Bango la sherehe
Baadhi ya watanzania waishio na kufanya kazi nchini Liberia katika picha ya pamoja na Mh. Balozi Akin O. Fayomi - Mwakilishi Maalum wa Jumuia ya Afrika (AU) nchini Liberia wa kwanza kushoto waliokaa. Katikati ni Profesa Henrietta Mensa-Bonsu ambaye ni Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia na watatu kulia waliokaa ni Mwenyekiti wa jumuia ya Watanzania Bw. John C. Minja.

Mwenyekiti wa jumuia hiyo Bw. John C. Minja akihutubia watanzania na wageni waalikwa katika ukumbi wa Taaj jijini Liberia. Katikati ni Mh. Balozi Akin O. Fayomi - Mwakilishi Maalum wa Jumuia ya Afrika (AU) nchini Liberia na watatu kulia ni Profesa Henrietta Mensa-Bonsu ambaye ni Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia.
wadau wakiserebuka

Watanzania wanaofanya kazi nchini Liberia wamefanya sherehe maalum kuadhimisha miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania iliyofanyika jijini Monrovia hivi karibuni.

Mgeni Rasmi katika sherehe hizo alikuwa Mheshimiwa Balozi Akin O. Fayomi - Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika (AU) nchini Liberia. Umoja wa Mataifa uliwakilishwa na Profesa Henrietta Mensa-Bonsu ambaye ni Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia.

Katika hotuba fupi ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa jumuia hiyo, Bw. John C. Minja alielezea kwa kifupi harakati za Watanganyika hadi kupatikana Uhuru, maendeleo ya kisiasa na kiuchumi yaliyofikiwa hadi sasa pamoja na jitihada za Tanzania katika kushughulikia tatizo la wakimbizi pamoja na migogoro mbali mbali barani la Afrika. Aidha walimpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Naye Mgeni rasmi katika Sherehe hiyo Balozi Akin Fayomi aliipongeza jumuia ya Watanzania waishio Liberia kwa nidhamu ya kazi waliyo nayo na weledi wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Aliwapongeza waasisi wa Taifa letu kwa michango yao ya hali na mali katika harakati za ukombozi katika bara la Afrika na dunia nzima kwa jumla.

Pia, aliipongeza Tanzania kwa kudumisha Muungano ambao sasa una miaka zaidi ya 46 pamoja na kuendesha Uchaguzi kwa amani na kudumisha Amani na majirani zetu.

Aidha, aliahidi ofisi ya AU Liberia kushirikiana na Watanzania waishio Liberia katika kuandaa sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru hapo mwakani.
Naye Profesa Henrietta Mensa-Bonsu aliipongeza na kuishukuru Tanzania kwa kutuma Wataalamu mbali mbali kuisadia Liberia. Aliwapongeza Wataalamu hao kwa kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu. Alimalizia kwa kukipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kutoa wataalam waliobobea kitaaluma.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jamani tarehe 9 Disemba ni siku ya Uhuru wa Tanganyika na siyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania....watch out...the day is not even registered in nomber of multilateral bodies...siku inayohusisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni "Muungano Day"...inashangazadiaspora huko nje hamjui hata hizi details...mnaandika tu mabango na kupotosha watu...
    Kaka Michuzi uwe makini na uhariri wa hizi habari na picha zake,

    mdau

    ReplyDelete
  2. UHURU WA TANGANYIKA

    ReplyDelete
  3. Hata historia ya nchi yenu hamuijui - uhuru wa Tanganyika si Tanzania.

    ReplyDelete
  4. kweli ukikuta sehemu hakuna mchagga ujue kuna mwamba wa chuma lakina hata kama ni mwamba wa kawaida lazima kumkuta mmachame,muorombo,mmalangu,mkibosho,mmhuru na wengine wengi kama mnavyojifahamu wenyewe na kukubali kwamba hakuna kabila la wachagga

    ReplyDelete
  5. HIVI WATANZANIA WANAFANYA NINI LIBERIA??

    ReplyDelete
  6. uhuru wa wadanganyika sio wa tanzania plzzzzzzzzzz

    ReplyDelete
  7. duh hv kuna nchi inayokosa wabongo !!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...