Retired President Alhaj Ali Hassan Mwinyi receives Rev. Canon Dr. E. J. Kandusi, Campaign Coordinator and FounderTanzania 50 Plus Campaign and other members of the organisation at his Msasani residence in Dar es salaam

Retired President talks to his guests of his mango tree garden at his Msasani residence
Retired President Alhaj Ali Hassan Mwinyi with his guests
The guests are happy with the mango presents Mzee Mwinyi gave them
Mzee Mwingi is happy to receive pamphlets of the organisation

Dear friends, Greetings!
Today we had a two hour visit to President (Rtd)
Alhaj Ali Hassan Mwinyi. President Mwinyi is our campaign PATRON.

We discussed in detail on the success of the campaign and the challenges we are facing. President Mwinyi continued his commitment to support the campaign and be more active in its work.

We talked of the campaign, visited his mango plantation, we were each given some harvest from the mango trees and we were escorted to the gates each currying a bag full of mangoes.
We had a great moment and we share you our joy.
Come and support the campaign NOW!

Regards,
Rev. Canon Dr. E. J. Kandusi
Campaign Coordinator and Founder
Tanzania 50 Plus Campaign
PROSTATE CANCER: Literacy, Advocacy and Support Initiatives
Phone:+255 754 402033

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Mwenyezi Mungu awabariki Rev. Canon Dr Kundusi na mzee wetu Ali Hassan Mwinyi kwa kazi yenu nzuri. Natoa wito kwa Watanzania wote wenye uwezo (hata vijana)waiunge mkono kampeni ya TZ 50+. Mdau wa afya.

    ReplyDelete
  2. Hawa wazee katika ari na moyo wao ni vijana kuliko vijana wengi wa miaka 20. Good role models.

    ReplyDelete
  3. Hawa wazee wangu mbona mnamchafulia carpet Mzee ruksa, mwenyewe kavua viatu nyie manasahau! vipiii....

    ReplyDelete
  4. Mzee Ruksa ana miaka 85 hapo, lakini anaonekana ana afya nzuri kuliko watu wengi sana wenye miaka 45. Kwa wale wenye akili timamu kuna mambo ya kujifunza kutoka kwa huyu babu yetu.

    ReplyDelete
  5. hivi tutaendelea lini katika swala la usafi kwa waswahihili?
    TUMEZOEA KUKANYAGAKANYAGA TUUUUUUU!!!!VUENI VIATU BWANA.

    ReplyDelete
  6. Salaam,

    Mh! watu wengine bwana! mwenyewe kaonesha ustraabu kavua viatu wao na maviatu yao hawajui kama wamekanyaga vinyesi au nini Loh! kweli kama hujui TOHARA! basi una khasara! maana mtu mwenye kujua TOHARA (USAFI NA UNADHIFU) basi hawezi kujali kama ndani huwezi kuingia na maviatu yako ulotoka nayo nje il hali hujui umekanyaga kitu gani!

    ReplyDelete
  7. mzee ruksa bado watanzania tunakukumbuka nakukuthamini sana,wewe ni muungwana,usiyependa makuu na mstaarabu sana.unaongea kwa hekima mnoo.vijana wanapaswa kuiga mengi kutoka kwao.wewe ni mfano mzuri sana kwa kizazi chetu.mungu akuzidishie miaka mingi zaidi tuendelee kupata hekima kutoka kwako.

    ReplyDelete
  8. yees this is a simple president. I like him. hana makuu kabisa wala makash-kash ya ajabu ajabu..hata kwake panaonekana pamekaa ki-uananchi kabisa.he is relaxed.
    Big up to Mzee Ruksa

    ReplyDelete
  9. Kadri ninavyomfahamu mzee wetu mpenzi mzee rukhusa, kwa ukarimu na hisani aliyonayo, ninaaamini kabisa aliwakatalia kuvua viatu hawa wazee wa watu! Nadhani cha muhimu tuzingatie ujumbe hawa wazee, kama wewe ni mwanaume kuanzia miaka 45 kwenda jioni kapime Prostate Cancer ni kipimo rahsi sana lakini ukidharau madhara yake weeee acha tu! tumekosa jamaa zetu wengi sana kwa kukosa kupima mapema, wangewahi wangetibiwa au kuiondoa na mtu kuishi maisha ya kawaida kabisa!!!

    Hongereni sana wazee wetu na endeleeni kutuhamasisha!

    ReplyDelete
  10. Mlalamika bure kuhusu hawa wazee kuingia na viatu,walipojaribu kuvua viatu,mwenyeji wao akawambia RUKSA KUINGIA NA VIATU!

