Dr. Bilal Philips (Dr. Abu Ameenah Bilal Philips) mzaliwa wa Jamaica na raia wa Canada atawasili Dar es Salaam, Tanzania, Ijumaa ya Desemba 17, 2010.

Dr. Bilal amealikwa na Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wataalam wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO). Madhumuni ya ziara ya Dr. Bilal ni kufanya kazi ya Daw’ah kuanzia Desemba, 17 mpaka 24, 2010, katika jiji la Dar es Salaam, Morogoro mjini na Zanzibar (Unguja).

Watanzania wa makundi mbalimbali wanakaribishwa kuhudhuria mikutano mikuu kama inavyoelezwa hapo juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Asante sana kaka michuzi kwa taarifa hizi huyu dr mi huwa naangalia tu mahubiri yake kwenye tv haswa ile channel ya peace tv. mimi ni mkristo ila jamaa namkubali sana kwa kile anachohubiri si kama wahubiri wengine wanaopoteza muda kwa kuhubiri mambo ya kufikirika tu na yasiyokuwa na msaada katika maisha yetu ya sasa na kila siku! Hakika sintokosa!

    ReplyDelete
  2. dah!napenda nıngemuona dr bilal ila nipo mbali,naomba mfanye juhudi ya kumalıka USTADH NAPOLIA ALIYEKUWA MSHIRIKI MKUBWA WA 2PAC ENZI ZILE WAKIWA KTK KUNDI LA OUTLAWS..nawatakıa mahubıri mema.

    ReplyDelete
  3. Woooh Welcome to TZ Dr Bilal. Kwa kweli ni rare opportunity.....!!! Na topics zake zimekaa sawa kweeli. Hii itakuwa fungua mwaka ya mwaka. jamaa ni mkali sana....!!!

    ReplyDelete
  4. jamani haya matukio yetu waislamu mbona mmeng'ang'ania DSM tu sisi wa mikoani mmetuvua uislamu?? Kwa kweli mtatufanya tusafiri kwa jambo hili inshaallah.

    ReplyDelete
  5. Halima AbeidDecember 14, 2010

    Jamani Dr. Bilal. Aaah msikose kututumia mikanda yake sisi wa huku UK waislamu wenzenu. Aaah, ingekuwa hip hop ni kama vile aje a big superstar.

    ReplyDelete
  6. Oh raha ilioneje kumuona live mhubiri huyu,thak you michuzi na chuo kilichomualika.

    ReplyDelete
  7. hii ni dunia ya science and technology. taasisi ya elimu ya juu inapaswa kujielekeza kuleta wataalamu wa fani hiyo ili watanzania tuweze kuchota from their experience. mahubiri ya dini hayasaidii sana wakati katika zama hizo.

    ReplyDelete
  8. Mashallah...huo ndo wakati wa kujifunza waislamu mzilaze damu...maswali ya kutofautiana kiitikadi, Akida etc...huyu ni miongoni mwa watu wenye exposure ya kutosha ya dunia...so mtumieni vizuri Mlioko Tanzania. Mdau Ughaibuni.

    ReplyDelete
  9. Michuzi hiyo picha mbona haionekani mpaka u click. Tunataka watu waione

    ReplyDelete
  10. Dr. Bilal Philips (Dr. Abu Ameenah Bilal Philips) mzaliwa wa Jamaica na raia wa Canada atawasili Dar es Salaam, Tanzania, Ijumaa ya Desemba 17, 2010. Dr. Bilal Philips alikuwa Mkristo na mwaka 1972 alisilimu na kuwa Muislamu. Dr. Bilal ni msomi mashuhuri duniani wa ngazi ya PhD, aliyoipata Chuo Kikuu cha Wales, Uingereza. Shahada yake ya kwanza (B.A) ya fani ya Elimu ya Dini ya Kiislamu aliipata Chuo Kikuu cha Madina.

    Dr. Bilal amealikwa na Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wataalam wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO). Madhumuni ya ziara ya Dr. Bilal ni kufanya kazi ya Daw’ah kuanzia Desemba, 17 mpaka 24, 2010, katika jiji la Dar es Salaam, Morogoro mjini na Zanzibar (Unguja). Katika kazi hiyo ya daw’ah atafanya muhadhara siku ya Jumamosi, Desemba 18, 2010, kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana, katika ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia, Dr. Bilal atafanya muhadhara Siku ya Jumapili, Desemba 19, 2010, saa 2.00 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana, katika ukumbi wa Diamond Jublee, Dar es Salaa. Siku ya Jumatatu, Desemba 20, 2010, saa 10.00 asubuhi mpaka saa 6.30 mchana, Dr. Bilal atafanya muhadhara Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro. Akiwa Morogoro, Dr. Bilal atatembelea miradi ya The Islamic Foundation ambayo ni pamoja na Redio Iiman, Kituo cha Yatima na Shule ya Dar Alqam.

    Siku ya Jumanne, Dr. Blala atarejea Dar es Salaam na kutembelea Ofisi ya Muft wa Tanzania, Sheikh Issa bin Shaban Simba, Ofisi ya Sheikh Musa Kundecha, Sheikh wa Baraza Kuu. Siku hiyo hiyo ya Juamanne, kuanzia saa 8.00 chana, Dr. Bilal ataanza kuendesha semina kwa watu wanaofanya kazi ya Daw’ah, kutoka Bara na Visiwani, katika moja ya shule za Kiislamu. Jumatano, Desemba 22, 2010, kuanzia saa 1.00 asubuhi mpaka 6.00 mchana, Dr. Bilal ataendelea na semina.

