
Hivi ndivyo soko la Mbeya uhindini linavyo onekana kwa sasa. Kwa hakika walio kuwa na maduka makubwa wote wameathirika kwa kiasi kikubwa sana na janga hilo la moto. Maduka makubwa sokoni hapo likiwemo la Mushi na Nanetelecomunnication yanayo angalia upande wa Benki ya NMB Mbalizi Road hayakuambulia kitu chochote kutokana na Moto kuunguza kila kitu na kuzingira eneo lote hilo...Taarifa zaidi zitazidi kuwajia.
Picha na Ripota wa Globu ya Jamii, Mbeya.
kwanza poleni sana watu wote walioathirika na moto huu. Pili nadhani huu ni wakati muafaka wa kufikiria bima za moto kwa wafanya biashara wadogo wadogo.
ReplyDeleteTupe Tamko la Mbunge wa huko kuhusiana na hali hiyo tafadhali!
ReplyDeletePole sana Mh.JOSEPH MBILINYI kwa watu wako wapendwa kuunguliwa na maduka yao,ama kwa hakika hiyo ni changamoto ya kwanza kwako.Pia hiyo sehemu iliyotajwa kuteketea kabisa lipo duka la dadangu schoolmate wangu sangu secondary 1990-1994 Agnes Memba popote alipo nampa pole yeye na mdogo wake,ni watu wazuri sana
ReplyDeleteMbona Jiji la Mbeya laandamwa na majanga ya kuungua kwa masoko yake?
ReplyDeleteMbeya kunani tena?
ReplyDeleteMwaka ulee ilikuwa Mwanjelwa moto mpaka chini. Leo ni Uhindini.
Mbona masoko ya huko yanapotea kwa moto tu? Halafu utasikia baada ya moto hakuna tena watu kurudi hapo bali watahamishiwa eneo jingine.
Somethingy smells fishy here!