Bendi maarufu ya muziki wa Dansi ya African Stars (Twanga Pepeta) watatoa burudani ya aina yake katika fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi jijini Mwanza Jumamosi, tarehe 4 Desemba.
Akizungumzia maandalizi ya Fainali hizo; Meneja wa Bia ya Balimi Fimbo Butallah alisema; Kimsingi maandalizi yote yamekamilika, na timu zote zitawasili jijini Mwanza kesho (Ijumaa) tayari kwa mpambano huu wa aina yake. Tutakuwa na timu tano toka kila kituo kilichoshiriki ngazi ya awali ikiwa ni pamoja na Kigoma, Kagera, Mara, Visiwa vya Ukerewe (UK) na wenyeji Mwanza.
Ili kunogesha zaidi burudani hizi, zitakazofanyika katika eneo la Mwaloni, bendi ya Twanga Pepeta itatoa burudani kwa mashabiki watakaohudhuria fainali hizi. Hivyo tunawaomba wakazi wote wa Mwanza na maeneo ya jirani kujitokeza kuja kupata burudani za mashindano haya ambayo kwa sasa ndiyo mashindano yenye mashabiki wengi zaidi katika kanda ya ziwa.
Mashindano yataanza saa 3 asubuhi hadi jioni.

hivi kwanini dar we don't have all these races???
ReplyDeletemwanza siku hizi burudani nyingi, musonye wa cecafa kazibaziba chalenji ifanyikie dar kwa kuweka masharti magumu mikoani sasa watu hawaingii badala yake wanaruhusu watu kuingia bure, wangekuwa ndio watu wa mwanza ungemsikia anavyolalamika lakini kwa vile ni wa dar kakaa kimya na tenga wake.
ReplyDeletembio za baiskeli, rockcity marathoni, mbio za mitumbwi na nafikiri baadaye kutakuja mbio za boti, hivi vyote vinatutosha kwa burudani kila mwaka tena havina viingilio.#
Bigup rockycity
mdau
uk