Auntie Ezekiel na mwenzie wakivinjari mitaa ya Kigali
Ray Kigosi na Steve Kanumba wakitembezwa mitaa ya Kigali
Kila walikopita walizingirwa na wapenzi wa filamu za bongo
Kanumba haamini macho yake kwamba wakati nyumbani Tanzania kuna wanaowabeza, huko ugenini wanapokelewa kwa furaha na heshima kubwa. Tujadili hili wadau. Ni lini tutaanza kuthamini vyetu na kukoma kukatishana tamaa bila sababu za msingi?Picha kwa hisani ya gazeti la NEW TIMES.
BOFYA HAPA


Sababu za msingi kubezwa ni kwamba hawazingatii maadili ya heshima ya Kitanzania ndani ya filamu zao, kila kitu wanataka kuweka hadharani hata mambo ya faraghani.
ReplyDeleteMdau
Sokoni Kariakoo
Kweli kabisa ndugu yangu, kwa mfano huyo Shangazi Ezekiel vitu vyake vya faragha anavianika hadharani.
ReplyDeletewaache mashauzi bana sielewi kwanini wasanii wengi bongo wakipata umaarufu wanataka walambwe miguu, hiyo yao ni kazi pia kama kazi za wengine heshimu kazi yako na ifanye kwa bidii utafika mbali usitake sifa za kijinga hazikufikishi popote!!!
ReplyDeleteni kweli usemayo mdau wa sokoni kariakoo, heshima na utamaduni wetu lazima tuulinde, tusifate mambo ya nje
ReplyDeleteWanajiona kama kina brad pitt kwi wi kwiiiiii.......
ReplyDeleteNabii hana heshima kwao
ReplyDeleteishu sio kama wasanii wa kibongo wanabezwa ukweli ni kwamba hawazingatii weledi "professionalism"katika kazi wanazofanya.
ReplyDeletewakitaka kusonga mbele na kuwa na mafanikio lazima wazingatie professionalism katika kazi zao otherwise wataendelea kudharauliwa tu.
Emerging film producer
mikocheni
KUMBUKA, MANABII WENGI WALIBEZWA NA KUKATALIWA MAKWAO KULIKO HATA UGENINI. MUHAMMAD SAW ALIDIRIKI KUKIMBIA KWAO MECCA NA KUPOKELEWA KWA MOYO MKUNJUFU UGENINI MEDINA.
ReplyDeleteBaba Ochu
Jang'ombe kwa maharuki
Z'bar
Hawa akina Kanumba hawapaswi kushangaa na kujiuliza kwanini Tanzania wanaonekana ni watu wa kawaida tu pamoja na kwamba wao wanajiona ni masupastaa wanaopaswa kusujudiwa na kila mtu. Hata Nigeria waigizaji kama Ramsey Nouah wanaonekana ni watu wa kawaida tu na hakuna anayewashangaa wanapotembea mitaani. Ni jambo la kawaida kwa waigizaji na wasanii wengine kuwa maarufu zaidi nje ya nchi zao.
ReplyDeleteWanaowabeza wasanii wetu wa Tanzania na kazi zeo eidha za tasnia ya filamu au muziki na kadhalika wanatatizo la kuwa na ROHO MBAYA zilizojaa chuki dhidi ya maendeleo ya wenzao. Maana kama ni kweli kazi za wasanii wetu hazina ubora mkubwa mbona wana nchi wa Rwanda wameonekana dhahiri kuzikubali kwa kuwapokea wasanii wetu wa kazi hizo kwa heshima kubwa kiasi hicho sawa na namna ambavyo hupokelewa wasanii wa Marekani na Ulaya wenye umaarufu wa kimataifa wanapotembelea nchi za kigeni?. Hapana, nyie mnaowabeza wasanii wetu acheni kuwabeza kwani kupokewa kwao vizuri sana namna hiyo Rwanda kumekuumbuweni. Ukweli usiyojificha ni kwamba kazi za wasanii wetu ni nzuri sana na zina ubora wa kimataifa ambao hata kama ni kushindana zinaweza sana kuchuwana vikali na zile za wengine wa Marekani na Ulaya na wakati mwingine hata kuzishinda baadhi yake. Ni kweli kwamba bado wasanii wetu wanapungukiwa na uwezo wa kipesa wa kuhusisha vifaa vya gharama kubwa kubwa sana katika tasnia zeo tatizo ambalo litakwisha tu kwa kuwa tasnia yao imeanza kuwatoa vizuri kifedha na hata Serikali yetu inaweza kuwasaidia inapobidi kwa kuwa tayari imekubali mchango wao mkubwa kitaifa na kijamii, lakini kwa upande wa uwezo (physical capabilities) na vipaji (talents) za kufanya tasnia zao hizo kwa kweli wasanii wetu wanafanana na wasanii wengi wa nchi za nje wenye umaarufu wa kimataifa na wengine wao hata wanawapita. Nakuombeni tupende kazi za wasanii wetu na kama kuna kasoro fulani fulani wasanii wetu wataonekana kuwa nazo au kuzifanya basi ni busara kuwasilisha kasoro hizo vizuri (kwa maneno mazuri) kwa wasanii husika ili wajirekebishe na siyo kuwavunja moyo na kuwakatisha tamaa kwa kuwatamkia maneno mabaya. ENYI MNAOWABEZA WASANII WETU NA KAZI ZAO ACHENI ROHO ZA KICHAWI.
