Mama Salma Kikwete

NA MWANDISHI MAALUM

MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete, amesema elimu ni nyenzo muhimu katika kupambana na umasikini.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizindua mafunzo ya uuguzi katika Taasisi ya A3 ambayo ni taasisi dada ya shule za Al Muntazir.

Mama Salma, alisema miongoni mwa mambo yanayotofautisha nchi zilizoendelea na zinachoendelea ni kiwango cha elimu.

“Hii ni kwa sababu utajiri na mali havijileti vyenyewe kwa mtu, ni matokeo ya mambo mengine ikiwemo elimu. Kiwango cha elimu na ujuzi ndicho kinachotofautisha nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea,” alisema.

Alifafanua kwamba, kwa kadri kiwango cha elimu, ujuzi na maarifa kinavyokuwa juu, ndivyo na maisha ya watu katika nchi husika yanavyokuwa bora.

Kutokana na sababu hiyo, alisema, serikali imeamua kuwekeza katika elimu, na katika hotuba ya kuzindua Bunge hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete alisisitiza kipaumbele ni elimu.

Mama Salma alisema, ujenzi wa shule za sekondari katika kila kata, na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho kimeshaanza kutoa wahitimu, ni uthibitisho wa dhamira ya dhati ya serikali katika kuinua elimu nchini.

Mama Salma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), alisema katika juhudi ya kuinua kiwango cha elimu na ujuzi nchini, ndipo nafasi ya mwanamke katika jamii inatambulika.

“Nilianzisha WAMA kutokana na shauku na hisia zangu katika kumuendeleza mwanamke wa kitanzania. Nataka kuona nchi yetu inaendelea, kwa sababu hii, wanawake wa nchi yetu wanahitaji kuelimishwa na kuwezeshwa,” alisema.

Mama Salma alisema inatia moyo kushuhudia ongezeko la taasisi za elimu ya juu nchini, ikiwemo hiyo ya A3.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Reading this News, Naona Huko nyumbani Private Sector are really Boosting government initiatives. Well DONE A3.
    Lakini A3 maana yake nini??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...