Mhe. Dk.Emmanuel J. Nchimbi
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Emmanuel J. Nchimbi (Mb) anatoa pongezi za dhati kwa Baraza la Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la ‘Challenge’ kwa mwaka 2010.
Aidha, anaishukuru CECAFA kwa uamuzi wake wa kuwaruhusu washabiki na wapenzi wa soka kuingia bure katika michezo ya hatua ya wali ili kushangilia na kupata burudani.
Katika kuunga mkono jitihada hizo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imefanya jitihada za kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kupata burudani kwa kuwapatia wadhamini wa kuchangia gharama za uendeshaji wa michuano hiyo, hivyo kuwezesha watazamaji na wapenzi wa soka kupata unafuu wa kuingia uwanjani.
Wizara inaishukuru na kuipongeza Kampuni ya Vodacom kwa kukubali kuchangia gharama za michezo kuanzia hatua ya Robo Fainali ili wananchi, washabiki na wapenzi wa soka waweze kuiona kwa gharama nafuu zaidi.
Mwisho, Wizara inawashukuru pia wadhamini wakuu wa mashindano hayo ‘Tusker Lager’ kwa kuwezesha michuano hiyo kufanyika hapa nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...