ReplyDeleteNi kweli mdau ulicho comment ni sahihi kabisa, we unafikri wakifanya hvyo nani atawabeza, maana kuna wasanii nchi zingine wanaheshimiwa mno na wa kwao. Hiki kwetu pia kinawezekana, wabadilike tu waache fujo zisizo na msingi watabebwa hata kubebwa.
ReplyDeletePamoja na kutozingatia maadili ya heshima, pia kiwango cha ubunifu ni kidogo mno, KUIGA filamu za Ki-Nigeria kumezidi na pia maudhui hayaendani na mila na mazingira ya Ki-Tanzania. Kinachowafanya watu wa Rwanda wapende filamu za Ki-Bongo ni matumiziya lugha ya Kiswahili.
ReplyDeleteKAKA MICHU KWANI WEWE HUJUI NABII HANA HESHIMA KWAO?
ReplyDeleteUKIWA NA KITU HUONI THAMANI YAKE LAKINI WENGINE WANAKITHAMINI
ASANTENE SANA WATOA MAONI MLIOTANGULIA HAPO JUU MIE YANGU NI KWAMBA WASANII WETU BADO HAWAJAKIZI KABISA KIU YA WATANZANIA WALIO WENGI. WAO KILA KIKICHA WANAIGIZA MAMBO YA MPENZI TUU NA MAJUMBA YA KIFAHARI MAGARI YA KIFAHARI WAKATI KATI YA WATANZANIA WAPATAO MLIONI 45 NI WASATNI WA 5MILION YA WATANZANI WANAKARIBIA AU WANAISHI MAISHA YA NMANA HIYO NDIO MAANA NASEMA WENGI WAPE. ILA KWA NCHI ZA WENZETU INAWEZEKAN KABISA MAJORITY WANAISHI MAISHA BORA NDIO MAANA WANAWAKUBALI. NA PIA MAUDHUI KATIKA FILAMU ZAO SI YA KIBONGO KABISA NA HILI HALINA UBISHI NA FIKIRI KAMA WANTASIKILIZA MAONI YA WALIO WENGI WATFIKA MBALI AU LA WATISHIA KUTOKUBSLIKA HOME PIA WAMULIKE NA MAENEO MENGINE MFANO MAISHA HALISI YA MTANZANIA WA MJINI NA KIJIJINI KAZINI MASHULENI NA SIASA KWA UJUMLA WA ACHE KUIGA PICHA ZA WENZETU KTOKA NIGERIA NA KWINGINEKO. PIA WASIJIONE WAO NDIO BORA KATIKA JAMII ILA JAMII NDIO ITAKAYOAMUA UBAORA WAO MDAU DANI NAWAKILISHA
ReplyDeletePamoja na mapungufu ya hapa na pale, sinema zetu za Kibongo zinakuja juu. Tuwatie moyo na kushauri inapopasa sio kuwabeza waigizaji wetu. Ushauri wa haraka tu kwa Kanumba, Ray na wengine ni kwamba wafanye mazoezi na wale lishe bora. Hivi vitambi na tasnia ya sinema naona haviendani kabisa. Watapoteza mvuto haraka sana kama wataendelea kujiachia kunenepeana ovyo!
ReplyDeletehao wanapenda kujifunza kiswahili thats y wanawaangalia hao washamba waliokosa ubunifu,!
ReplyDeleteKwa kweli wasanii wetu wa filam Tanzania mmejitahidi kuonyesha bidii na uwezo wenu katika tasnia hii.Miaka michache ya nyuma tulukuwa tunategemea sana sinema za ki nigeria ingawa baadhi ya watanzania tulikuwa hatuelewi vizuri kiingereza,tangu tuanze kuwa na sinema zetu wenyewe imekuwa vizuri sana kwa watanzania wote wanaoelewa kiingereza na wasioelewa,
ReplyDeletena hiki ni kitu cha kujivunia pia kinasaidia kuitangaza nchi yetu nchi za nje na nchi jirani.Hongera sana wasanii wetu wa filamu,Ushauri wangu mkubwa kwenu ni kuepuka na kashfa katika vyombo vya habari,maana kila tunaposoma magazeti ya huko nyumbani ni kashfa tupu zinazowahusu wasanii hawa,mara wamepigania wanaume ,mara
mwingine amechanganya wanawake mara ulevi wa kupindukia,na kila siku utasikia kama si mango garden,billicanas mara leaders club
mara sigara club,yaani siku zote inaonekana wasanii hawa wanashinda kwenye vilabu na kujihusisha na kashfa mbali mbali,nadhani wakati mwingine mngetumia muda wenu kuweza kujisomea ili muweze kujiendeleza na kuongeza upeo wenu katika field hii ya uigizaji,msiridhike na level mliyonayo hivi sasa,maana kila siku ni kashfa tupu vilabuni,hii inachefua sana,jirekebisheni muonyeshe mfano na maadili mema katika jamii, nasi tutawaheshimu na kuwakubali zaidi.
