Mpiganaji Shadrack Sagati wa gazeti la Habari Leo akitabasamu na mai waifu wake Cecilia Ndagula katika mnuso wao wa nguvu usiku huu katika ukumbi maarufu wa Golden Resort, Sinza, jijini Dar, baada ya kumeremeta katika kanisa la Ubungo Hill Seventh Day Adventist Church
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers Bw. Mkumbwa Ally akiwakabidhi maharusi risiti ya zawadi ya jokofu ambalo wafanyakazi wenzie Shadrack wamempatia kwa kumeremeta huko
Maharusi wakipokea kadi maalumu ya
wafanyakazi wenza wa Shadrack

Picha ya pamoja ya maharusi na wapiganaji toka vyombo mbalimbali vya habari waliojitokeza kwenye mnuso huo.
Ankal na wapiganaji wengine wakiwa katika foleni ya kutoa pongezi kwa maharusi
Wafanyakazi wenzie Shadrack katika picha ya pamoja
wapiganaji wa TSN wakiwa katika mnuso huo
Libeneke la 'shuffle' likipigwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Michu,
    Nasikia ile tshirt yako imeibiwa :) ha hah aha.

    Huyo dada mwenye mini gauni picha ya pili toka mwisho anastahili pongezi.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Sagati, maana ulikuwa umeshaanza kuzidi umri mpaka tukawa na wasiwasi. Hongera sana kwa tendo hilo la kihistoria. Tunakukaribisha Honeymoon huku USA.

    ReplyDelete
  3. Michuzi naomba utuwekee hii habari ya Zitto. Waandhishi wa habari mbona wanashindwa kutafsiri maneno madogo na wapotosha umma? Hebu angalia hivi ndio ilivyoandikwa "madaktari wameniambia ilikuwa food poisoning (chakula chenye sumu),” alisema Zitto." Food Poisoning sio chakula chenye sumu ni Gastro enteritis (mchafuko wa tumbo), hili linaweza kusababishwa na bacteria, virusi katika chakula, au kama chakula hakijapikwa vizuri,chakula kilichooza etc. Andikeni habari za uhakika

    ReplyDelete
  4. Hivi kweli kwenye harusi kuna umuhimu wa kuvaa mini!!!??? Hivi ukiwa umesim ama kwenye msitari wa mnuso bangili ikadondoka utaiokotaje?

    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  5. Huyo dada alievaa kinguo kifupi cheusi na kuanika mapaja kwenye shughuli za watu inahuu??? hiyo ni arusi sioni sababu jimama mtu mzima kuvaa namna hiyo utazani unaenda ngwasuma sio fresh, wadada lol! jifunzeni kuvaa nguo kuendana na shughuli.


    Hongerni sana maharusi bibi arusi kapendeza sana na shughuli inaonyesha ilikuwa ya kukata na mundu, hadi fulanaz iliwekwa kapuni!

    ReplyDelete
  6. Waswahili wanasema ndani ya Harusi kuna harusi nyingine inaweza tokea ndio maana huyo dada aliyevaa kimini anatenga ili napate buzz na kumuoa eti atoe nuksi. Sio unajua usemi wa dada zetu siku hizi. N.B wamesahau mwanamke mzuri ni wa tabia kuanzia mavazi mpaka kauli na utendaji.

    ReplyDelete
  7. nice wedding.i miss my team so much,vicky nnakukumbuka sana my dear.lakini frankly huyo dada aliye vaa nguo fupi kaniboa sana,kina dadatina,dada jenny da flora hamkuwepo.mngemtimua you are big sisters in this company you should make sure ladies are respecting themselves.hata kama hamko kazini lakini hiyo ni faction inayowahusisha wana TSN-ni mimi-from DXB

    ReplyDelete
  8. jamani naomba mnipe location ya ukumbi maana kwa kweli nimesikia mengi mazuri ya ukumbi huo "Golden resort"

    nina kaharusi kangu nategemea kukifunga mwishoni mwa january....

    michuzi tafadhali usibane comment hii

    wenu mtiifu manka

    ReplyDelete
  9. Michuzi,una tutumiaga wadau viota vya kujiachia pindi unapozuru sehemu,chonde naomba mdau kufikiriwa kutumiwa viota vya harusi Dar mfano tuanzie kwenye huo mnuso maana nisha pasikia ila bado sijafika


    Bachelor n Husband 2b

    ReplyDelete
  10. SOMENI HOSEA 8:8. Ndio mtaelewa waisrael walivyojichanganya na mataifa haijulikana mwisrael ni yupi wala wa mataifa ni yupi, unashangaa nguo fupi, labda huyo ni mwisrael. Pia hii ni ndoa ya WAESDA? au maana niwajuavyo wale sijui?

    ReplyDelete
  11. Ankal wewe ya kwako lini??

    ReplyDelete
  12. Chapeni kazi tujikomboe na ujinga, acheni biashara za kuoangalia watu wamevaa nini wakati wewe huchapi kazi upo kwenye internet. Hiyo ni Harusi na hakuna polisi wa kusema kavaa hiki au kile.

    ReplyDelete
  13. Kutyooo baba .....gwata akayumba !

    Bhulemo

    ReplyDelete
  14. wewe anony wa saa 07:48 tushachapakazi TSN na ndiyo umeikuta hapo ilipo na nnadhani wewe ndiyo muhusika uliyetukalia uchi hapo.Tumechapa kazi kwa adabu na heshima tungeenda uchi kama wewe usingepata kampuni ya kukuajili.Please anco mich mfahamishe I was there im not talking from the air asituharibie timu kabisa.By the way wana TSN I miss you dears.From DXB

    ReplyDelete
  15. Huyo mwenye mini mbona hivyo? Alikwenda kwenye harusi ya mwenzake kuchukua attention yote na ni siku ya mwenzake?

    Inabidi nikija kuolewa nawapa watu dress code ya harusi...It is my day that's it...usipopenda then don't show up...

    ReplyDelete
  16. Clubbing dresses mnaenda nazo kwenye harusi?

    ReplyDelete
  17. Mgasi wao ali wa kisi. Your wedding came fast brother. Hongela

    ReplyDelete
  18. Hongera Sana Shadrack Na Cecilia!

    ReplyDelete
  19. Huyo MDADA aliyevaa kamini ameenda kwenye harusi na lengo lake lakutafuta MBABA, na Rafiki yangu MICHUZI naona kila nikitoa ujumbe unanibania ujue nikija BONGO tutapambana maana ni wewe uliyepeleka ZANAKI kujifunza GO-JURUU wakati nachezea AVENGERS soccer club pale Chang'ombe.

    ReplyDelete
  20. Hongera sagati looh welcome to the club! we wish you all the best
    Debby- USA

    ReplyDelete
  21. We mdau hapo juu we unatafuta nini kwenye internet badala ya kuchapa kazi? umejuaje kama watu wesharudi job wako home wanacheki ishu za kwenye net? na kama mtu kachemsha lazima aambiwe next time awe na busara zaidi.

    ReplyDelete
  22. Hongera sana Sagati na mkeo, mmpendeza sana.Tulikuwa ktk msiba mie na chb tukashindwa kuja,but we are so glad ulipata support kubwa kutoka from fellow TSN members!God bless ur marriage

    ReplyDelete
  23. yego masika echinu echo chikomee, nyamuanga akuyane amanaga.

    ReplyDelete
  24. hayo ni mambo ya ulaya kwani huyo dada anaishi huko kaja juzi tu

    ReplyDelete
  25. huyo dada kaja juzi tu toka malekani msimsakame

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...