Baadhi ya Wadau waliohudhulia uzinduzi wa shina jipya la Luton wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Tawi la UK, Maina Owino.

Watanzania wengi walifurika Jiji la Luton Uingereza na kujiunga na chama cha mapinduzi katika ufunguzi wa shina jipya la Luton uliofanyika siku ya Jumapili Tarehe 12. 12. 2010 katika hoteli maarufu Chiltern UK.

Wengi wao wasema wana imani kubwa na CCM katika kuiongoza Tanzania kwa kuonyesha mwelekeo wa kuwa na imani na Vijana wasomi wachapakazi walioko ndani na nje ya nchi.

Ufunguzi huo ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa Tawi la CCM – UK Ndugu MAINA OWINO kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama akiwemo Katibu Uenezi wa siasa Bwana Moses Katega. Pia Viongozi kutoka mashina ya Reading, Birmingham na Sehemu zote za London walijumuika pamoja.

Katika hotuba yake fupi Ndugu MAINA OWINO alitoa changamoto nyingi za mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita chini ya Uongozi wa Mwenyekiti CCM Taifa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE katika nyanja mbalimbali kama Madini,Elimu, ukusanyaji wa mapato ya serikali, waajiriwa wenye sifa za kukidhi nafasi za uongozi serikalini katika nyanja zote na ujasialiamali kwa watanzania wanaojitafutia maendeleo bila bugudha.

Changamoto kuhusu ushiriki wa vijana wasomi hapa UK kuingia katika mchakato wa siasa ndani ya chama ili kuleta mabadiliko yatakayozidi kukiimarisha chama kisera, mwelekeo na kuzidi kuwaletea watanzania maendeleo katika nyanja mbalimbali kupambana na kupambana na umasikini yalitolewa na Katibu wa shina jipya la Luton aliyechaguliwa siku Ndugu ABRAHAM SANGIWA na kuungwa mkono na wajumbe wote waliohudhuria ufunguzi huo

Viongozi Waliochaguliwa siku hiyo ni:

ALBERT NTMI – MWENYEKITI

ABRAHAM SANGIWA – KATIBU MKUU

JOHN MBWETE – MJUMBE

SAMMY MARTIN – MJUMBE

NORMAN WAGE - MJUMBE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. wanaCCM Uingereza mti wa matunda ndio hutupiwa mawe mengi. Endelezeni mapambano bila kukoma.

    Kademi chris

    ReplyDelete
  2. Hivi wabeba box mbona mko bize na siasa sana huko/ kwani kuna visima au barabara za kuhamasisha kujengwa! khhaaaa!

    ReplyDelete
  3. Achane ukenge.... fungueni matawi ya CHADEMA achane CHAMA CHA MAFISADI

    ReplyDelete
  4. Sisi wana-CCM wa Moshi mjini tunawapongeza kwa hatua hiyo. Tuendeleze harakati hizo. Tuko pamoja nanyi. CCM DAIMA!!!!!!!!WanaCCM, Kiboroloni. moshi.

    ReplyDelete
  5. Swafi sana. Tukumbuke: CCM guardians of national unity and peace in our beloved Tanzania. Venceremos! CCM mbele daima. Ngulumbalyo.

    ReplyDelete
  6. Ingawa mko mbali, sisi wanachama wa CCM tuko pamoja na nyinyi. Morani7.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...