Home
Unlabelled
neshno jipya latapika mashabiki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
wajifunze kupunguza kiingilio ili wapate cho-chote, hii inaonyesha kuwa bongo inaendelea kuwa nchi ya kibepari, kwani marekani wananchi wasipoenda mpirani mashirika yananunulia viingilio wafanyakazi wao ili kuzuia tv blackout wakati huo huo kuimarisha jamii. mheshimiwa leodgar tenga kama utanisikiliza wabongo wanaweza kutengeza pesa nyingi kama utarudisha hamasa ya miaka ya xabini na themanini kama unavyoelewa enzi hizo mpira ulizalisha sana (talent) kama ingekuwa leo tusingekujua wewe au ezekiel greyson jujuman,shaaban katwila,katolila,leopold mkebezi nk
ReplyDeletewatu wanapenda kuangalia mpira ila viingilio haviko sawa kutokana na kipato chao. kunahitajika watendaji wanao weza kufanya hesabu za kupata faida wakati waangaliaji wakilipa bei ndogo. lakini hii pia inaonyesha kuna haja ya nchi kuangalia jinsi ya wananchi kupata kipato kwani hapa ni tabaka kubwa kutokauwa na kitu na hivyo kufanya wasiwe na nafasi ya kushiriki katika mambo mbalimbali ambayo kimsingi ni haki yao.
ReplyDeleteMichuzi upo?Nimebahatika kuingia mechi karibu zote tangu zimeanza,kabla ya kufutwa viingilio,baada ya kufutwa viingilio na nadhani niyaendelea kuingia baada ya kurudisha viingilio.Nimejitahidi sana kufanya 'study'ni kitu gani kinafanya watu wanashindwa kuingia viwanjani wakati mchezo wanaupenda sana?Hakuna cha viingilio vya juu wala nini,ni umasikini.Kiingilio cha chini kilifika hadi 2000TZS(Chini ya dola 2 )lakini watu wanashindwa "kuafford" kulipa.Baada ya mechi utaona watu wanatembea kwa miguu kuelekea makwao magomeni,mbagala,nk wakati daladala zimejaa uwanjani zinahita abiria(Tafakari)
ReplyDeleteKitu kingine ambacho nimekigundua ni kwamba wale wenye uwezo wa kulipa viingilio baada ya
"fungulia mbwa"hii wengi hawaji tena.Kijana mmoja anayefanya kazi ya "kulinda magari"nje ya uwanja alinidokeza juzi kwamba siku hizi baada ya kufuta viingilio 'HAWAPATI HELA' manake wenye magari hawaji tena!!Nadhani wanaogopa magari yao kudokolewa na vibaka waliozidi sasa uwanja wa Taifa.Ni hayo tu
1)VIINGILIO VIWE VINAVYOENDANA NA HALI HALISI YA MTANZANIA (WEKA KIDUCHU PATA WATEJA WENGI-FAIDA KIDOGO, AU WEKA KIKUBWA WATEJA WACHACHE-HASARA).
ReplyDelete2)KINGINE TIMU YETU YA TAIFA INAUMIZA KICHWA SANA. ITAFUTIWE UFUMBUZI WA KUDUMU.
Pale pale ni kuto thamini michezo na kuona ni mambo ya mzaha na bure bure, .Hebu tangaza Jay-Z anakuja halafu ona kutakavyo jaa,Mfano mzuri angalai hizo Fiesta, wanao jaa watuwa Huko huko Temeke na uswahilini wanalipa 10,000.
ReplyDeleteUmasikini una changia sana ila pia nihalai ya kuto ona umuhimu wa kuchangia mchezo wa mpira wa miguu.Viingilio vya watuwa chni viko chini sana kiasi utashangaa eti hawawezi afford.
Watu wenye pesa hawawezi kuja hapo tena , ukizingatia kuna vibaka wengi wanao pora mbele za watu, mimi mwenyewe nimeshihudia mtu akiporwa mbele yangu na kundi la vibaka na kupiga nika sema sito kanyaga tena hapo.
Aah jamani, wangefanya angalau T.shs 1000 tu(Elfu Moja)kiingilio, kuongezea gharama za utunzaji wa Wanja na kuzuia watu laki moja unusu kujitokeza kutaka kuingia ktk uwanja wenye uwezo wa watazamaji 70,000 tu. Tusiendekeze kuwa sponsor(wadhamini) wameshalipia kila kitu, Usalama Kwanza kwa watu ndio kipaumbele.
ReplyDeleteMaana kuna vyoo kuziba, viti kuchakaa n.k hivyo T.shs. 70,000,000(mchanganuo watu 70,000 X Tshs. 1,000 kiingilio) zingetumika kwa hilo na pia kuzuia watu laki moja unusu kutaka kuingia bure sije vifo vikatokea nje ya uwanja watu wakisukumana kama ilivyotokea Nairobi, Kenya juzi juzi.
Angalizo msicheze na uhai wa watu
Bora kuzuia maafa ya watu kukanyagana kwa kutoza kiingilio cha chini kabisa kama T.shs. 1,000.
Mdau
Changombe.
ni raha na ni hatari pia,
ReplyDeleteTFF Kiingilio kiwe ni sh 1,000
Timu ikishidwa kunaweza kukawa na tatizo kwa wachezaji pinzani
Hiyo inamaanisha michuano hiyo imekosa msisimko na mvuto. Mbona mechi ya Simba na Yanga viingilio vikubwa lakini watu wanajaa?! Wanaokuja kuangalia bure wote ni watu wa hali ya chini na wengi hawana shughuli zingine za kufanya. Wanatumia kwenda mpirani kama sehemu ya kupoteza muda.Inatakiwa kila mtu aone kukosa kuona mechi hizo ni jambo kubwa na mtu aone umuhimu wa kuacha hata shughuli zake aende mpirani. Pia hata timu nyingi za ukanda wa CECAFA zimeshuka viwango hivyo watu hawatarajii kuona ushindani na msisimko. Hata uamuzi wa kuzileta timu za nje ya CECAFA kama Zambia, Malawi na Ivory Coast ni kutaka kujaribu kuleta msisimko. Changamoto waliyonayo CECAFA ni kuhakikisha wanakuza kiwango cha mpira cha wanachama wao ili kuwa na timu kali zitakazoleta ushindani wa kweli na hivyo watu tuone kwenda mprirani ni muhimu.
ReplyDeleteUkweli katika timu ya taifa hakuna ari kama wachezaji wanapocheza Simba na Yanga......hilo limewaharibu mpaka viongozi, kwani mtu anaomba uongozi kwa ahadi ya kuifunga simba au yanga! hilo linaonekana hata wakati watu wanaposhangilia....hawakawii kugeuka kuanza kuzomea! Timu ya Taifa inakatisha tamaa.....na lawama kwa wachezaji hakuna kingine!........si mnaona offer za pesa kwa matajiri kwenye mechi ya simba na yanga!?
ReplyDelete