    ReplyDelete
  11. Nakumbuka wakati ule bado akiwa rais, alikuwa aki jog kila asubuhi. Alikuwa aki jog maeneo ya darajani (Sealender bridge). Ni mtu wa mazoezi, yuko fit. Na marehemu Nyerere naye alikuwa mtu wa mazoezi pia, waliokuwa karibu wanasema Nyerere alikuwa akifanya mazoezi ya martial arts.

    ReplyDelete
  12. hivi kuna utaratibu wowote wa wananchi kuwaona viongozi waliopita ?? na kama upo naomba nielekezi, mimi namfagilia sana mzee ruksa , ningetamani hata niwe nae dakika 1 nimsalimie na kumshukuru kwa aliyetutendea na kujua hali yake, wadau nifahamisheni, ila MKAPA sihitaji kumuona ...

    asante michuzi

    ReplyDelete
  13. Nyerere alikuwa na baiskeli ya mazoezi.

    ReplyDelete
  14. Tusipoteze lengo!

    Pamoja na kumpongeza Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, yafaa tujikite zaidi katika ujumbe wa mtundiko huu.

    Sijui kama hao wazee wa Tanzania 50 plus Campaign walikuja kumjulia hali Mzee Mwinyi; walikuja kumwona Patron wao wakiwa na ujumbe kuhusu kampeini na jitihada zao za kupambana na saratani ya prostate.

    Kwa muda mrefu, saratani ya prostate ilikuwa haipewei nafasi yake ya ugunduzi na tiba kamili.

    Mababa zetu wengi walikokuwa wanasumbuliwa na ugonjwa huu walikuwa wanatembea hospitalini wamenig’niza “catheter”.

    Tuliwafahamu kuwa walikuwa na “ugonjwa wa mkojo” tu; kumbe walikuwa na saratani (adenocarcinoma cancer)!

    Inafaa sana mababa walio na zaidi ya miaka 50 hivi kupimwa endapo wana dalili hizi: mchuruzi wa mkojo ni dhaifu, kukojoa kojoa kila mara, kukojoa kwa shida, maumivi wakati wa kukojoa, damu kwenye mkojo au shahawa, maumivu ya mgongo au nyonga, na maumivi wakati wa kutoa mbegu (ngono).

    Mganga anaweza kupima damu kubaini psa (prostate specific antigen). Kwa kawaida, psa ikiwa chini ya pointi 4, kuna uwezekano mkubwa wa kutibu. Zaidi, mganga anaweza kupima kiasi cha percent free-PSA ; PSA velocity; PSA density (PSAD) ; na Age-specific PSA reference ranges.

    Mganga anaweza kupima kwa kidole, DRE (Digital Rectal Examination); Transrectal Ultrasound; Prostate Biopsy; na X Rays and Imaging Techniques ili kuona kuna viini na jinsi vilivyo “how aggressive” katika kuenea na kuingilia sehemu nyingine za mwili (tezi za lymph au mifupa).

    Kuna haja pia ya mganga kuzingatia “biomakers” nyingine zinazoweza kuleteleza
    “aggressiveness” ya saratani.

    Inafaa sana kupimwa. Lakini wengine wanaogopa kuambiwa uweli kuwa wana saratini, mithili ya ukimwi. Tusiogope.

    Tiba ya sasa ni moja au mchanganyiko: upasuaji wa kuondoa tezi hilo; radiation therapy treatment ya kuua viini vya saratini; kuwekewa brachytherapy - punje yenye radio active – ukubwa sawa na punje ya mchele; na chemotheraphy, yaani, madawa ya kumeza ya hormoni ili kupunguza homoni za kiume (testosterone); kupewa madawa ya homoni za kike (estrogens) ili kupunguza korodani kutengeneza testosterone.

    Nayaandika haya kutokana na sababu mbili kubwa:

    Mosi, nipo hapa New York. Miaka miwili hivi iliyopita, prostate yangu ilikuwa inanipa matatizo ya kukojoa, na kadhalika.

    Kutokana na sababu kwamba baba alisumbuliwa na prostate hadi akaaga dunia, daktari wangu alishauri nifanyiwe upimaji wa hakika haraka iwezekananvyo.

    Ikagundulika kuwa prostate yangu ilikuwa ina viini vya saratini (adenocarcinoma). Nilifanyiwa matibabu ya radiation therapy treatment kwa muda wa siku 67 hivi. Naendelea kupona vizuri!

    Pili, inaambata na hiyo ya mosi, Rev. Canon Dr. E. J. Kandusi, aliwahi kutamka katika gazeti moja la mtandao (online) juu ya saratani ya prostate (akitumia mfano wake na methali ya ki-China):

    “’To know the road ahead, ask those coming back’. I am the one coming back and so share my experience”.

    (Tafsiri yangu: Ukitaka kujua barabara ikoje huko mbele, uliza wanaorudi kutoka huko; mimi ni mmoja wa hao wanaorudi hivyo nagaia ujuizi.)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...