    Jioni ya Jumatano hiyo hiyo atakwenda Zanzibar ambapo atafanya mihadhara miwili. Muhadhara wa kwanza ni Alhamisi, Desembna 23, 2010, kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana, katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Chukwani. Mchana wa siku hiyo hiyo atatembelea Ofisi ya Muft wa Zanzibar, Redio Nuur na Shule inayomilikiwa na UKUEM. Jioni ya Alhamisi, Dr. Bilal atafanya muhadhara wa pili, kuanzia saa 10.30 mpaka 12.oo jioni, katika Chuo Kikuu cha Serikali cha Zanzibar (SUZA). Dr. Nbilal atakuja na mke wake ambae nae alisimu, Dada Sara.

    Ziara yote ya Dr. Bilal itarushwa hewani live na kituo cha Redio Iiman cha mjini Morogoro, kinachomilikiwa na The Islamic Foundation. Pia ziaran hiyo itarikodiwa na kuzaliwa DVD, CD, n.k. – insha Allah. Waislamu na Wasiokuwa Waislamu, wote mnakaribishwa katika mihadhara iliyoelezwa hapo juu.

    Wasalam, Sharifu Muhammed, Mratibu wa Ziara ya Dr. Bilal. Mawasiliano zaidi piga: 0716-776226, , 0655-003744, 0655-654900, 0767-127718, 0754-208585.

    ReplyDelete
  11. mbona hapo mimi sijaelewa ISLAMIC SCHOOL ndio wapi?.big up Mwl.PAZI ila yuko wapi jita wako MWL.SAIBOKO?Kwa kweli nimependa sana kuona wailsamu wa Tanzania wanaanza kupiga hatua kama hizo huo ni mwanzao mzuri pia msisahau kumleta SHEIKH.SUDESSI.

    ReplyDelete
  12. Mimi nilikua nawaomba wamlete yule gwiji wa midahalo ya islam and comparative religion Dk. Zakir Naik

    ReplyDelete
  13. Controversies
    In an interview given, Philips accused the Australian authorities of "blindly following American allegations and unsubstantiated false accusations" claiming that investigations in the UK, Canada and Australia had found no evidence that he was in any way connected with terrorism.[2]. In this interview, he also pointed out that he had not entered the USA since 1995, characterizing media claims that he had been deported in 2004 as an "outright lie". Philips also called the statement that he was an "unindicted co-conspirator” in the 1993 World Trade Center bombing "really a joke", claiming that it was based on a "supposedly leaked report" of over 100 prominent Muslims who were never charged. His response to the issue is posted on YouTube as "Bilal Philips replies on Australian Visa denial".
    Source:
    http://en.wikipedia.org/wiki/Bilal_Philips

    ReplyDelete
  14. ni bahati ya kujivunia. huyu ni GOGO SI MCHEZO. Masheikh kwama hao wanakuwa tight sana na schedules zao kuwapata sio mchezo wala rahisi.

    ReplyDelete
  15. SASA NYIE WANYATURU NA WADENGELEKO, KWELI MTAMWELEWA HUYO JAMAA AKIPIG STOR ZAKE KWENYE KIINGILISHI NA KIARABU?AU NI KUMWONA SURA TU!

    ReplyDelete
  16. Mi nilikuwa naomba wafungue tv au website kama ile ya Eddie wa kule chicago.T he Deen show it's way of life(www.thedeenshow.com)

    ReplyDelete
  17. mdau wa Tue Dec 14, 06:27:00 PM pole sana, humdanganyi mtu ila unajidanganya nafsi yako.

    ReplyDelete
  18. The deenshow it's away of life(www.thedeenshow.com)

    ReplyDelete
  19. Huyu sheikh ana website yake (www.bilalphilips.com)

    ReplyDelete
  20. Alhamdullillahir Rabiliallamiin
    Sasa WaTZ tunaanza kuamka Kidini,sio huyo asokuwa na dini Tue Dec 14 05.27 naona hana Dini huyo,na asiwe karibu na wanaomcha Mungu kwani yeye Bila Mungu kukupa huwo uhai hiyo Dunia ya science na technology utaishuhudia wewe!Kaa chini ufikilie uko hapa kwa uwezo wake Mola bila yeye wewe ni nothing,,,,,Waislam wa Bongo jitahidini hasa wenye uwezo kuwaleta wasomi kama huyo Dr Bilal na wengine na wengine wengi tu kina Zakir Naik,,ili kuendeleza uislam wa TZ na waislam kusonga mbele!Ingawa waTZ walio wengi hatujui Lugha nina iman wakaliman wako Full kututafsilia, kwani kiingereza sio tija,ili mladi unamcha Mungu ipasavyo,,,Kila la KheriWaTZ,,,

    ReplyDelete
  21. Viwanja vyote vilivyotajwa ni vidogo kwa eneo, ilitakiwa apelekwe sehemu kama Biafra, Jangwani au Mnazi Mmoja. Na kuwe na mkalimani wa ukweli. Mara nyingine tulifikirie hilo.
    -Said Mandevu

    ReplyDelete
  22. Watanzania wenzangu msiipoteze bahati hii..wallah kama ningekua tanzania nadhan ningekua wa kwanza kuingia kwenye lango la DIAMOND kwani mi huyu jamaa ni miongoni wa wahubir ninao wakubali na naishia kuwaona kwenye internet tu..Inshallah wanaohusika na kuwaleta mashekh basi wafanye pia mpango wa kumshusha Tanzania Amir Muhadith(Loon)ambae alikua kwenye kundi la bad boys na kina p diddy na Napole aliekua na 2pac...Waislam na wasio waislam wa tanzania tumieni hiyo ni nafasi kubwa mmeipata..nasi wa huku mbali tunamuomba Nuurdin Kishk atutembelee..Tafadhal kaka Michuzi nifikishie Ombi langu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...