Msemaji mkuu wa timu ya Waandishi wa Habari wa Afrika Mashariki,Fred Alocho akizungumza leo katika mkutano uliofanyia katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho la soka nchini TFF,wakati wakizungumzia maandalizi ya mechi yao dhidi ya timu ya Waandishi wa Habari wa Tanzania utakaochezwa siku ya Jumatatu ya tarehe 6 katika viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii,Kijitonyama jijini Dar.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Waandishi wa Habari Nchini,Majuto Omary.
Ofisa Mipango wa UAM (United Against Malaria),Bremen Leak akikabidhi Fulana zenye ujumbe wa kupiga vita Malaria kwa viongozi wa timu za Waandishi wa Habari ikiwa ni kama maandalizi ya mchezo wao wa kirafiki ikiwa ni sehemu moja wapo ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria kwa kupitia michezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mwenzenu sijaelewa, waandishi wa habari wa "afrika mashariki" na waandishi wa habari "wa tanzania" ina maana gani? kwani hao wa "afrika mashariki" ndani yake hakuna watanzania? kwani tanzania ipo afrika magharibi?kiswahili hiki jamani mbona kinatusumbua?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...