Na Alpha Natai & Issa Sabuni

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amefanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Bwana Kocheril Velayudhan Bhagirath na kumueleza kuwa nchi yake imeamua kuisaidia Tanzania fedha, kiasi cha dola 92,000 za Kimarekani ambazo zitaelekezwa kwenye miradi ya Kilimo katika kutekeleza azma ya KILIMO KWANZA.

Balozi huyo wa India nchini aliwasilisha nakala ya barua iliyotoka kwa Waziri Mkuu wa India kwa Waziri Maghembe na kumueleza kuwa barua hiyo pia amemfikishia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda kumfahamisha kuhusu msaada huo wa fedha.

Aidha, Balozi Bhagirath alimweleza Waziri Maghembe kuwa India imeifanya Tanzania kuwa nchi ya pili kwa kuipatia udhamini wa wanafunzi wa Elimu ya Juu kwenda kusoma nchini humo na kwa mwaka wa masomo wa 2010/2011 jumla yake imefikia wanafunzi 196 nyuma ya Afghanistan.

Balozi Bhagirath aliongeza kuwa nchi yake ipo mbioni kuanzisha kituo kikubwa cha kuzalisha mbegu za mazao ya nafaka ambayo ni mpunga na mahindi chini ya Mpango wa Export Processing Zones (EPZ) na kwamba eneo limeshapatikana huko Bagamoyo mkoani Pwani.

Waziri Maghembe alimshukuru Balozi Bhagirath kwa niaba ya India na kumuakikishia kuwa Tanzania ipo mstari wa mbele katika kushirikiana na India katika maeneo yote yanayolenga kukuza na kuendeleza kilimo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Now you have totally confused me! Hizi fedha ($92K) ni kwa ajili ya "miradi" ya kilimo, na hapohapo india "ipo mbioni kuanzisha kituo kikubwa cha kuzalisha mbegu..." Je,hizi pesa ni kwa ajili ya kulipia eneo (shamba) huko Bagamoyo, ni kwa ajili ya kukopesha mkulima mwingine (muhindi), au ni kwa ajili ya miradi tofauti na huu wa mbegu za mazao?! Kwani tunashindwa kuhifadhi mbegu zetu wenyewe hadi tuletewe wataalam (wababaishaji) toka India?
    Tanzania tuna mpunga/mchele mzuri kuliko hata ule wa Taiwan/China, badala ya kuhakikisha kuwa tunazalisha zaidi na kuuza nchi za nje, tunaleta mhindi atusambazie mbegu za 'basimati'.... Be Serious!!!

    ReplyDelete
  2. We mtoa maoni wa Sun Jan 16, 01:54:00 AM 2011, kwanza unapewa msaada, ikisha unakashifu na kuwa mbaguzi. Sasa kama mnayo mawazo mazuri mbona mmekaa tu siku zote mnasubiria nini? Kama wataalamu tunao basi tuzalishe.. sio tumekaa tuu.. mkipewa misaada mnakwenda mbio kuichukua...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...