mdau,Tokyo,Japan.
Nabii hakubaliki kwao...!!!
ReplyDeleteSina budi kuwapongeza kwa kazi nzuri mnazofanya. Ila kinachonikondesha ni swala la COSTUME!!!! DRESSING CODE Dada yangu Auntie Ezekiel HIYO TOP NI YA KUVAA JIONI SIO MCHANA KWEUPE. Umependeza lakini siku nyingine consider about what to wear and the time of wearing it
ReplyDeleteNi kweli sekta ya filamu imekua kwa kasi kubwa katika miaka ya karibuni.Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kuona waigizaji wa Bongo wanalazimisha wapendwe na kila Mtanzania. Unapokuwa msanii watakuwepo wakataokuhusudu na vilevile watakuwepo watakaokuponda. Kinachotakiwa hapa ni kuheshimu mawazo ya kila mtu. Ikumbukwe kuwa si kila anayekukosa anakutakia mabaya au anakuonea wivu. Mapungufu mengi yanayozungumzwa kuhusu filamu za Bongo ni ya msingi. Waigizaji na 'producers' wanapaswa kuzingatia ukosoaji na ushauri huu bila kinyongo.
ReplyDeleteINASHANGAZA SANA KWAMBA ASILIMIA 99 YA WOTE MLIYOTOA COMMENT HAMUWAUNGI MKONO WASANII WA TANZANIA. HII INAASHIRIA KWAMBA WATANZANIA TUNAROHO MBAYA SANA ZA KUHUJUMIANA BURE BILA SABABU ZA MSINGI NA NDIYO MAANA KATI YETU KUNA IDADI KUBWA SANA YA VIBAKA, MIJIZI, MAJAMBAZI NA WACHAWI AMBAO WOTE HAO NI MAADUI WA MAENDELEO YA WATU WENGINE. NINAMUUNGA MKONO HUYO MDAU MMOJA TU PEKEE ALIYESEMA KUWA "ACHENI ROHO ZA KICHAWI".
ReplyDeleteANTIE EZEKIELI VIPI? TOTO LIMEWIVA KAMA NINI. DUHHHH
ReplyDeleteSASA MIMI SINGO OL DHA WEI BEBE
NISTUE BASI.
ALAFU MBONA NYAMA ZIMEONGEZEKA SANA ANTI-EZEKIELI? JIM NINAYO NYUMBANI SO ISHU
Filamu za Bongo haziendelei kwa kuwa waigizaji na ma-producer hawataki kukosolewa. Wakikosolewa hukimbilia kudai wanaonewa wivu au wanapigwa vita. Ikumbukwe kuwa Watanzania haohao wanaoangalia filamu zao pia huangalia filamu zinazotoka Hollywood, achilia mbali Nollywood (Nigeria) au Ghana. Sekta ya filamu Tanzania bado ni changa sana, tena sana. Waigizaji wa Bongo wawe wanakubali kuambiwa wapi wanakosea la sivyo hawatafika mbali.
ReplyDeleteYaani nimesoma hii article nikafurahi mnooooo siwezi kuelezea. kwa kweli nimefurahi sana kuona kuwa wasanii wetu wanakubalika hadi nje ya nchi, hii ni dalili nzuri maana wanaitangaza nchi yetu. Big up guys and all da best!!
ReplyDeleteJamani msiwakandie sana, makosa yapo ambayo yanarekebishika, tuwasaidie kwa kuwapa moyo na sio kuwakandia na kuwavunja moyo. KANUMBA WEWE NI MKALI AND I LIKE YOU BECAUSE U ARE ALWAYS URSELF, U DO NOT PRETEND. UNAFIT KILA MAHALI, HURINGI, HUNATI NA UNAONGEA NA KILA MTU. YAANI U R VERY GENUINE, NAPENDA HICHO KUTOKA KWAKO........... KEEP IT UP.
