Naomba kutoa pongezi binafsi kwenda kwa Jumuiya Ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japan Kwa kufanikisha sherehe za Uhuru zilizofanyika jana (12.December.2010) kwenye ukumbi wa PPP hapo Sagamino, Kanagawa.

Mgeni rasmi alikuwa ni Mh. Balozi Mrs. Salome Sijaona, ambaye kwenye hotuba yake aliongela mambo mengi, ikiwemo kusisitiza Umoja miongoni mwa Watanzania wanaoishi nchini Japan. Na pia kuwakumbusha majukumu yao katika kuleta maendeleo ya Tanzania ambayo sasa imetimiza miaka 49 kwa upande wa Tanganyika.

Pia mgeni rasmi alifungua rasmi tovuti
hii ya Jumuiya ijulikanayo kwa jina la:
http://www.tanzanitesociety.jp

Watanzania wote mnaruhusiwa kujiunga
nayo kwa kutembelea tovuti ifuatayo:
http://www.tanzanitesociety.jp/ForumMemberProfile/register
ambapo utafanya Registration
ili kuweza kushiriki katika majadiliano mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...