Mwanasiasa Mongwe Dk. Aleck Chemponda akisalimiana kwa furaha na bintiye Da' Chemi Che-Mponda ambae katua jana kutoka Marekani anakoishi kuja kumtakia hali mzee wake ambaye amelazwa katika hospitali ya Muhimbili wodi namba 8 Mwaisela akisumbuliwa na maumivu ya mguu wa kulia yaliyotokana na gauti. Baada ya matibabu ya takriban siku 14 leo anajisikia ahueni na anapiga stori kama kawaida yake

Dk. Aleck Che-Mponda akiongea na mke wa Dk. Remmy Ongalla aliyekwenda kumtembelea. Mumewe, Dk. Remmy, naye alilazwa hapo Mwaisela ila leo ameruhusiwa kuondoka.
Ankal akimsabahi Dk. Che-Mponda alipomtembelea Muhimbili leo jioni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Fulanazzzz in the building kama kawa kaka...

    ReplyDelete
  2. Ze Fulanaz!!!

    ReplyDelete
  3. Pole Dr! Pole Da Chemi na familia!

    ReplyDelete
  4. Mungu awasaidie ma Dk wetu. Dokta Remmy Ongala, na Dk chemponda

    ReplyDelete
  5. Dr. Che-Mponda, wish u speedy recovery and many more healthy years to come!

    ReplyDelete
  6. Michuzi andika kiswahili chepesi. Maanake hapa najiuliza YATENGEMAA maanake ni nini?
    Tunamuombea mzee wetu apone haraka

    ReplyDelete
  7. mie hata sijaelewa inamaana na remmy ongala naye alilazwa au? naona kama ankal umechapia hapo kiswahili mhh kinajirudia rudia au jamani wenzangu mnaonaje hapo

    kisura

    ReplyDelete
  8. Mungu akutie nguvu mzee DR.CHE-MPONDA na pia DR.REMMY ONGALA, mmewatumikia watanzania kwa moyo mzuri mmoja kupitia darasani na mwingine kupitia muziki. Mungu awalinde na kuwaongezea siku nyingi zenye afya njema.

    ReplyDelete
  9. Pole sana Prof. Dk Alex Chemponda!

    Naandika haya kutokana na historia yangu ki-afya ya kusumbuliwa na gout.

    Nilianza kuumwa gout nikingali Tanzania miaka ya 70s. Mwanzoni sikujua kwa nini kila baada ya miezi mitatu hivi dole gumba la mguu wagu lilikuwa linavimba na kuumwa sana kiasi cha kunizuia kutembea. Kwa umbumbu wangu nilikuwa nalikanada na maji moto; kumbe, ndio nilikuwa nazidisha maumivu.

    Nilipokuja huku Amerika, ugojwa huo ulizidi. Ikabidi niwaone madaktari walioniambia kuwa nilikuwa ninasumbuliwa na gout! Nikaanza matibabu ya kutumia dawa ya “nonsteroidal anti-inflammatory” ya indomethacin (indocin) pamoja na kuahidiwa kunywa maji engi kila siku.

    Lakini siku hizi hali yangu imetengamaa. La sivyo, gout si ugonjwa wa kuweza kumulaza mtu, japo una maumivu makali na kushindwa kutembea.

    Gout inatokana na kuzidi kwa uric acid mwilini. Lakini uric acid inaweza kupunguzwa kutokana na figo kufanyakazi zake vizuri na kutoa mkojo. Pengine uric acid inaweza kuzidi kwa sababu figo hazifanyi kazi vizuri au mwili unatoa uric acid nyingi au kutokana na vyakula vinavyozalisha uric acid vya “purines” au kubugia pombe na kula nyama-choma kwa wingi – ambako kunaweza ku-“trigger a gout attack.”


    Ajabu! Wa Ulaya-Amerika wengine huamini kuwa gout ni wa matajiri wenye kula vizuri (Mfalme Henry VIII wa Uingereza alikuwa anaugua). Wengine wanaamini kuwa wenye IQ ya juu hupatwa na gout (Albert Einstern). Kuna pia wenye kuamini kuwa gout unawaandama wanaume wenye testosterone nyingi ... na sababu nyinginezo.

    Rais Mzee Jomo Kenyatta ulimsubua kiasi cha kutovaa vitu ila viatu vya kanda. Rais M-7 naye (nasikia) anasumbuliwa na huu uonjwa, ingawa hanywi pombe, ndio maana wakati mwingine huvaa viatu vya kanda.

    Kwa wenye kusumbuliwa na gout, yafaa sana tuangalie vyakula tulavyo; tutafute tiba kupunguza maumivu; na tutafute njia ya kuzuia kabisa ugonjwa huu.

    ReplyDelete
  10. Asanteni sana wadau kwa maombi na salamu zenu. Baba ana matatizo ya prostate.

    Ndiyo Dr. Remmy naye amelazwa Muhimbili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...