KATIBU WA TUME MR RAYMOND MAUKI AKITANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA WALIOPITISHWA NA TUME BAADA YA MCHUJO MKALI

Tume ya uchaguzi chini ya wizara ya sheria na katiba inawatangazia rasmi wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kama walivyopitishwa na tume baada ya kufanyiwa mchujo. Tume imezingatia vigezo vyote kama katiba ya ATSA inavyoelekeza.

Waliopitishwa ni kama ifuatavyo :
RAISI :-
1) ISSA M. MATIMBWA
2) SAIDI LUWE
3) KIKWEMBO MLEKWA

MAKAMU WA RAISI:-
1) AHMED KHAMIS
2) BEATRICE MALINGA
3) HAMIS KIDAGO

WAZIRI MKUU :-
1) MICHAEL MAGOTI
2) MUSA KIMATI

MWEKA HAZINA :-
1) IDD PILINGU
2) MWAJUMA SHABANI
3) BONIFANSIA BOZA
4) SELINA NDYAMBI

Tume inawatangazia uchaguzi utafanyika siku ya jumatano tarehe 22/12/2010 ukumbi wa TAIBA FOOD CENTRE kuanzia saa tano kamili asubuhi (NB.kama kuna marekebisho yoyote mtaarifiwa haraka iwezekanavyo.)

Kampeni zimeanza rasmi leo tarehe 18/12/2010 hadi siku ya kupiga kura .Tume inawatahadharisha wagombea kutotumia lugha chafu wala mbinu chafu kwa muda wote wa kampeni na pia tunawahakikishia wananchi wote kuwa uchaguzi utakuwa wa HURU NA HAKI.

Tume pia inawaomba viongozi wa kila jimbo kutoa ushirikano kwa kila mgombea iwapo itahitajika kufanya kampeni kwa wanachama wa jimbo husika.

Aina za kampeni zinazoruhusiwa ni kama :
:mikutano ya hadhara
:mawasiliano ya simu
:mabango
:picha
Vipeperushi n.k

Tume inapinga vikali matumizi ya pesa(RUSHWA) kama kishawishi kwa wapiga kura.hatua kali zitachukuliwa kwa yoyote atakaye kamatwa.

Mwisho,tunawatakia maandalizi mazuri ya uchaguzi na likizo njema.

IMETOLEWA NA

ISSA MALUKA-MWENYEKITI
RAYMOND MAUKI-KATIBU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...