Watanzania wanaofanya kazi nchini Liberia wamefanya sherehe maalum kuadhimisha miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania iliyofanyika jijini Monrovia hivi karibuni.
Mgeni Rasmi katika sherehe hizo alikuwa Mheshimiwa Balozi Akin O. Fayomi - Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika (AU) nchini Liberia. Umoja wa Mataifa uliwakilishwa na Profesa Henrietta Mensa-Bonsu ambaye ni Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia.
Katika hotuba fupi ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa jumuia hiyo, Bw. John C. Minja alielezea kwa kifupi harakati za Watanganyika hadi kupatikana Uhuru, maendeleo ya kisiasa na kiuchumi yaliyofikiwa hadi sasa pamoja na jitihada za Tanzania katika kushughulikia tatizo la wakimbizi pamoja na migogoro mbali mbali barani la Afrika. Aidha walimpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Naye Mgeni rasmi katika Sherehe hiyo Balozi Akin Fayomi aliipongeza jumuia ya Watanzania waishio Liberia kwa nidhamu ya kazi waliyo nayo na weledi wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Aliwapongeza waasisi wa Taifa letu kwa michango yao ya hali na mali katika harakati za ukombozi katika bara la Afrika na dunia nzima kwa jumla.
Pia, aliipongeza Tanzania kwa kudumisha Muungano ambao sasa una miaka zaidi ya 46 pamoja na kuendesha Uchaguzi kwa amani na kudumisha Amani na majirani zetu.
Aidha, aliahidi ofisi ya AU Liberia kushirikiana na Watanzania waishio Liberia katika kuandaa sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru hapo mwakani.
Naye Profesa Henrietta Mensa-Bonsu aliipongeza na kuishukuru Tanzania kwa kutuma Wataalamu mbali mbali kuisadia Liberia. Aliwapongeza Wataalamu hao kwa kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu. Alimalizia kwa kukipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kutoa wataalam waliobobea kitaaluma.


Jamani tarehe 9 Disemba ni siku ya Uhuru wa Tanganyika na siyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania....watch out...the day is not even registered in nomber of multilateral bodies...siku inayohusisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni "Muungano Day"...inashangazadiaspora huko nje hamjui hata hizi details...mnaandika tu mabango na kupotosha watu...
ReplyDeleteKaka Michuzi uwe makini na uhariri wa hizi habari na picha zake,
mdau
UHURU WA TANGANYIKA
ReplyDeleteHata historia ya nchi yenu hamuijui - uhuru wa Tanganyika si Tanzania.
ReplyDeletekweli ukikuta sehemu hakuna mchagga ujue kuna mwamba wa chuma lakina hata kama ni mwamba wa kawaida lazima kumkuta mmachame,muorombo,mmalangu,mkibosho,mmhuru na wengine wengi kama mnavyojifahamu wenyewe na kukubali kwamba hakuna kabila la wachagga
ReplyDeleteHIVI WATANZANIA WANAFANYA NINI LIBERIA??
ReplyDeleteuhuru wa wadanganyika sio wa tanzania plzzzzzzzzzz
ReplyDeleteduh hv kuna nchi inayokosa wabongo !!
ReplyDelete