ipmwaipaja@yahoo.com
Wengi wa mnaowabeza wasanii wetu mbona hamfanyi haki? Maana mnakosoa tuuu kana kwamba filamu zao zote hazina hata mahala pamoja pakustahili kusifiwa!! Hapana siyo kweli, filamu zao zina mengi tu ya kustahili kusifiwa. Na ni kwa tabia hizo hizo zilizojaa katika jamii zetu na kwa bahati mbaya hata katika serikali yetu za watu kutopewa haki zao ipasavyo ndiyo maana baadhi yetu wanaamua kufanya utaalamu wao nje ya nchi wanakothaminiwa na kupewa moyo. Nami naunga mkono hao waliyochangia waliyosema acheni roho za kichawi kwani roho za aina hiyo ndiyo zinapelekea baadhi ya wataalamu wetu wengi kufadhilisha kufanya kazi nje ya nchi yetu wanakothaminiwa na kulipwa vizuri na matokeo yake sasa ni taifa letu kukosa kufaidika na utaalamu wao.
ReplyDeleteMIMI NI MSANII MKUBWA TU SANA HAPA NCHINI KWETU TANZANIA. LAKINI KWA JINSI TUNAVYOBEZWA NA WATANZANIA WENZETU, NIMEAMUA KUANZISHA KAMPENI BABKUBWA NA IMEANZA KUFAULU YA KUWAKINAISHA WASANII WENZANGU TUHAMIE RWANDA KUFANYIKA KAZI ZETU ZA USANII AMBAKO WATU WANATUTHAMINI NA KUTUUNGA MKONO. KAMA NI VITA RWANDA SASA VIMEKWISHA KWA HIYO NI NCHI POWA TU YA KUISHI. NA MATOKEO YA HICHI NINACHOKISEMA MTAYAONA BAADA YA MIEZI MITATU HADI SITA KUAZIA SASA KWANI MTATUSHUHUDIA AU KUTUSIKIA MMOJA BAADA YA MWINGIENE AU KIKUNDI KIMOJA BAADA YA KINGINE TUNAHAMIA ZETU RWANDA KUFANYA KAZI ZETU ZA USANII TUKUACHENI NA ROHO ZENU HIZO AMBAZO KUNA MDAU MMOJA HAPO JUU KAZIITA KUWA NI ZA KIUCHAWI. “I really mean what I am saying and you will see”.
ReplyDeletemimi nawapongeza wasanii wetu woote kwa kazi nzuri , ila mimi nina ushauri nataka kuwapa ni kuhusiana na miili yao wanajiachia sana MITUMBO HIYOO NA MAPAJA MPAJA JEANS ZINABANA !! HASA HUYO RAY NA SWAHIBA WAKE , JAMANI FANYENI MAZOEZI MUWE NA SIXPACK AU ANGALAU 2 PACKS SIO TUMBO HILOOOOO ... WAANAGALIENI CELEBRITY WENGINE DUNIA WANAVYOKEEP BODY ZAO...
ReplyDeleteni ushauri tu
mdau soko shimoni kariakoo
kumbuka usemi nabii hakubaliki Nyumbani, ukitaka kujua wewe una uwezo gani nenda ugenini, kisha ukirudi punguza presha utafanikiwa, watu wakishtuka, watakufuata na kusema uliweza wezaje?
ReplyDeleteHaiwezekani mkusanyiko wote huo wa Warwanda waliyowazunguka wasanii wetu uwe wote ni wa watu mambumbumbu na mahohehahe lazima miongoni mwao kuna wasomi wenye upeo mkubwa wa kupima mambo na kutofautisha kati ya kitu kizuri na kibaya na kati ya filamu nzuri na mbaya. Kujitokeza kwao kwa wingi kiasi hicho kuwapokea wasanii wetu kwa furaha kubwa kama hivyo kunaashiria kwamba wanawakubali wasanii wetu na filamu zao. Sasa inakuwaje Warwanda wawakubali sisi wenyewe Watanzania tusiwakubali? Jamani embu tuache roho mbaya. Ninachokuulizeni mimi hapa ni kitu kimoja kwamba, hao wasanii wetu (Kanumba, Ray, Auntie Ezekiel na Johari na wengine) wakiamua kuhamia huko Rwanda wanakokubaliwa sisi Watanzania tutakuwa tumepata nini? Ni lazima mjue kwamba walivyo wasanii wetu wanaotafuta mafanikio ni kama binaadamu wengine wowote wanaotafuta mafaanikio ambapo daima kilicho muhimu ni kupata mafaanikio bila kujali mafaanikio hayo yatayapatikania wapi, sasa kama wasanii wetu wataona mafaanikio yao yatapatikana kirahisi Rwanda wanakokubalika si wanaweza wakaamuwa kuhamia huko? Natamka maneno haya huku machozi yananitoka. Nakuombeni jamani tuache roho mbaya za kukatishana tamaa kwani kuna mtu aliyekamilika katika dunia hii???
ReplyDelete