili ya kihindi na kiarabu, hatuna ubaguzi wala ukabila.. [MIMI NASHANGAA MLIKUWA MNAMCHUKIA MSHIRIKI MZUNGU, WAKATI MAJAJI WANNE WOTE HAKUNA HATA MMOJA AMBAE NI MWAFRIKA TYPICAL!! Mfano: Judge Aspen ni mzungu, Rita Paulsen ni Danish/Norwergian, Salama Jabir ni mzanzibari mwenye asili ya kiarabu, Master Jay na yeye pia hivyo hivyo -- sasa ubaguzi unakuja vipi hapo nyie tunapowachukulia kama wazalendo wenzetu kabisa!!] .. Ila Rita na Aspen; hawa walikuwa wakitumia busara ktk kutoa comments kwa washiriki ingawa tulikuwa tunaelewa wanamaanisha nini kama watu wazima.. KAMA HUMPENDI MTU, TUMIA BUSARA KUFIKISHA UJUMBE WAKO WA KUTOMKUBALI MTU (kama alivyokuwa anafanya Rita kwa Joseph Payne).
ReplyDeleteTUEPUKE UBAGUZI NA UCHAKACHUAJI, TUTAJIVUNIA BONGO STAR SEARCH..
Amongst of all, Rita, you came a long way with BSS, don't blow it up, please remember that.. We also need to be proud of BSS. I want to be like "BSS is my thing" when Im overseas.
We sijui Master juju au Master Joke ...Whatever u call urself....You are trash!....kama hapo unajiona celebrity think again...haupo kwenye list ya macelebrity wala wenye pesa wa Bongo. Listen...acha wenye nazo tuongee. Nakuambia tena hauna lolote, this was a chance for you to become a celebrity but you suck! Also you comments zinaonyesha School was not reachable. Wasomi always wanatafakari before speaking out..this proves you talk non sense..Go to school first then come and mingle with us...otherwise Trash
ReplyDelete