SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeweka wazi wachezaji 34 waliosajiliwa dirisha dogo kwenye timu mbali mbali zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania bara ambayo kwa sasa imesimama kupisha michuano ya Chalenji na imepangwa kuendelea mzunguko wa pili Januari 16 mwaka ujao.

Kaimu katibu mkuu wa shirikisho hilo Sunday Kayuni alisema timu ya Yanga imesajili wachezaji wawili ambao ni Davies Mwape kutoka Konkola Blades Fc ya Zambia na tayari ITC yake imeshawasili na Juma Seif kutoka JKT Ruvu, huku mahasimu wao Simba wakiwa wamemsajili Ali Mohamed 'Shibori' kutoka KMKM ya Zanzibar na imemrejesha mchezaji wake Meshack Abeil ambaye walimpeleka kwa mkopo Afrika Lyon msimu uliopita.

Kwa upande wa Majimajji imesajili mchezaji wa zamani wa Simba Ulimboka Mwakingwe ambaye amekumbwa na kashfa ya kutumiwa kutoa rushwa kwa mchezaji wa Mtibwa Shaban Kado na aliachwa na Simba kwenye usajili wa msimu huu, wengine ni Patrick Betweli, Yahaya Shaban, Kassim Kilungo, Mohamed Kijuso ambaye ameichezea Simba msimu huu.

AFC ya Arusha imemnasa David Naftali kutoka Simba na wamemsajili kwa mkopo huku Azam Fc imewasajili Ahmad Chimpele na Ali Chimpele ambao ni wachezaji wao wa U20 wamewapandisha Ligi Kuu.

JKT RUVU: Erick Majaliwa, Bakari Kondo na Feisal Swai
MTIBWA: Salum Sued, Hussein Javu
JKT RUVU: Jumanne Juma, Maneno Isaya, Lungwecha Rashid, Omary Senkobo, Oscar Fanuel,Shaban Nassoro, Hamis Salum na Yasin Abdallah
TOTO AFRIKA: Kamana Bwiza, Musa Vologwe, Mathias Wandiba, Maleges Mwanga na Said Mwanga.

Kagera: Juma Mwenza na Steven Mazanda wakati Polisi Tanzania haijasajili dirisha dogo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...