
Bi. Mary Mwangisa, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala, Utumishi na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akimkabidhi ua Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Waziri wa Wizara hiyo mara alipowasili ofisini hapo kuanza kazi rasmi leo. Wengine wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Wizara hiyo.

Bi. Mary Mwangisa, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala, Utumishi na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akimkabidhi ua Mhe. Charles Kitwanga (Mb), Naibu Waziri wa Wizara hiyo mara alipowasili ofisini hapo kuanza kazi rasmi leo. Wengine wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Wizara hiyo.

Dkt. Florens Turuka (aliyevaa miwani), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akimkabidhi ua Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri aliyeteuliwa kuongoza Wizara hiyo ikiwa ni ishara ya kumkaribisha ofisini hapo.


Prof. Makame Mbarawa (Mb), Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akitia saini kitabu cha wageni mara alipowasili ofisini kwake wizarani hapo leo kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais Kikwete kuongoza Wizara hiyo.

Mhe. Charles Kitwanga (Mb), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akitia saini kitabu cha wageni mara alipowasili kwa mara ya kwanza ofisini kwake Wizarani hapo leo baada ya kuteuliwa na Rais Kikwete kushika wadhifa huo.
Mkuu asante kwa kutuhabarisha....ila leo ni tarehe 01.12.2010 si november tena...mwaka kwisha.
ReplyDeleteNaona waheshiwa wote walikuwa na shauku ya kupiga picha huku waksign kitabu cah wageni, maana wote nawaona wameikazia macho kamera ya michuzi sijui walihesabiwa, 1,2,3 piga.
ReplyDeleteHaya mambo ya siku hizi. Zamani zile utaona picha kwenye gazeti la Uhuru Mwalimu J K Nyerere kasimama upande mmoja upande mwingine yupo Mzee Timothy Apiyo Upande mwingine anayeapishwa kashika kitabu mkono juu. Halafu hakuna tabasamu wala vicheko wala dhifa dhifa na tafrija tafrija. Halafu hakuna cha waifu, hazibandi wala watoto wala mashosti wala baba wala mama ndani ya viwanja vya Ikulu. kwenye geti la Ikulu kulikuwa na tangazo la mkwara linasema IKULU NI UWANJA WA FARAGHA.
ReplyDeleteMawaziri walikuwa wanaziogopa nyadhifa zao kwa sababu kulikuwa na kazi za kufanya. Ukipewa Ulinzi kuna kulinda nchi na kusaidia FRELIMO, SWAPO, ZANU, ZAPU, ANC, PAC, MPLA nk. Ujenzi na Uchukuzi kuna kushughulikia MECCO, ATC,TRC, TAZARA, SINOTASHIP, BANDARI, UDA, KAMATA nk. Elimu vere vere bize na TTC na kutengeneza mitaala ya itikadi za kijamaa. Utumishi lazima kichwa kikuume kuwaandalia post magraduate wa UDSM, MZUMBE, Uhazili Tabora, nk. Madini lazima abalance mambo ya STAMICO na kumonitor mambo ya Mwadui Williamson Diamond Mines. Nchi za Nje huko ni diplomasia kwa kwenda mbele Tanzania ipo kimbelembele kwenye kila kitu. Bongo anatua Queen Elizabeth akipishana airport na President Leonid Brezhnev next week anakuja Rais Tito wakipishana Fidel Castro huku tunamsubiri Nikolai Ceausescu halafu anakuja General Olesegun Obasanjo the same week akipishana Norman Manley akifuatiwa na Pierre Treadue na Deng Xiao Ping, William Tolbert na Siaka Steven wapo kwenye waiting list garademshit! Wizara ya Utamaduni, Michezo na Vijana iko vere bize na kikundi cha Taifa na kuwaweka sawa kina Filbert Bayi, Mwinga Mwanjala, Suleiman Nyambui, Gidamas Shahanga na wenzao wengine kwenda kunyakua medali Christchurch au Moscow au kugomea na kuathiri Commonwealth au Olympic Games for South Africa,s sake!
Hiyo ilikuwa zamani. Siku hizi kuna nini?
bwana michuzi embu siku nyingine bwana uwe unakata hizo LEBO kwa waheshimiwa hao, usiwe unakubali kupiga picha za hivyo inatia aibu
ReplyDeletewaziri mzima kweli anavaa suti na LEBO kweli jamani.. embu waambie hii haifai bana..inakera
Hongera sana ndugu Kitwanga tunakutakia kila la kheri ktk utendaji na utekelezaji wamajukumu ulokabidhiwa na wananchi. Ni mimi Classmate wako Same Sec school.
ReplyDeleteha ha haaaaa. anony wa tatu nimekulovee!!!
ReplyDeleteJamani Sayansi na Technolojia Waziri hana Computer.
ReplyDeleteTehe tehe tehe te he Anon wa tatu unachambua balaa, hata siye tuliyekuwa hatujakuwa tumejua kilichojiri. Big up kaka/dada
ReplyDelete