Mkurugenzi wa kampuni ya Unique Entertainment,Methusule Magesse akizungumza katika mkutano huo pamoja na kuwatambulisha washiriki wa shindano ya Giraffe Unique Model katika hotel ya Giraffe Ocean View Jijini Dar leo.Kushoto ni Meneja Mwajili wa Giraffe Ocean View Hotel,Elsie Mntenga na kulia ni Mwalimu wa warembo hao,Hidaya Maeda
Warembo washiriki wa shindano la Giraffe Unique Model wakiwa katika mkutano huo.

UINQUE ENTERTAINMENT Kampuni inayoandaa shindano la GIRAFFE UNIQUE MODEL leo imeamua kutangaza majina ya warembo watakaoshiriki katika fainali za shindano hilo.

Warembo hao wako kumi (10) na wanatarajiwa kupanda jukwaani katika fainali za shindano hilo zitakazofanyika tarehe 24-12-2010 kwenye Hoteli ya Girrafe Ocean View iliyoko Kunduchi Beach.

Lengo likiwa ni kuwatambulisha pia majaji wetu ambao ambao kwa imani yetu tunaamini wataweza kutufanyia kazi nzuri itakayoturidhisha. warembo wenyewe pamoa ja mashabiki watakaohudhuria katika onyesho hilo

Washiriki wetu hao kumi ni Dora Mhando, Ritha Samwel, Bilkis Suleiman, Asia Dachi, Neema Purity Walele, Careen Suleiman, Caroline Mwakasaka, Diana Manason, Mariam Rabii na Jacline Jiabe.

Majaji wetu watakua ni Ally Rehemtulah, Miriam Gerald, Steven Kanumba, Victoria Martin na Asia Idarus

Pia tanapenda kuwatangaza wadhamini wetu kuwa ni Giraffe Ocean Vew Hotel, Robialack Paint, Global Publisher blog ya uniqueentertz.blogspot.com ambayo ndio inayotoa habari zetu kwa haraka zaidi na kuweza kuwafikishia wadau na Chanel Ten televisheni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hivi haya mambo ya kuanika dada zetu tanzania kwa kusingizia miss wa hiki na kile ni miezi 12 kwa mwaka?

    Naona kila shindano moja likisha jengine linafuata. Seuze mwakani brother michuzi akaanzisha miss wa blog ya jamii :(

    ReplyDelete
  2. mdau wa Wed Dec 01, 04:51:00 PM, umesema kweli.

    ReplyDelete
  3. Asante Mkubwa.

    Usisahau tu lile ombi letu Wakubwa wenzio.

    Asante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...